Saturday, October 6, 2012

Mkutano kati ya Waziri Membe na Waandishi wa Habari kuhusu mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akifafanua kwa  Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu hoja zilizotolewa na Serikali ya Malawi za kujitoa katika mazungumzo kuhusu mgogoro uliopo kati  ya Tanzania na Malawi kuhusu Ziwa Nyasa. Wengine katika picha kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule  na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju.

Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Vyombo na Mashirika mbalimbali ya Habari hapa nchini wakimsiliza kwa makini Mhe. Waziri Membe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (aliyesimama) wakati akimkaribisha Mhe. Waziri Membe kuzungumza na  Waandishi wa Habari (hawapo pichani).

Mmoja wa Wanahabari  Bw. Florian Kaijage akiuliza swali wakati wa mkutano wao na Mhe. Waziri Membe.

Mhe. Waziri Membe akijibu swali kwa msisitizo aliloulizwa.

Mhe. Waziri Membe (waliokaa kushoto) akionesha kwa Waandishi wa Habari Ramani mpya ya Tanzania. Wengine katika picha (aliyekaa kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule akifuatiwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Selasie Mayunga na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria hapa Wizarani Balozi Irene Kasyanju.

Mhe. Waziri Membe akifafanua kwa Waandishi wa Habari kuwa mpaka katika ramani ya Tanzania umepita katikati ya Ziwa Nyasa na si ufukweni kama inavyodaiwa na Malawi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule,  akimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Membe wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiririkiano wa Kimataif, Balozi Irene Kasyanju akiwa makini kusikiliza ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mhe. Waziri Membe kwa Waandishi wa Habari kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi juu ya Ziwa Nyasa.

Wageni waalikwa na baadhi ya waandishi wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe.

Friday, October 5, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kesho Jumamosi tarehe 6 Oktoba, 2012 atafanya Mkutano na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Mikutano hapa Wizarani.  

Suala kuu litakalozungumzwa ni mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi.

Mkutano huo utaanza saa tano kamili katika chumba namba 27.


 

Imetolewa na:

 Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Dar es Salaam.

5 Oktoba, 2012


Tanzania Diaspora Conference in Canada

 
 
 

logosm

Tanzanian Diaspora Conference in Canada:
Tanzania Engaging the Diaspora, A Win-Win Strategy

Edmonton, Alberta, October 5-7, 2012

Venue: Fantasyland Hotel
17700-87 Avenue
Edmonton, AB T5T 4V4 Canada 

  

Conference Chair: Deogratias Nondi Conference Co-Chair: Dr. Zaheer Lakhani

CHIEF GUEST: His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania
SPECIAL GUEST: Mr. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation of the United Republic of Tanzania
 
 
 
For more information, please visit:
 
 
 
 
 

Hafla ya Kumuaga Balozi wa Cuba hapa Nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akihutubia wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Cuba aliyemaliza muda wake hapa nchini, Mhe. Ernesto Gomez Diaz. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Double Tree, Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Cuba aliyemaliza muda wake hapa nchini, Mhe. Ernesto Gomez Diaz naye akizungumza machache wakati wa hafla hiyo.

Mhe. Naibu Waziri akiwa na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo. Walio pembeni ya Mhe. Naibu Waziri, kulia ni Mhe. Juma Mpango, Mkuu wa Mabalozi na kushoto ni Mhe. Diaz, Balozi anayeondoka.

Mhe. Balozi Diaz akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mhe. Naibu Waziri.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Grace Shangali akitoa neno la ufunguNzi wa hafla ya kumuaga Balozi wa Cuba.

Mhe. Naibu Waziri akiagana na Balozi Diaz mara baada ya hafla kumalizika.


Hon. Membe, Chief Secretary Sefue in a group photo



Hon. Bernard K. Membe (MP), (2nd left), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation in a group photo with Chief Secretary H.E. Ambassador Ombeni Y. Sefue (right), Ambassador Liberata Mulamula (2nd right), Senior Advisor to President Kikwete (Diplomatic Affairs) and Deputy Ambassador Ramadhan Muombwa Mwinyi (4th left), Deputy Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations.  The group was waiting to receive H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania in New York on 1st October, 2012 during his official tour in the United States of America and later his State Visit in Canada.



