Wednesday, December 2, 2015

MHE. BALOZI WILSON M. MASILINGI AKUTANA NA BI. CATHY BYRNE, MKURUGENZI MWANDAMIZI WA MASUALA YA AFRIKA, IKULU YA MAREKANI (WHITE HOUSE) TAREHE 30 NOVEMBA 2015

Mhe. Balozi Masilingi (kulia) ametembelea ofisi ya Bi. Cathy Byrne, Mkurugenzi Mwandamizi wa masuala ya Afrika katika Ikulu ya Marekani (White House). Katika maongezI yao, Bi. Cathy Byrne alimueleza Mhe. Balozi Masilingi jinsi Serikali ya Marekani inavyoridhishwa na mahusiano mazuri baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani. Pia alieleza kuhusu serikali ya Marekani kuridhishwa na hatua za serikali ya Tanzania, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
 Mhe. Balozi Masilingi amemhakikishia mwenyeji wake kuwa ataendeleza mashirikiano mazuri sana yaliyopo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani kwa njia ya diplomasia ya uchumi yenye lengo la kuhamasisha biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

==============================
Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, akifuatana na Bw. Paul Mwafongo alihudhuria mkutano na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Dunia, Kundi la Nchi za Afrika. 

Wengine waliohudhuria ni pamoja na Bw. Andrew Ndaamunhu Bvumbe, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, na Bw. WilsonToninga Banda, Mshauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Shabaha ya Mkutano ilikuwa ni kufuatilia mazungumzo yaliyofanyika Lima, Peru kuhusu kuimarisha ushirikiano kwa maslahi ya Afrika. 

Mhe. Balozi Masilingi alishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri uliopo na kwa misaada na mikopo wanayotoa kuunga mkono juhudi za kujenga uchumi na kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote. 

Aidha aliwahakikishia ushirikiano muda wote atakapokuwa katika kutekeleza wajibu wake wa kazi kwa maslahi ya Taifa. Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Dunia, Kanda la Afrika, Bw. Louis Larose, alieleza kwa upande wake kuridhirishwa kwake na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Benki ya Dunia. 

Aidha Bw. Larose aliipongeza Tanzania kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba , 2015 kwamba ulikuwa huru na wa haki. Pia, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John P. Magufuli kwa ushindi na kwa juhudi zake katika kuangalia udhibiti wa ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuziba mianya ya uvujaji wa mapatao ili zipatikane fedha kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Watanzania. 

 Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kwamba Benki ya Dunia iko tayari kutoa msaada wowote wa haraka utakaohitajika na kuombwa na Serikali ya Tanzania ili kufanikisha mpango wa kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza program za maendeleo na huduma za serikali. 

 Bw. Larose, alimdokeza Mhe. Balozi kwamba Benki ya Dunia itaandaa siku maalumu mjini Washington, D.C. kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake nchini Marekani na kuomba kwamba Benki ya Dunia itamwalika Mhe. Balozi kuzindua siku hiyo. Akijibu hoja hiyo Mhe. Balozi alikubali mwaliko huo.

Tuesday, December 1, 2015

Balozi wa Afrika Kusini nchini amtembelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe. Thamsanga Dennis Mseleku katika mazungumzo yaliyolenga kuboresha mahusiano mema na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.  
Balozi Thamsanga Dennis Mseleku, akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Balozi Mulamula.
Mazungumzo yakiendelea huku Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto), Bw. Merdard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje (katikati) pamoja na Afisa Habari wa Mambo ya Nje, Bw. Ally Kondo wakifuatilia mazungumzo hayo.
    
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akiagana na Balozi wa    Afrika Kusini hapa nchini Mhe. Thamsanga Dennis Mseleku,           baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Wizarani tarehe 01/12/2015.
                         =========================
                           Picha na Reuben Mchome.

Monday, November 30, 2015

Balozi Mulamula akutana kwa mazungumzo na Kamishna wa masuala ya Afrika wa Ujerumani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi Georg Schmidt, Kamishna anayeshughulikia  masuala  ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani ambaye yupo katika ziara ya kikazi hapa nchini. Mazungumzo yao yalijikita kwenye masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan kwenye maeneo ya biashara na uwekezaji.
Mazungumzo yakiendelea
Mkurugenzi wa Idara y Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine (kushoto), na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Olivia Maboko wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Schmidt  (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Mulamula akiagana na mgeni wake Balozi Schmidt mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.



Picha na Reginald Philip

Rais Magufuli Aonana na Mabalozi wa China na Korea Kusini, Ikulu jijini Dar Leo

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Korea ya Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL, wakati akimkaribisha na kufanya nae mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea ya Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.

