Wednesday, October 24, 2012

Mhe. Waziri Membe nchini Ufaransa kwa Ziara ya Kikazi‏



Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Mhe. Laurent Fabius, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ofisini kwake jijini Paris leo, Jumatano tarehe 24 Oktoba, 2012.

Mheshimiwa Waziri Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika mazungumzo na Mhe. Abdou Diouf, Katibu Mkuu wa La Franchophonie na Rais Mstaafu wa Senegal alipofanya nae mazungumzo ofisini kwake Paris leo. Wa kwanza kushoto ni Mhe. Begum Karim Taj, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa.

Mhe. Waziri Membe na mwenyeji wake Mhe. Abdou Diouf katika picha ya pamoja na ujumbe wao mara baada ya mazungumzo.

Mhe. Waziri Membe na mwenyeji wake Mhe. Abdou Diouf katika picha ya pamoja na ujumbe wao mara baada ya mazungumzo.

Mhe. Waziri Membe Ziarani Ufaransa
Mhe. Waziri Membe yuko nchini Ufaransa kuwasilisha ujumbe maalum wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa Ulinzi na Usalama kwa Mhe. Francois Hollande, Rais wa Ufaransa.

Mhe. Waziri Membe amewasili leo asubuhi na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Mhe. Laurent Fabius, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ofisini kwake jijini Paris. Mhe. Membe aliwasilisha ujumbe wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa Mhe. Francois Hollande, Rais wa Ufaransa. Tanzania ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, chombo kinachoshughulikia migogoro na usuluhishi katika ukanda wa SADC.

Baadaye, Mhe. Waziri Membe alifanya mazungumzo na Mhe. Abdou Diouf, Katibu Mkuu wa La Francophonie na Rais Mstaafu wa Senegal.

Mhe. Waziri Membe anatarajia kumaliza ziara yake kesho kwa kukutana na Mshauri wa Rais Hollande wa Masuala ya Afrika.





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.