Friday, July 1, 2016

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ampokea Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame Nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda kwa ziara rasmi ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame. Ziara hii ni ya siku mbili.Baada ya Hapo ataelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kufanya Mazungumzo.

Baada ya hapo wataelekea katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ufunguzi rasmi ya maonesho ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba  leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakiwa ameambatana na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda mara baada ya kuwasili asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara rasmi ya siku mbili ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame.  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakipata Gwaride la heshima uwanjani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakitazama kikundi cha ngoma za asili kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo.

Rais Paul Kagame akiwapungi mkono baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika kumlaki uwanjani hapo,kushoto kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli .


Thursday, June 30, 2016

Waziri Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikii, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha na kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili pamoja na Ziara ya ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame anayetarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku mbili. 

Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana alipokuwa akimkaribisha Mhe. Waziri Mushikiwabo mara baada ya kuwasili Wizarani.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Samuel Shelukindo akiwa na Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo.




Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (kulia) pamoja na Afisa aliyeambatana na Mhe. Waziri Mushikiwabo wakifuatilia mazungumzo.

Wakati mazungumzo yakiendelea
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo





Diaspora wahimizwa kutii Sheria bila Shuruti


TANGAZO KWA WATANZANIA WOTE NA WALE WANAOISHI NJE YA NCHI (DIASPORA)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inaendelea na jitihada zake za kuhamasisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) katika kuchangia maendeleo ya nchi yao.  Ili kufanikisha hilo, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imekuwa ikizishawishi taasisi mbalimbali hapa nchini kutoa huduma na fursa za biashara na uwekezaji, ambazo zitasaidia Diaspora kuwekeza kiurahisi hapa nchini.  Juhudi hizi ambazo zilianza tokea Serikali ya Awamu ya Nne zimeanza kutoa matunda makubwa ambapo thamani ya uwekezaji kutoka kwa Diaspora inaongezeka kila kukicha.