Saturday, November 28, 2015

UN wakishirikiana na Ubalozi wa Palestina wafanya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati), Kaimu Balozi wa Palestine Derar Ghannam (kulia) pamoja na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali wakikata utepe kwa ajili ya maonesho ya picha za matukio mbalimbali yanayoendelea nchini Palestina hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 
Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam (wa kwanza kulia) akimuonyesha picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati) za matukio ya mauaji ya watu nchini Palestina yanayofanywa na Waisraeli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 

Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi Stella Vuzo (kulia) akitazama picha za wananchi wa Palestina waliouliwa na kutokana na mapigano ya Palestina na Israel yanayosababisha vifo vya watu wengi wasiokuwa na hatia.  
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima akisoma hotuba yake mbele ya Mabalozi, wanafunzi wa chuo cha Diplomasia pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye maadhimisho ya ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 
Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina.  
Baadhi ya Mabalozi waliofika kwenye maadhimisho hayo wakiendelea kufuatilia yanayojiri.  
Naibu Mkurugenzi wa Mipango Utawala na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Dk.Bernard Achiula akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika chuoni hapo. 
Prof Josephat Kanywanyi ,Chairperson Tanzania- Palestine Solidarity committee akitolea ufafanuzi kuhusu mahusiano ya Tanzania na Palestina wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina.  
Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiendelea kusikiliza kwa makini kinachozungumzwa kutoka meza kuu.  
Baadhi ya Mabalozi waliofika kwenye maadhimisho hayo wakiendelea kufuatilia yanayojiri. 
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi mbalimbali pamoja mabalozi.  
Viongozi wakiwa kwenye picha na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.


Na Mwandishi wetu

UN Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Palestina nchini waadhimisha Siku ya Kimataifa na Mshikamano na watu wa Palestina na Tanzania katika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma na kukutana na mabalozi wa wa nchi mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima, Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali ambapo ikiwa kuendeleza ushirikiano pamoja na mfululizo wa maonesho ya picha mbalimbali za matukio yanayoendelea huko nchini Palestina.

Mabalozi hao ambao walikutana katika jijini Dar es salaam kwaajili ya kuadhimisha siku hiyo ya kumbukumbu za picha za mapigano ya Palestina kwa ajiri ya kudumisha upendo na mshikamano pia mabalozi hao wameuomba umoja wa mataifa kuweza kuchukua hatua za ziada zitakazo pelekea nchi hiyo kuwa huru na kuweza kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka UNDP, Steve Lee akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kuwa uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina alisisitiza kuwa na na umoja baina ya nchi zote mbili hususani Palestina kuweza kupata uhuru na kutambulika kuwa ni nchi nyenye mipaka yake binafsi ili kuepusha mapigano hayo yasiweze kutokea na kila mtu aweze kuishi na amani akiwa ndani ya nchi yake na kuweza kufanya maendeleo ya nchi. Na aliweza kuziomba nchi mbalimbali kulitambua taifa la Palestina kama nchi kamili tofauti na inavyotambulika kwa sasa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa siku ya maonesho ya picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima amesema wamefanya hivyo kwani ni hari ya kuwatakia heri Wapalestine wote kwani watu wote waparestine walipoteza uhuru na kwa sasa wanautafuta uhuru kwani nchi wanayo lakin hawako huru kwahiyo ni lazima tuwaunge mkono kwa kuweza kuadhimisha siku hii sehemu mbalimbali tunayoishi.

Kwa upande wa Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi Stella Vuzo amesema wameamua kuwa na maadhimisho kwani ndani ya miaka 50 Palestina wamekuwa hawajatambulika kama taifa lenye mipaka yake ambapo kumekuwa na migogoro ya mda mrefu ambao unawahusu wa Palestine na wayahudi ambao upo tangu mwaka 1947,wakati katika maadhimio walio fikiana ni kuwa na mataifa mawili ndani ya eneo moja ambap mpaka sasa Israel pekee ndo iliyo pata kuwa hali ya taifa lenye mipaka yake wakati .


Kila siku Israel huwa wanaleta vita ndani ya Palestine, sasa maadhimisho haya ni kwa ajili ya kuwaunga mkono kwa vitendo vinavyo endelea huko si vizuri. Pia aliwaomba viongozi wa pande zote mbili kuweza kuketi na kuweza kuweka maadhimio mapya kwaajili ya kuepusha mapigano yanayokuwa yakitokea kila siku baina ya nchi hizo mbili. Pia katika siku hiyo waliweza kuzindua picha za matukio ya vifo pamoja na watu walioumia kutokana na vita Palestina na Israel zilizo kuwa zimeandaliwa kwa Tanzania kwa ajili ya kuonyesha dunia matukio yanayoendelea katika nchi za Mashariki ya mbali hii yote ni kwa kuwa Palestina ina ushirikiano na Tanzania na kuwaombea katika kuelekea hali ya utulivu.