Thursday, December 10, 2020

JOB ANNOUNCEMENT AT THE AFRICAN DEVELOPMENT BANK - AfDB



 

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, MHE. OLE NASHA ALIVYOPOKELEWA WIZARANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Amina Abdallah  ikiwa ni ishara ya kukaribishwa mara alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa Ikulu tarehe 9 Desemba 2020.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimkaribisha Wizarani Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha mara baada ya kula kiapo Ikulu tarehe 9 Desemba 2020
Mhe. Prof. Kabudi akimtambulisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi kwa Naibu Waziri Mhe. Ole Nasha wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Mhe. Prof. Kabudi akimtambulisha Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Alex Mfungo kwa Naibu Waziri Mhe. Ole Nasha wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Mhe. Ole Nasha akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Wizarani

Mhe. Ole Nasha akiwa ofisini kwake baada ya kuwasili Wizarani

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimkabidhi  Mhe. Ole Nasha Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama moja ya kitendea kazi chake anapoanza majukumu yake mapya Wizarani 


Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi kwa pamoja na Sehemu ya Menejimenti ya Wizara  wakimsikiliza Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha alipozungumza nao mara baada ya kupokelewa rasmi Wizarani
 Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Caesar Waitara wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Agnes Kayola wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Swalehe Chondoma wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salifius Mligo wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani.

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Japhary Kachenje wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Agnela Nyoni wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Caroline Chipeta wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Masoud Balozi wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Macocha Tembele wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Aman Mwatonoka wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Emmanuel Buhohela wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw.  Gwamaka Lazarous wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani




Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Isaac Kalumuna wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Leonce Bilauri wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani


Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani
Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani

Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na mmoja wa Watumishi wa Wizara waliofika kumpokea  alipowasili Wizarani
aibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Wizara mara baada ya  Wizarani baada ya kuapishwa

Mhe. Prof. Kabudi akiwa na Mhe. Ole Nasha wakizungumza na Watumishi wa Wizara

Picha ya pamoja  kati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (wa tatu kushoto mstari wa kwanza)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha (wa nne kulia mstari wa kwanza) pamoja na Watumishi wa Wizara walioshiriki mapokezi ya Mhe. Ole Nasha alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa  
==========================================

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha ameahidi ushirikiano kwa Watumishi wa Wizara katika kuhakikisha Wizara inakuwa na matokeo chanya yenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mhe. Ole Nasha ameyasema hayo aliwapowasili Wizarani mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla iliyofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma tarehe 9 Desemba 2020.

Mhe. Ole Nasha ambaye alipokelewa na Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa yupo tayari kujifunza kutoka kwa Watumishi wote ili kuiwezesha Wizara kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake. Prof. Kabudi alimhakikishia Mhe. Ole Nasha ushirikiano wake binafsi na kutoka kwa Watumishi wote na kwamba uwepo wake utaongeza nguvu za kuifikisha Wizara katika viwango vya juu kiutendaji.



























 

Tuesday, December 8, 2020

HABARI KATIKA PICHA MAHAFALI YA 50 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya vitabu Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha salamu za Serikali kwenye mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi moja kati ya zawadi Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku shahada ya heshima Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah


Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa ukumbini tayari kwa ajili ya kutunukiwa shahada  


Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Nchini wakifuatilia sherehe za mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


FURSA YA AJIRA


 

Monday, December 7, 2020

WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI WAPIGWA MSASA KUHUSU MANUNUZI YA UMMA

Mkurugenzi wa Rasilimali watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Alex Mfungo akizungumza na Wakurugenzi Idara na wakuu wa Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ( hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya manunuzi ya Umma yanayofanyika Mkoani Morogoro

TANZANIA, NAMIBIA ZAKUBALIANA KUIMARISHA SEKTA ZA UVUVI NA MIFUGO

Katika jitihada za kuendeleza Diplomasia ya Uchumi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekubaliana na Jamhuri ya Namibia kuimarisha sekta za uvuvi na mifugo.

Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekubaliana na Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Uvuvi pamoja na Sekta ya Mifugo.

"Tumekubalina kuimarisha ushirikiano katika enao la uvuvi wa bahari kuu lakini pia kuwahamasisha wadau wa sekta binafsi kutoka Tanzania na Namibia kuwekeza katika eneo hilo. Kwa upande wa mifugo na uuzaji wa nyama nchi za nje Namibia wamepiga hatua kubwa sana na sasa wanauza nyama Ulaya na Asia," Amesema Prof. Kabudi

Aidha, Prof. Kabudi ameongeza kuwa wamekubaliana pia kuhamasisha sekta binafsi kutoka Namibia kuja kuwekeza katika machinjio na viwanda vya kusindika nyama hapa nchini (Tanzania) kwa ajili ya kuuza nyama hiyo nje ya Tanzania na kuendeleza sekta za uvuvi na mifugo.

Pamoja na mambo mengine, kikao cha leo kimepitia makubaliano ya miaka miwili iliyopita ambapo Tanzania na Namibia zimekubaliana kutumia fursa zilizopo kati yao kuendeleza sekta za uwekezaji, uvuvi, kilimo na mifugo kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah amesema kuwa wamekubaliana kuimarisha sekta mbili ambazo ni Uvuvi na mifugo pamoja na kilimo kwa ujumla kwa kuzingatia mazingira bora ya uwekezaji na biashara ndani ya Umoja wa Afrika (AU).

"Kuna maeneo mbalimbali ambayo kwa pamoja tumekubaliana kuyaimarisha ikiwemo uvuvi, mifugo na kilimo kwa ujumla, kupitia kikao cha leo tunaamini kuwa wawekezaji kutoka Namibia watakuja kuwekeza Tanzania na vilevile wawekezaji kutoka Tanzania watawekeza Namibia," Amesema

Ameeleza kuwa Namibia itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika kuhakikisha kuwa wanakuza uchumi wa nchi zetu zote mbili na Afrika kwa ujumla kwa kuzingatia misingi ya biashara na uwekezaji iliyopo ndani ya Umoja wa Afrika (AU).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi katika picha ya pamoja. Kushoto mwa Mhe. Ndaitwah ni Balozi wa Namibia hapa nchini, Mhe. Theresia Samaria ambaye amamaliza muda wake wa utumishi, na Kulia mwa Prof. Kabudi ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Bw. Frank Mwega. 


Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Ndaitwah akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi zawadi za vitabu