Photo by Mrs. Maura Mwingira of Tanzania Mission to the United Nations 



Thursday, October 4, 2012

Mama Maria Nyerere, Balozi Mujuma wazuru kaburi la Hayati Mama Betty Kaunda



Mama Maria Nyerere akiweka maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mke wa Rais wa Kwanza wa Zambia, Marehemu Mama Betty Kaunda. Mama Kaunda alizikwa tarehe 28 septemba 2012, mjini Lusaka, nchini Zambia.  Aidha, Mwili wa Marehemu Mama Kaunda ulizikwa kwenye shamba ambalo ni eneo alilozikwa Mmewe, Hayati Dkt. Kenneth David Kaunda.  Kushoto ni Mhe. Balozi Grace Joan Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia.   

 

Wednesday, October 3, 2012

Ziara ya Rais Kikwete nchini Canada


Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikagua gwaride rasmi katika Viwanja vya Jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada. 


Rais Kikwete akitambulisha ujumbe wa Tanzania, uliomjumuisha Mhe. Bernard K. Membe (MB) (pichani akisalimiana na Gavana Jenerali Johnson), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, katika Viwanja vya Jumba la Rideau Hall jijini Ottawa.  Jumba hilo pia ni makazi na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangu mwaka 1867, ambalo hutumika kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema.  Aidha, Jumba hilo ni sehemu ya mapokezi ya wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo mahala Gavana Jeneralia anapofanya shughuli zote kitaifa akiwa kama Mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.


Rais Kikwete akisalimiana na Watanzania waliojitokeza kumpokea.


Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika mazungumzo na Mhe. David Johnson, Gavana Jenerali wa Canada.  Mhe. Rais Kikwete alikuwa nchini Canada kwenye ziara rasmi ya siku mbili, mjini Ottawa.


Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Mhe. Bernard K. Membe (MB) (kulia kwa Rais), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa katika mazungumzo na Gavana Jenearli Johnson wa Canada. 


Rais Kikwete awasili Canada kwa ziara rasmi ya Kiserikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Ottawa, Canada, Jumatano mchana, Oktoba 3, 2012, kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Gavana Jenerali Mheshimiwa David Johnston.
Rais Kikwete na ujumbe wake wamewasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Macdonald-Cartier wa mji mkuu wa Canada wa Ottawa kiasi cha saa nane na dakika 55 mchana baada ya safari ya ndege ya saa moja kutoka mjini New York, Marekani, ambako amefanya ziara ya siku mbili pia.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Ottawa, Rais Kikwete amelakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mheshimiwa John Baird, Balozi wa Tanzania katika Canada, Mheshimiwa Alex Masinda, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mheshimiwa Deepak Obhrai, Balozi wa Canada katika Tanzania, Mheshimiwa Robert Orr na Mbunge Mheshimiwa Joe Daniel.
Miongoni mwa viongozi wengine walimpokea Rais kwenye Uwanja wa Ndege huo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe na Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Sospter Muhongo ambao wametangulia kuja Canada lakini ni sehemu ya ujumbe wa Rais Kikwete kwenye ziara hiyo.
Kwenye Uwanja wa Ndege huo, Rais Kikwete pia ameweka saini kwenye kitabu cha kumkaribisha rasmi Canada.
Kutoka uwanja wa ndege, msafara wa Rais Kikwete umekwenda moja kwa moja hadi kwenye Nyumba ya Serikali, ambako Mheshimiwa Kikwete ametoka kwenye gari na kuingia kwenye gari maalum linalovutwa kwa farasi na kuelekea kwenye Viwanja vya Jumba la Rideau ambako amepokelewa rasmi, kwa mbwembwe zote za Ziara Rasmi ya Kiserikali.
Mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Jumba la Rideau, Rais amepokelewa na Gavana Jenerali Johnston na mkewe, Mama Sharon Johnston, amepewa heshima ya kupigiwa mizinga 21 na pia amekagua Gwaride la Heshima la Majeshi ya Ulinzi ya Canada.
Katika hotuba fupi kwenye sherehe hiyo ya mapokezi ambayo pia imehudhuriwa na Watanzania wanaoishi Canada, Rais Kikwete ameishukuru Canada kwa misaada mingi ya maendeleo ambayo imechangia sana katika jitihada za Tanzania kujiletea maendeleo tokea uhuru mwaka 1961.
Akizungumza wakati akimkaribisha Mheshimiwa Kikwete, Gavana Jenerali amemshukuru Rais Kikwete kwa kukubali kufanya ziara hiyo ambayo iliahirishwa mapema mwaka huu kutokana na ajali ya meli M.V. Skargit iliyozama kwenye pwani ya Zanzibar na kupoteza maisha ya watu.
Amesema Gavana Jenerali Johnston: “Nafurahi sana umeweza kupata muda wa kuja kututembelea Mheshimiwa Rais na ninayo heshima sana kukukaribisha kwenye Jumba la Rideau, nyumbani kwa wananchi wa Canada.”
Ameongeza: “Tumekuwa na uhusiano mzuri kwa miaka mingi na kwa hakika hizi ni nyakati za kusisimua na zenye changamoto nyingi kwa nchi zetu mbili ambazo zinaendelea kujenga jamii zenye uvumilivu na za kidemokrasia.”
Mara baada ya sherehe za mapokezi, Mheshimiwa Kikwete na mwenyeji wake wamefanya mazungumzo ya kiasi cha dakika 40 kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuhusu masuala ya kimataifa.
Jumatano usiku, Oktoba 3, 2012 Gavana Jenerali Johnston ameandaa dhifa ya kitaifa kwa heshima ya Rais Kikwete kwenye Jumba la Rideau.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

