Thursday, February 16, 2023
Wednesday, February 15, 2023
DT. TAX AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA 42 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA UMOJA WA AFRIKA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023.
Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 18-19 Februari 2023.
Pamoja na mambo mengine, mkutano wa Mawaziri utajadili masuala ya kimkakati yanayohusu Bara la Afrika ikiwemo utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika-AfCFTA, uhakika wa chakula, hali ya ulinzi na usalama, mabadiliko ya tabianchi, pamoja na masuala ya kiutawala na usimamizi wa rasilimali za Umoja wa Afrika.
Akichangia katika mkutano huo, Dkt. Tax alisisitiza umuhimu wa Kamisheni na Taasisi za Umoja wa Afrika kusimamia vyema rasilimali za Umoja wa Afrika kwa kuchukua hatua za kuondoa mapungufu yaliyobainika kwenye taarifa ya ukaguzi wa rasilimali za Umoja wa Afrika.
Mhe. Waziri pia alieleza hatua ambazo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inachukua katika kutekeleza Mikataba ya Uenyeji ya Taasisi za Umoja wa Afrika zilizopo Tanzania ambazo ni Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Umoja wa Posta Afrika na Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri dhidi ya Rushwa.
Awali akiwasilisha hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mhe. Moussa Faki Mahamat alisisitiza umuhimu wa Umoja wa Afrika kuendelea kutoa kipaumbele kwenye masuala yanayowagusa wananchi wa Afrika ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za mabadiliko za kijamii, kiuchumi na kiusalama. Alisisitiza umuhimu wa Afrika kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nje kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za vyakula ndani ya bara la Afrika pamoja na kutumia fursa za mkataba wa AfCFTA katika kukuza Mtangamano wa Kiuchumi.
Bw. Faki aliongeza kuwa Umoja wa Afrika umeendelea kusimamia masuala ya amani na usalama katika bara la Afrika katika nchi za Ethiopia, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Libya ambapo jitihada zilizofanyika zimelenga zaidi kupata suluhisho la amani kwa mataifa hayo.
Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Demeke Mekonnen amesema Ethiopia ameshukuru Umoja wa Afrika kwa mchango na ushirikiano wake ambao umewezesha kupatikana amani na utulivu nchini Ethiopia na kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka miwili. “Ethiopia inaamini kuwa kupitia Umoja wa Afrika amani, ulinzi na usalama vitailetea Afrika maendeleo zaidi,” alisema Mhe. Mekonnen.
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja |
Mawaziri mbalimbali walioshiriki Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023. |
Tuesday, February 14, 2023
MKUTANO WA MAJADILIANO YA KIMKAKATI YA NGAZI YA JUU KATI YA SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO WAFANYIKA
Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo katika meza kuu wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023. |
Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023. |
Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023. |
Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023 ukiendelea. |
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023 katika picha ya pamoja. |
Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati ya Ngazi ya Juu ulioshirikisha watendaji wakuu wa Serikali na wadau wa maendeleo wafanyika jijini dar es Salaam.
Akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amewahakikishia wadau wa maendeleo ushirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza kwa pamoja mipango ya maendeleo.
Balozi Mbarouk amesema kufanyika kwa kikao hicho kunadhihirisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wa maendeleo na Taasisi za Umoja wa Mataifa.
“Uwepo wenu hapa katika kikao hiki unadhihirisha ushirikiano usliopo kati ya Tanzania na wadau wa maendeleo, Sio kwamba uwepo wenu unachochea ubia wetu na kuimarisha nia yenu ya kuhakikisha tunatekeleza kikamilifu Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo ambao umelenga kutekeleza malengo Endelevu ya Milenia ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya Addis Ababa ya kuchangia maendeleo na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Balozi Mbarouk
Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye uwakilishi wao hapa nchini, wadau wa maendeleo , sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikal.
TANZANIA, COMORO KUANZIASHA TUME YA KUDUMU YA PAMOJA
Monday, February 13, 2023
Saturday, February 11, 2023
TANZANIA, IRAN KUSHIRIKIANA SEKTA ZA KIMKAKATI
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeahidi kushirikiana katika sekta za kimkakati hususani kilimo, pamoja na biashara na uwekezaji kwa lengo la kukuza na kuimarisha diplomasia ya uchumi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam.
“Tanzania na Iran tumekuwa tukishirikiana katika maeneo mbalimbali, hadi sasa tumekuwa tukishirikiana katika sekta za elimu, afya, utalii, nishati, madini. Pia kwa sasa Irani imeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo hasa ukizingatia kilimo ni kipaumbele cha Serikali,” alisema Dkt. Tax
Waziri Tax ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na Iran katika maeneo mapya ya kimkakati ikiwemo sekta ya kilimo ili kupata uzoefu katika maendeleo na uwekezaji wa kuifanya nchi kuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha pamoja na kuongeza viwanda.
