Monday, October 29, 2012

Waziri Membe akiwa ziarani Mkoani Mbeya



Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisaini kitabu cha wageni leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, wakati akiwa katika ziara ya siku mbili Mkoani humo.


Mhe. Waziri Membe akifafanua kuhusu mgogoro wa Mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Uenyekiti wa Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mbeya wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani).




Wilayani Kyela, Mbeya

Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mhe. M. Malenga akimkaribisha Mhe. Waziri Membe (wa pili kulia), wakati alipotembelea Ofisini yake Wilayani Kyela.  Mhe. Membe yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya siku mbili ambapo atatembelea na kuzungumza na wananchi waishio katika maeneo yaliyopo kando ya Ziwa Nyasa.

Wajumbe mbalimbali waliohudhuria Mkutano wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kyela (hayupo pichani).


Balozi Irene Kasyanju (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Dkt. Mohamed Maundi (kushoto), Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia - Kurasini wakisikiliza maelezo ya Mhe. Malenga kuhusu Wilaya ya Kyela.




Safari ya kuelekea kwenye mpaka wa Mto Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Kyela akiuongoza msafara wa Waziri Membe kuelekea kwenye mpaka wa Mto Songwe uliopo kati ya Tanzania na Malawi.


Mhe. Waziri Membe na msafara wake wakiwa wamesimama kwenye mpaka wa Mto Songwe.


Waziri Membe akiangalia Mto Songwe, huku akitafakari mpaka kwa vile hapo aliposimama kwa ufupi ni nchini Malawi ambapo wananchi wa nchi zote mbili upishana wakiwa katika shughuli zao za kawaida (angalia alama ya tundu lililoko chini ya fensi - kulia).


Mhe. Waziri Membe akiongea na Wajumbe wa msafara wake akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro (mwenye shati jeupe mbele ya Waziri), Balozi Irene Kasyanju (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Dkt. Mohamed Maundi (kushoto), Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia - Kurasini.  (Picha hii na Mbaraka Islam)


Makazi ya wananchi wa Malawi kando ya Mto Songwe ambapo mmoja wa wananchi anaonekana akifua nguo (pichani - upande wa kushoto ambao ni ng'ambo ya mpaka kwa upande wa Malawi) wakati wengine (kulia) wanaonekana wakiendelea na shughuli zao za kawaida huku wakiwa tayari ng'ambo ya mpaka kwa upande wa Tanzania.

  
Mhe. Waziri Membe akisalimiana na mmoja wa Machifu kutoka Malawi, Bw. Clement Kyungu Mwakasungura ambaye alikutana naye Kasumulu, Wilayani Kyela - Mkoani Mbeya.

Picha, maelezo na Tagie Daisy Mwakawago


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.