Tuesday, November 12, 2013

Mkutano wa Ushirikiano baina ya Nchi za Afrika na Kiarabu



Na Ally Kondo, Kuwait

Mkutano wa Ushirikiano baina ya Nchi za Afrika na Kiarabu (Afro – Arab Summit) umeanza nchini Kuwait siku ya Jumatatu tarehe 11 Novemba, 2013 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) kuandaa Kongamano la Uchumi na Uwekezaji. Mkutano huo unafanyika katika ngazi mbalimbali ukianzia na mkutano wa ngazi ya maafisa waandamizi baadaye  Mawaziri na kuhitimishwa na Mkutano wa Ngazi ya Wakuu wa Nchi na Serikali ambao umepangwa kufanyika tarehe 19 na 20 Novemba, 2013.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal atamwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mkutano wa ngazi ya Wakuu wa Nchi na Serikali.

Mkutano wa mwaka huu wa Afro –Arab Summit ni watatu kufanyika ambapo wa kwanza ulifanyika Misri katika miaka ya 70 na wa pili ulifanyika mjini Sirte, Libya mwaka 2010. Katika Mkutano wa Libya, Wakuu wa Nchi na Serikali walijiwekea malengo mbambali ambayo utekelezaji wake utatathiminiwa katika mkutano wa mwaka huu nchini Kuwait.

Mkutano wa mwaka huu wenye kaulimbiu isemayo “Wabia katika Maendeleo na Uwekezaji” unadhamiria kuweka mikakati madhubuti ya kushirikiana baina ya nchi za Afrika na Kiarabu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, bishara, uwekezaji, siasa na masuala ya kijamii.

Kwa upande wa sekta ya kilimo, nchi hizo zinakusudia kuimarisha ushirikiano ili kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo kwa kutumia ardhi kubwa na yenye rutuba iliyopo katika nchi za Afrika ambazo hazina mitaji yakutosha kama zilivyo nchi za Kiarabu. Lengo kubwa la mkakati huo ni kukomesha njaa ya mara kwa mara inayozikumba nchi za Afrika pamoja na kuondoa hali ya wasiwasi wa tishio la njaa linaloweza kutokea katika nchi za Kiarabu.

Katika mkutano huo pia nchi za Afrika na Kiarabu zitajadili namna zitakavyoweza kushirikiana kwa pamoja katika kukabiliana na kudhibiti majanga ya asili ambayo yanapotokea husababisha uharibifu mkubwa wa maisha ya watu na mali zao.

Sanjari na mkutano huo, Serikali za Tanzania na Kuwait zinatarajia kuweka saini Mikataba miwili ya Kukuza na Kulinda Vitega Uchumi; na Ushirikiano katika Sekta ya Utalii. Mikataba hiyo itakaposainiwa itahamisisha uwekezaji pamoja na kuongeza idadi ya watalii kwa manufaa ya nchi hizi mbili. 
   

Minister Membe meets with the Commonwealth Secretary General


Hon. Bernard K. Membe (MP) (right), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation greets Mr. Kamalesh Sharma, Commonwealth Secretary-General today in Colombo, Sri Lanka.

Hon. Minister Membe is in Sri Lanka to participate at the Foreign Minister's Meeting which begins tomorrow 13-14 November, 2013.  The Commonwealth Leaders are scheduled to meet on the 15th through 17th November.  

Minister Membe in a discussion with the Secretary-General of the Commonwealth, Kamalesh Sharma.


Minister Membe also met with Ms. Mmasekgoa Masire-Mwamba, the Commonwealth Deputy Secretary-General.

Hon. Minister Membe in a continued discussion with Ms. Mmasekgoa Masire-Mwamba (right), the Commonwealth Deputy Secretary-General.  Listening on is Ambassador Peter Kallaghe, High Commissioner of the United Republic of Tanzania in London, with accreditation to the United Kingdom, to the Republic of Ireland and to the Commonwealth.


Hon. Membe in a group photo with Mr. Kamalesh Sharma (left), Commonwealth Secretary-General, Ms. Mmasekgoa Masire-Mwamba (2nd right), the Commonwealth Deputy Secretary-General and one of the members in the Commonwealth Secretariat. 



All photos by Tagie Daisy Mwakawago 



Tanzania, Sri Lanka Foreign Ministers meet


Hon. Prof. G.L. Peiris, Sri Lanka Minister for External Affairs welcomes his counterpart Hon. Bernard K. Membe (MP), Tanzania Minister for Foreign Affairs and International Affairs during their meeting today at Hilton Colombo Hotel in Sri Lanka. 

 Hon. Minister Membe (left) thanks the Sri Lanka Minister for External Affairs for his country's hospitality and to congratulate Sri Lanka for hosting the Commonwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) 2013. 

The Meeting continues. 

Tanzania delegation was represented by Ambassador Peter Kallaghe (left), High Commissioner of the United Republic of Tanzania in London with accreditation to the United Kingdom, the Republic of Ireland and the Commonwealth and Ambassador Mbelwa Kairuki (2nd left), Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.  

The Sri Lanka delegation was represented by Mrs. Aruni Ranaraja (2nd right), Acting Director General of Africa Affairs in the Ministry of External Affairs and Mrs. Sithara Khan (right), Acting Additional Secretary for Public Relations in the Ministry of External Affairs. 

The two Ministers in a tête-à-tête meeting.


All photos by Tagie Daisy Mwakawago