Akielezea kuhusu biashara na uwekezaji, Dkt. Tax alisema kuwa kupitia kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji lililofanyika Mwezi Agosti, 2022 limefungua fursa za biashara na uwekezaji. “Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwavutia wafanyabiashara na wawekezaji wengi zaidi kuwekeza nchini,” alisema Dkt. Tax
Naye Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh alisema kuwa Iran imekuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania kwa miaka 40 hadi sasa na mataifa hayo yamekuwa yakishirikiana kijamii, kisiasa, kiuchumi na utamaduni kwa maslahi ya pande zote mbili.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Tanzania zimekuwa marafiki wa muda mrefu na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuimarisha sekta za kilimo, elimu, afya pamoja na biashara na uwekezaji kwa maslahi ya mataifa yote mawili.
Balozi Alvandi aliongeza kuwa mazingira ya biashara kati ya Iran na Tanzania yanaridhisha kwani hadi mwaka jana 2022 biashara kati ya Iran na Tanzania iliongezeka kutoka dola milioni 20 hadi dola milioni 70.
“Biashara kati ya Iran na Tanzania imeongezeka kutoka dola milioni 20 hadi dola milioni 70 mwaka jana, hii ni ishara kuwa uchumi wa mataifa yetu mawili unazidi kuimarika,” alisema Balozi Alvandi
Tanzania na Iran zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1983 na zimekuwa zikishirikiana katika sekta za biashara, kilimo, masoko, utalii, uwekezaji, afya, madini, nishati na utaalamu.
WAZIRI TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA MISRI, MAREKANI
Friday, February 10, 2023
DKT. TAX ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA UTURUKI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam, kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki tarehe 6 Februari, 2023.
Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Dkt. Tax ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Uturuki na kuwasihi kuendelea kuwa wavumilivu wakati huu wa msiba mkubwa kwa Taifa hilo uliosabaisha vifo vya watu zaidi ya 18,000.
“Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla tunaungana na Serikali ya Uturuki katika kuombeleza msiba huo mzito,” alisema Dkt. Tax.
Mwaka 1999 Uturuki ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambapo watu wapatao 17,000 walipoteza maisha kutokana na tetemeko hilo. Kadhalika, mwaka 2011 ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika mji wa Van lilipelekea vifo vya watu 500.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam |
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA UCHUKUZI, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) ukiendelea jijini Bujumbura, Burundi |
Thursday, February 9, 2023
TANZANIA YAJIZATITI KUTUMIA FURSA ZINAZOPATIKANA NDANI NA NJE YA NCHI KUKUZA UCHUMI
Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kushirikiana
na nchi mbalimbali duniani ili kukuza uchumi
wa nchi kupitia fursa za biashara, uwekezaji na utalii zilizopo ndani na nje ya
nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Bungeni leo tarehe 09
Februari,2023 wakati akijibu swali la Mhe.
Felista Njau, Mbunge wa Viti Maalum kuhusu umuhimu
wa Serikali wa kuainisha nchi zenye fursa za biashara na uwekezaji ili kukuza
pato la Taifa.
Amesema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa
kushirikiana na Wizara za kisekta na Balozi za Tanzania imeendelea kutangaza
fursa za biashara na uwekezaji zenye manufaa kwa Taifa na kwamba Wizara
inaandaa Mpango wa Kitaifa wa kutekeleza Diplomasia ya Uchumi utakaojumuisha
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kufikia malengo tarajiwa.
Amesema Mpango huu ambao unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Desemba
2023, pamoja na mambo mengine unalenga kuhakikisha fursa za biashara, uwekezaji
na utalii zinakuwa na tija zaidi kwa wananchi wa Tanzania. Pia Mpango huo
utajumuisha Sekta zote husika ikiwa ni pamoja na kuainisha maeneo muhimu ya
kisekta yatakayo changia katika kukuza uchumi na pato la Taifa.
Akichangia hoja kuhusu mkakati wa utoaji elimu kwa wananchi kuhusu dhana ya Diplomasia ya Uchumi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, amesema Wizara inaendelea kutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali na kufafanua kwamba Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi unaoandaliwa pia utajumuisha Mpango wa kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana hiyo ili kuwawezesha wananchi kuielewa dhana hii na kuwawezesha kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali.
Kuhusu taarifa hasi zinazotolewa na vyombo vya kimataifa dhidi ya Tanzania, Mhe. Dkt. Tax amesema tayari Wizara imeanza kushirikiana na vyombo vya habari vya Nje hususan vile vinavyorusha matangazo yake kwa Kiswahili ili kupitia vyombo hivyo fursa na taarifa chanya kuhusu Tanzania zitangazwe duniani kote.