Tuesday, November 30, 2021

MKUTANO WA NANE WA MAWAZIRI WA JUKWAA LA USHIRIKIANO KATI YA CHINA NA AFRIKA WAANZA


Rais wa Senegal  na Mwenyekiti Mwenza wa mkutano wa Nane wa  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC)Mhe. Macky Sall akihutubia wakaati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Abdou Diouf ulioko jijini Dakar.

Rais wa China na Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa nane wa  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) Mhe. Xi Jinping na viongozi wengine ambao walihutubia katika ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya mtandao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaariki Balozi Liberata Mulamula akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa nane wa  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC)jijini Dakar , Senegal.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza kitu na mmoja wa wa shiriki wa Mkutano wa nane wa  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaofanyika jijini Dakar , Senegal.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa nane wa  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaaofanyika jijini Dakar , Senegal.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine (kushoto)  huku Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil (kulia) akisikiliza baada ya ufunguzi wa Mkutano wa nane wa  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC)jijini Dakar , Senegal.

Mkutano wa Nane wha  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) umefunguliwa rasmi jijini Dakar nchini Senegal na kuhutubiwa na wenyeviti wenza kwa njia ya mtandao na moja kwa moja.

Awali mwenyekiti mwenza na Rais wa Senegal Mhe. Macky Sall alihutubia mkutano katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Abdou Diouf ulioko jijini Dakar.

Baadaye mwenyekiti mwenza ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping alihutubia mkutano huo kwa njia ya mtandao akiwa nchini China.

Mkutano huo wenye kauli mbiu ya “kuimarisha ubia wa  China na Afrika na kukuza maendeleo endelevu na kujenga jamii ya China-Afrika yenye  kesho ya pamoja katika zama mpya” unahudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya China Mhe. Wang Yi na Mawaziri wengine wa Mambo ya Nje akiwamo Balozi Liberata Mulamula .

Katika ufunguzi wa Mkutano huo ulihutubiwa pia kwa njia ya mtandao na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Felix Tshisekedi, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais wa Visiwa vya Comoro Mhe. Asumani Azali, Rais wa Umoja wa Afrika Mhe. Ndiya Musa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Getterez.

Viongozi hao wote kwa umoja wao wameelezea kuridhishwa kwao na ushirikiano imara uliopo kati ya China na Afrika na kupongeza juhudi zozote zinazochukuliwa katika kuimarisha zaidi uhusiano huo.

Viongozi hao pia wameelezea juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na nchi na viongozi wao katika harakati za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maelfu ya watu wa Afrika wanapatiwa chanjo kama njia mojawapo ya kukabiliana na virus hivyo.

Pia wameongelea juu ya hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na nchi husika katika kuhakikisha mabadiliko ya hali ya hewa hayaleti changamoto zaidi kwa nchi zao.

 Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamesisitiza juu ya umuhimu wa kuendelea kuzingatia uimarishaji na ukuzaji wa demokrasia, haki za binadamu, usawa wa kijinsia na utawala wa sheria katika nchi zao

Katika hotuba yake rais wa China aliahidi kutoa dozi bilioni moja za chanjo ya covid 19 kwa nchi za Afrika ikiwa ni ziada ya dozi ambazo zimeshatolewa na China kwa nchi hizo.

 

Monday, November 29, 2021

MKUTANO WA NANE WA JUKWAA LA USHIRIKIANO KATI YA CHINA NA AFRIKA KUANZA LEO

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine katika kikao cha 15 cha maafisa waandamizi kutoka nchi za Afrika na China katika kikao cha maandalizi ya Kikao cha Nane cha  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba ,2021 jijini Dakar nchini Senegal.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha maandalizi ya Kikao cha Nane cha  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 jijini Dakar nchini Senegal .

Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Afrika katika kikao cha maandalizi ya Kikao cha Nane cha  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 jijini Dakar nchini Senegal .

Washiriki  wa kikao cha maandalizi ya Kikao cha Nane cha  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 jijini Dakar nchini Senegal wakifuatilia kikao hicho .

Washiriki  wa kikao cha maandalizi ya Kikao cha Nane cha  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 jijini Dakar nchini Senegal wakifuatilia kikao hicho .

Ujumbe wa Tanzania katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao cha maafisa waandamizi kwa ajili ya kuandaa kikao cha Nane cha  Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 jijini Dakar nchini Senegal .




 

Na mwandishi wetu, Dakar

 

Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaanza leo tarehe 29 hadi 30 Novemba 2021 jijini Dakar nchini Senegal.

Maafisa waandamizi kutoka katika nchi za Afrika na Jamhuri ya Watu wa China wamekamilisha maandalizi  yaliyokuwa yanahitajika ya mkutano huo, kwa kupitia na kukubaliana na nyaraka za taarifa za utekelezaji wa miaka mitatu baada ya kikao cha saba katika kikao kilichofayika tarehe 28 Novemba, 2021.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine ameongoza ujumbe wa Tanzania hicho, ambacho pia kilihudhuduriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mpango Zanzibar Dkt. Juma Akil, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bibi Amina Shaaban, Balozi wa Tanzania Nigeria ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchni Senegal Dkt. Benson Bana na Balozi Ceasar Waitara Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mkutano huo wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, utakuwa chini ya Wenyekiti Wenza wa Rais wa Jamhuri ya Senegal Mhe. Macky Sall na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping ambao pia watahutubia wakati wa ufunguzi wake.

