|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) alipomwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jijini New York nchini Marekani. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA). |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto) Waziri wa Nchi Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa Zanzibar Mhe. Masoud Ali Mohammed , Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu na Mama Dionisia Mpango Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais Dkt. Mpango katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijijini New York nchini Marekani
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania inaamini diplomasia na
meza za mazungumzo ni chombo bora cha kutatua migogoro duniani na kwamba nchi
zina wajibu wa kuzingatia utatuzi wa migogoro kwa njia za amani ili kulinda
ustawi wa watu watu na kuepuka athari zinazoweza tokana na migogoro duniani.
Mhe. Dkt. Mpango amesema hayo jijini
New York alipohutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) alipomuwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
“Tanzania inaamini kuwa diplomasia na
meza za mazungumzo ndiyo chombo muhimu na ni vitu vikuu vya kuzingatia wakati
wa kutatua migogoro duniani, Mataifa
yanapaswa kuzingatia kuwa yanahaki na wajibu wa kulinda maisha ya binadamu hasa
watoto na wanawake lakini pia lazima wahakikishe ustawi wa watu wote , ni
muhimu kutafuta suluhu au kutatua migogoro
kwa njia za amani, hii inasaidia kuepuka athari zitokanazo na migogoro hiyo
kama vile ongezeko la bei za chakula na mafuta na kushuka kwa uzalishaji wa
kilimo na viwanda duniani kote,“ alisema Dkt. Mpango.
Makamu wa Rais pia amepongeza juhudi
za Umoja wa Mataifa katika kukuza lugha mbalimbali duniani ikiwemo tamko la
kihistoria la Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi (UNESCO) lililoitaja
"7 Julai" kuwa Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani na kuwezesha lugha
hiyo kuadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani na hivyo kuitambua arsmi kimataifa.
Amesema Tanzania inajivunia kushiriki
katika shughuli za kulinda amani ambapo imechangia Askari katika misheni 5 kati
ya 16 zilizopo za kulinda amani duniani na kuahidi kuwa itaendelea kuchangia zaidi iwapo itaombwa
kufanya hivyo na kuiomba Umoja wa Mataifa kuongeza uungaji mkono wake kwa
juhudi za kikanda katika za kujenga na kulinda amani.
Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Dkt.
Mpango amesema nchi za Afrika zinahitaji mabadiliko ya haki na utaratibu katika
kufikia matumizi ya nishati mbadala kwa kuzingatia hali za Maisha ya watu wa
bara hilo wenye changamoto mbalimbali za upatikanaji wa nishati hizo na kutoa wito
wa kuondolewa kwa upinzani dhidi ya ufadhili wa kimataifa katika utekelezaji wa
miradi ya mageuzi katika nchi za Afrika ambayo inalenga kutumia rasilimali
ikiwemo gesi kwa ajili ya nishati na matumizi mengine katika kufikia maendeleo.
Amesema biashara ya hewa ukaa barani
Afrika inapaswa kufanyika kwa uwazi na kuwanufaisha wananchi waliotunza
mazingira na misitu inayozalisha hewa hiyo kwa matumizi ya dunia na kuongeza
kuwa Tanzania ni moja ya iliyowekeza zaidi katika uhifadhi wa misitu ambapo
asilimia 30 ya eneo la ardhi ya taifa hilo imehifadhiwa.
Kuhusu mapambano ya ugonjwa wa COVID 19, Dkt.
Mpango amesema amezishukuru nchi na jumuiya za kimataifa zilizoshirikiana na Tanzania
kupambana na janga hilo kuanzia utoaji wa vifaa vya uchunguzi, dawa, programu
za msaada wa chanjo, ambazo zimekuwa muhimu katika kushinda vita dhidi ya janga
hilo na kuwezesha nchi kufikia asilimia 60 ya kuchanja watu wake hadi sasa na
kuongeza kuwa kuchelewa kwa Afrika kupata chanjo za ugonjwa huo kunasisitza
hitaji la Nchi za Kiafrika kufanya kazi pamoja katika ukuzaji wa masuluhisho
asilia kupitia utafiti wa pamoja wa kisayansi.
Ametoa wito kwa mataifa kuweka
vipaumbele vya vitendo hasa kwenye malengo ya maendeleo endelevu ambapo
amayasihi mataifa kujitolea kufanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa na Nchi
Wanachama wake, kwa nia ya ushirikiano na mshikamano wa kimataifa kuelekea
mustakabali endelevu.