4 Oktoba, 2012



VIFO VYA AKINA MAMA HAVIVUMILIKI-JK‏



Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na  Bw. Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mjini New York, nchini Marekani.  Rais Kikwete alikutana na Bw. Ki-moon kwa ajili ya mazungumzo ya namna kuendeleza ushirikiano, hususan katika masuala ya Mama na Watoto.


Mhe. Rais Kikwete akisaini kitabu cha wageni. 


Mhe. Rais Kikwete (wa tatu kushoto), akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon.  Wengine ni wajumbe kutoka pande zote mbili, Tanzania ikiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Ombeni Y. Sefue (wa nne kushoto), Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa kwanza kushoto), Afisa Mwandamizi wa Rais Kikwete (masuala ya diplomasia), Mhe. Balozi Tuvako Manongi (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na Ndugu Prosper Mbena (wa tano kushoto), Msaidizi wa Rais Kikwete.  Wengineo ni Wajumbe kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon, mara baada ya mazungumzo yao mjini New York.




VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI HAVIKUBALIKI- JK

Na MAURA MWINGIRA, New York
2 Oktoba, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  amesema,  vifo vya akina mama vitokanavyo na matatizo wakati  wakujifungua havipaswi kutokea na havikubaliki.
Na kwa sababu hiyo, anasema juhudi zaidi zinahitajika katika kubabiliana na hali hiyo na hasa ikizingatia kwamba   sababu zinazosabisha kutokea kwa vifo hivyo zinazuilika.

“ Vifo vya wanawake wajawazito havikubaliki” akasema na kuongeza “ na ndiyo kwasababu tunahitaji kuongeza  juhudi zaidi kuokoa maisha ya wanawake, kwa sababu si haki na si jambo jema kwa mwanamke kufa wakati wa kujifungua , si haki afe wakati akimleta kiumbe mwingine duniani, na cha kusikitisha zaidi wanakufa kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika”, akasisitiza Rais Kikwete.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa  awamu ya pili ya mpango wa ubunifu wa uboreshaji wa huduma ya  afya ya mama na mtoto katika maeneo ambayo huduma hiyo haipatikani kwa urahisi nchini Tanzania.

Uzinduzi wa mpango huo umefanyika mbele ya waandishi wa habari siku ya  jumanne  hapa  Makao Uakuu ya Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki  Moon, Rais Jakaya kikwete na wafadhili wakuu wa mpango huo ambao ni Meya wa Jiji la New  York  na philanthropist Michael Bloomberg na Dkt. Helen Agerup, Mkuu  wa Mfuko wa  H&B Agerup.

Wafadhili hao wawili wametoa dola za kimarekani  milioni 15 kufadhili huduma za uboreshaji wa vituo vya afya,  na mafunzo ya huduma za upasuaji wa dhararu kwa  waganga,  wakunga na manesi lengo likiwa ni kuokoa maisha ya wanawake wanapojifungua na kupunguza umbali wa  kuifuata huduma hiyo.

Rais Kikwete amesema kwamba, uboreshaji wa huduma za afya ya mama na mtoto na afya kwa ujumla  ni moja ya vipa umbele  vyake muhimu na ni jambo lililo ndani ya moyo wake.

“Tumefanya mengi na tunaendelea kufanya, lakini tunahitaji kuongeza kasi ya juhudi hizi,  uboreshaji wa huduma ya afya ya mama na mtoto ni kupaumbele changu ni jambo lililo moyoni mwangu na tunapopata wafadhilli kama nyinyi kuchangia juhudi zetu tunafarijika zaidi na kutiwa moyo na tunawashukuru” akasema Rais.

Naye  katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania nakutetea  haki za wanawake na watoto, amesisitiza haja na umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta za umma na sekta binafsi kuokoa maisha ya wanawake na watoto kwa kuboresha huduma zao.

“Tunahitaji marais, mameya, wanaharakatiwa   kuboresha huduma za afya na wafanyakazi wa afya hadi ngazi ya chini kabisa. Leo tunashuhudia matokeo ya ushirikiano huu ambapo kwa ushirikiano wa viongozi watatu tumeweza katika kipindi cha miaka miwili  kupunguza kwa  asilimia kubwa vifo vya wanawake wajawazito katika  maeneo ya mikoa ya Kigoma,  Morogoro na Pwani ambako mpango huu wa ubunifu umekuwa ukitekelezwa” akabainisha Ban ki Moon.

Aidha  Ban Ki Moon amemuelezea  Rais Jakaya kikwete kama  mmoja wa viongozi  wa kwanza duniani kuungua mkono mkakati wa Kimataifa kuhusu Afya ya mama wajawazito na watoto, mpango uliozinduliwa mwaka 2010 ambapo kiasi cha  dola milioni 400 zitaelekezwa katika  uboreshaiji wa huduma hizo. Na ni   mpango unaokwenda sambamba na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo  Millenia ( MDGs).

Kwa upande wake Meya na philanthropies Michael Bloomberg  akizungumza  kwenye uzinduzi huo anasema aliamua kuichagua Tanzania  kufadhili  uboreshaji wa huduma za afya ya mama na mtoto kutokana na kuvutiwa kwake na juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kukabiliana na  vifo vitokanavyo na uzazi.

“Mwaka 2006 niliamua kuwekeza Tanzania kwa kubuni mpango huu wa kuboresha huduma ya dharura ya uzazi  hasa katika maeneo  ambayo hayafikiki na hakuna huduma za afya. Niliamua hivi kwa sababu nilivutiwa sana na juhudi za Rais Kikwete, ni kiongozi makini, imara na  ambaye amekuwa mstari wa mbele katika suala hili, Tanzania inabahati ya kuwa na kiongozi kama huyo” akasisitiza.

Na kuongeza kwamba mpango wake huo ambao amesema ni wa aina yake na wa kwanza kufanyika na  umeanza katika maeneo machache kwa lengo la kuona maendeleo na mafaniko yake  ili baadaye uweze kusambazwa katika maeneo mengine ya nchi.
Naye Dkt. Helen Agerup, yeye amesema ameamua kuugana na Meya Bloomberg kufadhili mpango huo  kutokana  kuvutiwa na  kazi nzuri inayofanywa na Meya na kubwa zaidi baada ya kujionea kwa macho yake kile ambacho kimekuwa kikifanyika nchini Tanzania.

“Nilikwenda Tanzania  mimi na binti yangu na mume wangu, tukajionea kazi nzuri ya  ubunifu huu na namna ilivyoweza kuokoka maisha ya wanawake wajawazito. Tumeamua kuwekeza kwa sababu kile tulichokiona Tanzania kimekidhi malengo ya mfuko wetu, kwa sababu tunahitaji kufanya jambo ambalo matokeo yanapimika,  yanaonekana na yanazaa matunda na haya yote tumeyashuhudia Tanzania”, akabainisha Dkt. Hellen.

Uzinduzi wa mpango huo ulikwenda sambamba na onesho la video fupi iliyoonyesha  kile kilichokuwa kikifanyika nchini Tanzania, kwa maana ya uokoaji wa vifo vya wanawake wajawazito kwa utoaji wa huduma za dharura za upasuaji baada ya waganga na wakunga kupewa mafunzo ya upasuaji wa dharura.

Aidha video hiyo imeonyesha wanawake wakipoteza maisha aidha kutokana na kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua au kupata maambukizo wakati wa kijifungua. Lakini imeonyesha pia jinsi ya wataalamu hao wakitoa huduma hiyo kwa uhodari na uadilifu mkubwa na nyuso zao zikiwa zimejaa faraja hasa baada ya kupewa mafunzo kupitia mpango huo.






Tuesday, October 2, 2012

Press Conference: UN Secretary General, President Kikwete and NYC Mayor Bloomberg unveil results of Innovative Maternal Health Program in Tanzania




H.E. Jakaya Mrisho Kikwete (3rd right), President of the United Republic of Tanzania in a press conference held today in New York to unveil results of Innovative Maternal Health Program in Tanzaina.  Others are the United Nations Secretary General Ban Ki-moon (2nd left), New York City Mayor Bloomberg (left) and Ms. Helen Agerup (2nd right) of the H&B Agerup Foundation and Mr. Martin Nesirky (right), Spokesperson for the Secretary-General, in the Dag Hammarskjöld Library at the United Nations Headquarter in New York, USA.


President Kikwete reading his Statement before members of media.  Listening are UN's Secretary General Ban Ki-moon (center) and New York City Mayor Michael Bloomberg (left).



Tanzania Delegation which consisted of Chief Secretary H.E. Ambassador Ombeni Y. Sefue (5th left), Ambassador Liberata Mulamula, Senior Advisor to President Kikwete, Ambassador Mwanaidi Sinare Maajar (3rd left), Ambassador of the United Republic of Tanzania to the United States of America, H.E. Ambassador Tuvako Manongi (left), Permanent Representative of Tanzaia to the United Nations.  Others are Deputy Ambassador Ramadhan Muombwa Mwinyi (4th left), Deputy Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations, Mr. Prosper Mbena (6th left), Assistant to President Kikwete and Mr. Salva Rweyemamu, Director of Communications to the Tanzania State House.     



President Kikwete (right), UN's Secretary General Ban Ki-moon (center) listening to New York City Mayor Michael Bloomberg during the press conference.   The Bloomberg Philanthropies have been supporting Tanzania since 2006, with investment of over USD 7.5 million towards projects aim to prevent maternal and newborn deaths.


Ms. Helen Agerup of H&B Agerup Foundation gives her remarks during the press conference which was held today in the Dag Hammarskjöld Library at the United Nations Headquarter in New York, USA.  Bloomberg Philanthropies in collaboration with H&B Agerup Foundation will cost-share the second phase to support Tanzania for a combined commitment of USD 8 million.  The first phase which started since 2006 cost USD 7.5 million where over 9 health centres had been upgraded in Kigoma, Morogoro and Pwani Regions.  The project aims at exploring opportunties to incentivize and promote retention of trained health care workers.   In the photo also is Mr. Martin Nesirky (1st right), Spokesperson for the UN's Secretary-General.



A short video on the work of Bloomberg Philanthropies in Tanzania is playing in the background.


Dr. Peter Mfisi (left) of the President Kikwete's office and Ms. Ellen Maduhu (2nd left), main organizer of the event and Foreign Service Officer at the Tanzania Mission to the United Nations. Others in the photo are official personnels from the Bloomberg Foundation.


A news reporter from CBS Channel of Americans asks few questions to President Kikwete.   Third left is Mr. Modest Jonathan Mero, Minister Plenipotentiary of the Permanent Mission of the United Republic of Tanzania to the UN. 


President Kikwete answering few questions from the reporters (not in the photo).


Ms. Ramla Khamis, Second Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation listening to the press conference.



All photos by Tagie Daisy Mwakawago