Mkutano huo unatarajiwa kufanya maamuzi na kutoa maelekezo kuhusu utekeleaji wa masuala ya namna ya kuendelea kukabiliana na virusi vya ugonjwa wa Korona, ushirikiano kati ya China na Afrika, Ushirikiano wa Kisiasa, Ushirikiano wa Kiuchumi, Ushirikiano wa Maendeleo ya Kijamii, Utamaduni na Ushirikiano kati ya Watu na Watu, Ushirikiano wa Ulinzi na Usalama, Mapinduzi ya Kijani, Ubadilishanaji Uzoefu katika masuala ya Uongozi Bora pamoja na Maendeleo ya Kitaasisi ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika na mabadiliko ya tabia nchi.


HABARI PICHA: RAIS WA JAMHURI YA UGANDA AHITIMISHA ZAIRA YAKE YA KIKAZI YA SIKU TATU NCHINI



Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshiwa Yoweri Kaguta Museveni wakikata utepe wakati wakuzindua rasmi Shule ya Awali na Msingi ya "Museveni Pre & Primary School" iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita

********
Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda leo tarehe 29 Novemba, 2021 amehitimisha ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini, na kurejea nchini Uganda ambapo ameagwa rasmi na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Geita uliopo wilayani Chato. 

Akiwa Wilayani Chato, Rais Museveni amekabidhi majengo ya Shule ya Awali na Msingi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyopo katika kijiji cha Nyabilezi wilayani Chato. Ujenzi wa Shule hiyo umegharimu jumla ya Dola za Marekani Milioni 1.67, yamefanyika wakati muafaka ambapo itaongeza fursa kwa wanafunzi wote kupata elimu hata kwa wale wenye mahitaji maalum.

Rais Samia sambamba na kupokea majengo ya shule hiyo ameelezea kuwa shule hiyo ni matunda ya ushirikiano na uhusiano mzuri uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Uganda.
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni wakiondoa kitambaa wakati wakizindua rasmi Shule ya Awali na Msingi Museveni Pre & Primary School iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita.
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni wakiwa katika ukaguzi wa baadhi ya majengo ya Shule ya Awali na Msingi ya Museveni Pre & Primary School iliyopo Wilayani Chato, Geita
Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni  Rais wa Jamhuri ya Uganda akimkabidhi mfano wa funguo, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya uzinduzi kama ishara ya makabidhiano ya Shule hiyo ya Awali na Msingi

Taswira ya sehemu ya jengo la Shule ya Awali na Msingi ya Museveni Pre & Primary School iliyopo Wilayani Chato, Geita
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiagana na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa ndege wa Chato Geita baada ya kukamilisha ziara yake ya Kitaifa ya siku tatu hapa nchini

Sunday, November 28, 2021

TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO JUKWAA LA USHIRIKIANO KATI YA CHINA NA AFRIKA

 


Na mwandishi wetu, Dakar

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaoanza leo tarehe 28 hadi 30 Novemba 2021 jijini Dakar nchini Senegal.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ataongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo.

 

Katika Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, Marais wa Nchi Wenyeviti Wenza wa Mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Senegal Mhe. Macky Sall na Rais  wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping watahutubia Mkutano huo.

 

Mkutano huo wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika unatanguliwa na Mkutano wa Maafisa Waandamizi unaoanza leo tarehe 28 Novemba 2021 hapa Jijini Dakar, Senegal ambapo  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mpango Zanzibar Dkt. Juma Akil na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bibi Amina Shaaban watashiriki.

 

Mkutano huo utakaowashirikisha viongozi na wawakilishi kutoka nchi za Bara la Afrika na Jamhuri ya Watu wa China pamoja na mambo mengine utajikita katika majadiliano ya maeneo yafuatayo:- Ushirikiano wa Kisiasa, Ushirikiano wa Kiuchumi, Ushirikiano wa Maendeleo ya Kijamii, Utamaduni na Ushirikiano kati ya Watu na Watu, Ushirikiano wa Ulinzi na Usalama, Mapinduzi ya Kijani, Ubadilishanaji Uzoefu katika masuala ya Uongozi Bora pamoja na Maendeleo ya Kitaasisi ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

RAIS SAMIA NA RAIS MUSEVENI WAFUNGA KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museven wameshiriki katika kufunga Kongamano la Wafanyabiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam

Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wameahidi kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika sekta ya nishati na gesi ili kufungua fursa kwa wananchi wa pande zote mbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufungaji wa Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda lililohudhuriwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufungaji wa Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda lililohudhuriwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kufunga Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda lililofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam  


Baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali wakifuatilia ufungaji wa Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda lililofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam  


Sehemu ya Mawaziri na Wafanyabiashara wakifuatilia ufungaji wa Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda lililofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam