Wednesday, July 18, 2018

Mabalozi wanne waagwa jijini Dar Es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) aliyesimama katikakti akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi waliomaliza muda wao wa uwakilishi nchiniTanzania. Mabalozi hao, wakwanza kutoka kushoto ni Balozi wa Norway, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, Balozi wa Malawi, Mhe. Hawa Olga Ndilowe, Balozi wa Sweden, Mhe. Katarina Rangnitt na Balozi wa Canada, Mhe. Ian Myles. Mhe. Dkt. Mahiga aliandaa hafla ya kuwaaga Mabalozi hao iliyofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 17 July 2018. Katika hafla hiyo, Dkt. Mahiga aliwashukuru Mababalozi hao kwa niaba ya Serikali zao kwa mchango mkubwa wanaotoa kuboresha sekta mbali mbali hapa nchni zikiwemo za Elimu, Afya, Biashara, Kilimo pamoja na Miundombinu. Aidha, Mabalozi pia walipata nafasi ya kutoa neno la shukrani kwa Wizara pamoja na watumishi wake kwa ujumla kwa kuwapa ushirikiano wa kutosha uliowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hapa nchini.
Dkt. Mahiga akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga Waheshimiwa Mabalozi walio maliza muda wao wa uwawakilishi nchini.

Sehemu ya Mabalozi walio hudhuria hafla hiyo wakisimsikiliza kwa makini Mhe. Dkt. Mahiga (hayupo pichani).
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya naAmerika, Bw. Jestas Nyamanga (kulia) pamoja na Balozi Rangnitt nao wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mahiga.
Sehemu nyingine ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo
Mabalozi walio maliza muda wa uwakilishi nchini wakigonga glasi na Waziri Mahiga ikiwa ni ishara ya kuwatakia Viongozi wa Nchi zao Afya njema na Baraka tele kwenye kufanikisha gurudumu la maendeleo.
Dkt. Mahiga akimkabidhi Balozi wa Sweden picha ya mchoro wa Tembo wa Tatu pamoja na Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuikumbuka Tanzania pamoja na kuendelea kuvitangaza vivutio vinavyopatikana nchini. 
Balozi wa Malawi naye alipewa Picha yenye tembo wa Tatu na mlima Kilimanjaro
Dkt. Mahiga akimkabidhi Balozi wa Norway picha inayofanana na wenzake isipokuwa yake ilikuwa na Michoro ya Wanyama aina ya Twiga, Tembo pamoja na Mlima Kilimanjaro.
Balozi wa Canada naye alipata zawadi ya picha yenye mchoro wa Tembo pamoja na Mlima Kilimanjaro, kwa pamoja Mabalozi hao walionyesha kuzifurahia zawadi hizo.
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi waliomaliza muda wa uwakilishi nchini pamoja na Mabalozi ambao bado wanaendelea kuziwakilisha nchi zao. 











Tuesday, July 17, 2018

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Kenya nchini

Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.). Mara baada ya kuwasilisha nakala hizo Mhe. Mahiga na Balozi Kazungu walipata fursa ya kuzungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya hususan kwenye sekta za biashara, uchumi na elimu. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ofisi Ndogo ya Wizara iliyopo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Julai, 2018. 
Dkt. Mahiga akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Kenya hapa nchini
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Kenya nchini. Kushoto ni Bibi Judica Nagunwa na Bw. Magabilo Murobi
Balozi Kazungu akimweleza jambo Dkt. Mahiga
Mazungumzo yakiendelea kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Kazungu
Picha ya pamoja.
Dkt. Mahiga akiagana na Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania. 






Thursday, July 12, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU FURSA ZA MASOMO


TAARIFA KWA VYOMBO VY HABARI

FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo katika kozi mbalimbali kutoka Serikali ya Saudi Arabia.

Mafunzo hayo yatatolewa katika Chuo Kikuu cha Imam Abdulrahman bin Faisal kilichopo Saudi Arabia. Taarifa kamili kuhusu ufadhili, kozi na taratibu zote za namna ya kuomba zinapatikana kupitia tovuti ya Chuo hicho www.iau.edu.sa
 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
12 Julai, 2018


Tuesday, July 10, 2018

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaendelea kutoa huduma kwenye maonesho ya sabasaba

Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa mteja aliyetembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa yanayoenedelea jijini Dar es Salaam.
Mhe. Balozi Rajab Luhwavi Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji (wa kwanza kulia) akizungumza na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya sabasaba.



Balozi Mohamed Haji Hamza Mkurugenzi wa ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje Zanzibar (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia Bw. Shoo Innocent alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba 

Bw. Zakariyya Kera Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya sabasaba

Bw. Teodos Komba akifanunua jambo kwa mteja aliyembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

Wanafunzi kutoka Dar es Salaam Islamic Secondary School wakipewa maelezo walipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya sabasaba


Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiangalia bidhaa kwenye maonesho ya sabasaba

Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiangalia bidhaa kwenye maonesho ya sabasaba

Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiangalia maonesho ya kazi ya ubunifu wa teknolojia kutoka kwa Wataalam wa Taasisi ya Mafunzo ya Ufundi Zanzibar

Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoka kuangalia bidhaa kwenye jengo la Zanzibar katika maonesho ya sabasaba 

Sunday, July 8, 2018

Waziri Mahiga atembelea maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba)



Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alipotembelea banda la Wizara.

Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika mahojiano na wanahabari kwenye maonesho ya biashara kimataifa maarufa sabasaba yanayofanyika jijini Dar  es Salaam
Mhe.Waziri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

Mhe. Mahiga akisikiliza maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa ya sabasaba

Thursday, July 5, 2018

Naibu Waziri atembelea maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa (sabasaba)



Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga pamoja na watumishi wa Wizara. 

Dkt. Kolimba alifurahishwa na ushiriki wa Wizara  kwenye maonyesho ya sabasaba, ambapo aliwasisitiza watumishi wa Wizara kuendelea kutumia fursa hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara. 
 Mhe.Dkt. Kolimba akipata maelezo kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga

Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na watumishi alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

Mkurugenzi wa Masomo wa Chuo cha Diplomasia Prof. Watengere Kitojo  akizungumza na watumishi alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya sabasaba .
Wanafunzi kutoka Chuo cha Diplomasia wakipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara walipotembelea bandala kwenye maonesho ya saba.Wanafunzi hao walipata fursa ya kuelezwa kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa sambamba na fursa na faida zinazopatikana.
Bw. Teodos Komba Afisa Mawasilino, akielezea jambo kwa wananchi waliojitokeza  kwenye banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bw. Hassan Mnondwa akielezea jambo kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara.

Mhe.Dkt. Susan Kolimba akiwa katika Picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara

Tuesday, July 3, 2018

Wananchi waendelea kujitokeza katika banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba


Mama Anna Mkapa Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, akiangalia moja ya machapisho yanayopatikana katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya biashara ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Wananchi wengi wameendelea kujitokeza kwenye banda la Wizara ili kuongeza  uelewa  juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara, ikiwemo namna Wizara inavyosimamia na kuteleza sera ya mambo ya nje ya nchi,  faida  na hatua mbalimbali za mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lipo katika jengo la sabasaba hall.Wananchi  wote wanakaribishwa 
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto) wakizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye banda la Wizara (kulia)



Sehemu nyingine ya watumishi wa Wizara wakihudumia wananchi

Sehemu nyingine ya wananchi wakiuliza masuala mbalimbali kwa watumishi wa Wizara
Sehemu nyingine ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara

Sehemu nyingine ya wananchi wakipewa maelezo na mtumishi wa Wizara

Friday, June 29, 2018

Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa wafikia tamati


Mhe. Prof. Makame Mbarawa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, akizungumza kwenye Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Prof.Mbarawa akizungumza katika mkutano huo amezisihi nchi wananchama za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza kasi ya kutekeleza miradi inayopangwa katika ngazi ya Jumuiya kwa kuzingatia ukomo wa tarehe.


Mhe. Prof. Makame Mbarawa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akisaini taarifa ya mkutano mara baada ya  majadiliano

Kutoka kushoto  Bibi. Zaina Ibrahim Mwalukuta Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Dkt. Leonard Chamuriho Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Maria Sassabo Katibu Mkuu Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mhandisi Happiness Mgalula Mkurugenzi wa barabara, Wizara ya Ujuenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Ujenzi wakifuatilia mkutano

Meza kuu ikiongoza mjadala wakati wa mkutano

Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mkutano


Mhe. Prof. Mbarawa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza wakati wa mkutano

JAJI IMANI ABOUD ASHINDA UCHAGUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU


Jaji Imani Aboud wa Tanzania


JAJI IMANI ABOUD WA TANZANIA ASHINDA UCHAGUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU


Mkutano wa 33 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaoendelea Jijini Nouakchott, Mauritania kwa siku mbili, leo tarehe 29 Juni, 2018 umefanya uchaguzi wa Majaji wanne wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
Mgombea wa Tanzania Mhe. Jaji Imani D. Aboud ameshinda uchaguzi huo kwa kura 47 kati ya kura 50 zilizopigwa na kufanikiwa kuchukua nafasi ya Jaji Solomy Balungi Bossa wa Uganda aliyejiuzulu nafasi hiyo kabla ya kumaliza kipindi chake.
Kwa ushindi huo, Mhe. Jaji Aboud atakuwa Jaji wa Mahakama hiyo akiwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka miwili.
Majaji wengine walioshinda kwenye uchaguzi huo ni pamoja na Jaji Kioko Ben (Kenya), Jaji Tchikaye Balise (Jamhuri ya Congo), na Jaji Anukam Stella Isibhkhomen (Nigeria).
Ushindi huu unadhihirisha uwezo mkubwa alionao Mhe. Jaji Aboud na heshima kubwa iliyonayo nchi yetu katika Bara la Afrika.
-Mwisho-


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 29 Juni, 2018