Saturday, October 6, 2012

Mkutano kati ya Waziri Membe na Waandishi wa Habari kuhusu mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akifafanua kwa  Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu hoja zilizotolewa na Serikali ya Malawi za kujitoa katika mazungumzo kuhusu mgogoro uliopo kati  ya Tanzania na Malawi kuhusu Ziwa Nyasa. Wengine katika picha kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule  na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju.

Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Vyombo na Mashirika mbalimbali ya Habari hapa nchini wakimsiliza kwa makini Mhe. Waziri Membe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (aliyesimama) wakati akimkaribisha Mhe. Waziri Membe kuzungumza na  Waandishi wa Habari (hawapo pichani).

Mmoja wa Wanahabari  Bw. Florian Kaijage akiuliza swali wakati wa mkutano wao na Mhe. Waziri Membe.

Mhe. Waziri Membe akijibu swali kwa msisitizo aliloulizwa.

Mhe. Waziri Membe (waliokaa kushoto) akionesha kwa Waandishi wa Habari Ramani mpya ya Tanzania. Wengine katika picha (aliyekaa kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule akifuatiwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Selasie Mayunga na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria hapa Wizarani Balozi Irene Kasyanju.

Mhe. Waziri Membe akifafanua kwa Waandishi wa Habari kuwa mpaka katika ramani ya Tanzania umepita katikati ya Ziwa Nyasa na si ufukweni kama inavyodaiwa na Malawi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule,  akimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Membe wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiririkiano wa Kimataif, Balozi Irene Kasyanju akiwa makini kusikiliza ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mhe. Waziri Membe kwa Waandishi wa Habari kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi juu ya Ziwa Nyasa.

Wageni waalikwa na baadhi ya waandishi wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.