Thursday, June 17, 2021

WAZIRI MULAMULA AFUNGUA MKUTANO WA MABALOZI WA EAC AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA EAC JIJINI ARUSHA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata  Mulamula akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt.Peter Mathuki muda mfupi baada ya kuwasili katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo jijiini Arusha leo.


Mhe. Waziri Mulamula  akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe.Martin Ngoga  katika Makao Makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mh.Jaji Nestory Kayobera akimkabidhi Waziri Mulamula  machapisho mbalimbali yahusuyo Mahakama hiyo wakati Mhe. Waziri alipomtembela Rais huyo ofisini kwake makao makuu ya Mahakama hiyo iliyopo jijii Arsuha.

Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mh.Jaji Nestory Kayobera akimtembeza Mhe.Waziri Mulamula katika chumba cha Mahakama hiyo.

Mhe. Waziri Balozi Mulamulla akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha                                                                
  
  
Mhe. Waziri Balozi Mulamulla akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha leo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (MB) ametembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyopo Jijii Arusha. 

Mhe. Balozi Mulamula amefungua Mkutano wa Mashauriano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Taasisi za Jumuiya hiyo yenye makao yake Makuu jijini Arusha. 

Mhe. Mulamula kwanza amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Peter Mathuki na baadaye amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mhe. Jaji Nestory Kayobera katika Makao Makuu ya jumuiya hiyo. 

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Mulamula pia amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe.Martin Ngoga. Mikutano kati ya Mhe. Waziri na Mhe. Ngoga umefanyika katika Makao Makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

NAIBU WAZIRI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAANDAAJI MASHINDANO YA UREMBO AFRIKA MASHARIKI

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwake jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota akizungumza wakati Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati walipokutana na akizungumza na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwa Naibu Waziri jijini Dodoma

Makamu Rais wa Kamati ya Waandaaji wa Mashindano ya Urembo Afrika Mashariki bi Jolly Mutesi wa Rwanda (katikati) akizungumza akiwa na bi Mariam Ikoa kutoka Tanzania wakia na naibu Waziri Ofisini kwake jiini Dodoma.

mazungumzo yakiendelea

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (walioko Kulia kwake) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodom


Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kufanya mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwake jijini Dodoma.

Waandaaji hao ni  bi Jolly Mutesi ambaye ni makamu wa Rais anayetokea nchini Rwanda na bi Mariam Ikoa ambaye ni muandaaji wa kimataifa anayetokea Tanzania.

Katika mazungumzo hayo  na waandaaji hao wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk amewapongeza waandaaji hao  kwa kuja na wazo  hilo pamoja na kutaka kufahamu miongozo na itifaki za kufuatilia ili kufanikisha mashindano hayo.

Akizungumza  katika kikao hicho Mratibu wa mashindanoo hayo Bi Mariam Ikoa amemuelezea Mhe. Naibu Waziri Mbarouk kwamba ujio wao Wizarani una lengo la kujitambulisha pamoja na kupata miongozo na itifaki za jinsi ya kuendelea na taratibu za mashindano hayo ya urembo kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema mashindano hayo yamepangwa  kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi Novemba 20 2021

SADC yaitaka EU Kuiondolea Vikwazo Zimbabwe

SADC yaitaka EU Kuiondolea Vikwazo Zimbabwe

Na Mwaandishi Maalum, Dodoma

Tanzania imeendelea kutoa wito wa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi Zimbabwe, ambavyo vimetajwa kuwa vinadumaza jitihada za nchi hiyo za kujiletea maendeleo. Wito huo umetolewa wakati wa Mkutano wa majadiliano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 16 Juni 2021.


“Hakuna sababu ya kuendelea kuiwekea vikwazo Zimbabwe ilihali imefanya mabadiliko ya kimfumo katika maeneo mengi yakiwemo ya siasa, uchumi na mifumo ya sheria”, walisikika wakisema Mawaziri wa SADC, baada ya ujumbe wa Tanzania ambao uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) kuwasilisha hoja hiyo.

Ikijibu hoja hiyo, EU kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Mhe. Augusto Santos Silva ilisisitiza umuhimu wa Zimbabwe kuendelea kufanya mabadiliko katika mifumo yake na kudai kuwa vikwazo vilivyosalia havina athari yoyote kwa watu wa Zimbabwe. Ilisema, licha ya vikwazo hivyo, EU imeendelea kushirikiana na Zimbabwe kwa kuipatia misaada ya maendeleo na ya kibinadamu ambapo Euro milioni 366 na milioni 66 mutawalia zimetolewa kwa Zimbabwe katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

 

Katika majadiliano hayo yenye lengo la kusaidia kukuza uchumi na maendeleo katika kanda ya SADC, Waheshimiwa Mawaziri walijadili kuhusu janga la UVIKO-19 na athari zake katika ukuaji wa uchumi na mikakati ya kujikwamua kiuchumi baada ya ugonjwa huo kudhibitiwa. EU iliahidi kuendelea kushirikiana na nchi za SADC kupitia programu mbalimbali zikiwemo za kuhakikisha kuwa kila mtu anapata chanjo na programu nyingine za unafuu wa kulipa madeni na misaada ya fedha za kukabiliana na athari za UVIKO-19.

Kuhusu mikakati ya kukabiliana na UVIKO-19, Nchi za SADC kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Mhe. Verónica Macamo alizihimiza nchi za EU kuzijengea uwezo nchi za SADC wa kutengeneza vifaa vya kukabiliana na UVIKO-19 badala ya kuagiza vifaa hivyo kutoka nchi zilizoendelea.

Kwa upande wa agenda ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC, Waheshimiwa Mawaziri walieleza kuwa hali ni ya kuridhisha, isipokuwa kumekuwepo na matishio na mashambulizi ya kigaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Msumbiji. EU iliahidi kuendelea kushirikiana na nchi hizo ili kukabiliana na changamoto za kiusalama katika Mashaiki ya DRC na jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.

Nchi za SADC, zilitoa shukrani kwa misaada ya kiusalama inayopokea kutoka EU na kuzisihi nchi hizo kuendelea kutoa misaada hiyo kwa kuwa suala la ulinzi na usalama ni ndiyo moyo wa progarumu za ushirikiano wao kuendelea. Kutokana na umuhimu wa usalama katika kanda, EU iliombwa kuunga mkono mchakato wa uanzishaji wa Kituo cha Kukabiliana na Ugaidi cha SADC (SADC Regional Counter Terrorism Centre-RCTC).

Suala lingine lililojadiliwa na Waheshimiwa Mawaziri ni biashara na uwekezaji ambapo EU imepongeza jitihada zinazoendelea za kuwa na Soko Huru la SADC-EAC-ECOWAS na la Bara la Afrika (AFCFTA). Ilielezwa kuwa masoko hayo itakuwa chachu katika uwekezaji, ujenzi wa miundombinu, kuongezeka kwa ajira na kumaliza umasikini barani Afrika.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya Mtandao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk akifuatilia majadiliano ya Mkutano wa  Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya Mtandao.


Maafisa waandamizi kutoka taasisi za Serikali wakifuatilia majadiliano ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya Mtandao. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Mteule Agnes Kayola na Bw. Joseph Haule kutoka Wizara ya Fedha na Mipango kabla ya kuanza  Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya Mtandao.