|
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi
Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud (kulia) akizungumza na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (kushoto) aliyekwenda Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini
Riyadh kuonana naye wakati wa ziara ya kikazi nchini humo. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akiwa
katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme,
Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud (kulia) alipowasilli katika Ofisi za Wizara ya
Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini Riyadh. |
| |
|
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata
Mulamula ukiwa nje ya Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia baada ya
kumalizika kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana
Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud ulipokwenda kuonana naye katika Ofisi
za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini Riyadh |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha na makamu Mwenyekiti wa
Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia Bw. Tariq Al
Haidary walipokutana jijini Riyadh |
|
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Balozi Liberata
Mulamula katika picha ya pamoja kabla ya kikao na viongozi wa Shirikisho la
wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia kilichofanyika katika
Ofisi za Shirikisho hlo jijini Riyadh.
|
|
Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika
kikao na viongozi wa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini
Saudi Arabia kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hilo jijini Riyadh |
|
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza (katikati) na Afisa Dawati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Davis Byarugaba wakifuatilia kikao na Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda Saudi Arabia
|
|
Ujumbe wa Tanzania ukikabidhi zawadi kwa Makamu
mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi
Arabia Bw. Tariq Al Haidary baada ya kikao na viongozi wa shirikisho hilo
kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hilo jijini Riyadh |
|
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki
akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyabiashara
na wenye viwanda nchini Saudi Arabia Bw. Tariq Al Haidary baada ya kikao na
viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hlo
jijini Riyadh |
|
Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa
Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia baada ya
kikao na viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho
hilo jijini Riyadh |
Na mwandishi wetu, Riyadh
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amekutana na
kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme,
Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud alipomtembelea katika Ofisi za Wizara hiyo
jijini Riyadh- Saudi Arabia.
Katika mazungumzo yao Waziri
Mulamula amemuhakikishia mwenyeji wake Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan
Al Saud kwamba Tanzania iko tayari kushirikiana na Saudi Arabia na kuendelea
kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo.
Balozi Mulamula pia
amemuhakikishia mwenyeji wake juu ya utayari wa Tanzania katika kufanya
biashara na Saudi Arabia ikiwa ni pamoja na kuelezea fursa za uwekezaji
zilizopo Tanzania kupitia sekta za mifugo, uvuvi, kilimo, utalii na usafiri wa
anga.
Naye Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal
bin Farhan Al Saud alimuhakikishia Mhe Waziri juu ya nia na utayari wa Saudi
Arabia kufanyabiashara na kuwekeza Tanzania kwa ajili ya kuzinufaisha nchi zote
mbili.
Katika mazungumzo yao viongozi
hao wamesisitiza umuhimu wa Tanzania na Saudi Arabia kuendelea kushirikiana na
kuhakikisha biashara za uwekezaji vinashamiri baina ya nchi hizo.
Katika hatua nyingine Waziri Mulamula amekutana na
viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara na wenye viwanda wa Saudi Arabia jijini
Riyadh na kuelezea fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini na
kuainisha maeneo ya kipaumbele kwa sasa.
Maeneo yaliyoainishwa kama kipaumbele katika kikao
hicho ni pamoja na kilimo, mifugo, uvuvi, utalii na usafiri wa anga.
Waziri Muamula ametumia kikao hicho kuwaalika
nchini wanachama wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kushiriki Maonesho ya Kimaatafa
ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba yanayofanyika kila mwaka jijini
Dar es Salaam mwezi Julai
Viongozi wa jumuiya hiyo wameshukuru kupata nafasi
ya kuonana na ugeni huo kutoka Tanzania ambao ulijumuisha Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara na wenye viwanda
nchini (TCCIA) Mr. Joseph Koyi, kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini
(TIC) bibi Anna Lyimo na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka Tanzania Bara.
Waziri Mulamula na Ujumbe wake wako nchini
Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa
Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alioutoa mwezi
Machi 2021 alipotembelea Tanzania.
Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, mwakilishi wa TAWA, Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC) na wawakilishi wa Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini.
Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia
kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia,
wafanyabiashara marafiki wa Tanzania wa jijini Riyadh na Jumuiya ya
Wafanyabiashara katika miji ya Jeddah na Makkah atakaokutaana nao jijini
Jeddah. Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia kurejea nyumbani tarehe 13
Machi 2022.