Friday, March 8, 2024

WANAWAKE WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WALIVYOADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Watumishi Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na wanawake wengine duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake leo Machi 8, 2024.

 

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yamefanyika kitaifa jijini Dodoma katika Wilaya ya Chamwino ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima.

 

Pamoja na mambo mengine, uzinduzi wa Sera wa Taifa ya Maendeleo ya Wanawake umefanyika wakati wa maadhimisho hayo yenye kaulimbiu isemayo “Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (wa pili kulia) akiwasalimia Watumishi Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) walipopita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika Wilayani Chamwino jijini Dodoma tarehe 08 Machi 2024. Kulia kwa Mhe. Dkt. Gwajima ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule
Sehemu ya Watumishi Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliopo Dodoma wakipita kwa furaha mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Shamrashamra zikiendelea
Sehemu nyingine ta watumishi wanawake wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo
Picha ya pamoja

Watumishi hao wakiwa na bango lenye kaulimbiu ya maadhimisho hayo

Shamrashara za maadhimisho ya siku ya waawake zikiendelea

Sehemu ya watumishi wanawake wa Wizara wakati wa maadhimisho hayo


Sehemu ya watumishi wanawake wa Wizara wakati wa maadhimisho hayo

Watumishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara za Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Mpango wa Hiari wa Afrika wa kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) na Kituo cha Usiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Dodoma

...Maadhimisho katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


Sehemu ya Watumishi Wanawake wa Wizara waliopo Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam nao hawakubaki nyuma kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kama wanavyoonekana pichani.

Watumishi hao wakiwa katika picha ya pamoja



 

Wednesday, March 6, 2024

WIZARA YA MAMBO YA NJE KUSHIRIKI MAONESHO MAALUM KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashiriki maonesho maalum ya wanawake yanayofanyika kimkoa katika viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024 ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika duniani kote tarehe 08 Machi 2024.


Maonesho hayo ambayo yanaratibiwa na  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma yatafunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Rosemary Senyamule tarehe 07 Machi 2024.


Huduma zitakazotolewa katika Banda la Wizara wakati wa maonesho hayo ni pamoja na uthibitishaji wa nyaraka mbalimbali ikiwemo vyeti vya taaluma, ndoa na nyaraka nyingine, zoezi ambalo litaanza rasmi tarehe 07 hadi 11 Machi, 2024.


Taarifa nyingine  ni kuhusu utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje na  mchango wa wanawake kwenye medani za kimataifa na diplomasia.

Kadhalika maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim zamani Chuo cha Diplomasia; Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) na Mpango wa Hiari wa Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) yatatolewa.


Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2024 yamebeba kaulimbiu isemayo "Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii". 

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Kawina Kawina akimsikiliza Afisa Mambo ya Nje, Bi. Elizabeth Bukwimba akimweleza kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya ushiriki wa Wizara kwenye maonesho maalum yatakayofanyika katika Viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07  hadi 11 Machi 2024 ikiwa ni maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa duniani kote tarehe 08 Machi 2024. Bw. Kawina ametembelea banda hilo tarehe 06 Machi 2024 kukagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya ushiriki wa Wizara
Bw. Kawina akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara kukagua maandalizi  ya ushiriki wa Wizara katika maonesho maalum kuelekea siku ya wanawake duniani yanayofanyika  katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024. Wanaoshuhudia ni Watumishi kutoka Taasisi za Wizara akiwemo Badriya Masoud (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa APRM, Bi. Praxeda Gaspar kutoka APRM na Bi. Susan Masawe kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim


Bw. Kawina akikagua vipeperushi vitakavyogawiwa kwa wananchi watakaotembelea banda la Wizara wakati wa maonesho maalum kuelekea siku ya wanawake duniani yanayofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 07 hadi 11 machi 2024

Afisa kutoka Taasisi ya Wizara ya Mpango wa Hiari wa Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM), Bi. Praxeda Gaspar akimpatia Bw. Kawina kipeperushi kuhusu Taasisi hiyo

Bw. Kawina akipata maelezo kutoka kwa Bi. Janeth Benedict kutoka  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC)  kuhusu vipeperushi watakavyosambaza kwa wananchi kuhusu taasisi hiyo

Mwonekano wa Banda la Wizara



 

BALOZI MUSSA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA FEDHA CHA SADC

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameendelea kuongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha Kamati ya Fedha ya Jumuiya ya Maendeleo Kusaini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika Jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.


Pamoja na masuala mengine, kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa ya Kamati Ndogo ya Fedha ya SADC na Kamati ya Ukaguzi ambapo ajenda mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo mpango wa bajeti ya kanda kwa kipindi cha 2024/2025 na mapendekezo yake yatawasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuidhinishwa tarehe 10 na 11 Machi, 2024.

Kutoka kulia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Afisa kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Joseph Haule na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Noah Mboma wakifuatilia majadiliano katika Kikao cha Kamati ya Fedha cha SADC kinachoendelea jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikifuatilia majadiliano ya Kikao cha Kamati ya Fedha kinachoendelea jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.

Balozi Mussa akiteta jambo na sehemu ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Tanzania na Afrika Kusini.




 

Monday, March 4, 2024

TANZANIA, MOROCCO KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Tanzania na Morocco zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri Makamba amesema kuwa Tanzania na Morocco zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia wa imara na wa muda mrefu, hivyo ni vyema kwa mataifa hayo kujikita zaidi kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi wa pande zote mbili.

Naye Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Koumiri amesema kuwa Morocco itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akimkaribisha Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri  kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba katika picha ya pamoja na ujumbe wa Morocco ukiongozwa na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Guomiri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE ASHIRIKI MKUTANO WA KAMATI YA KUDUMU YA MAKATIBU WAKUU WA SADC


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024.

Kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha Kamati ya Fedha tarehe 6 Machi, 2024 ambapo kwa pamoja vikao hivyo ni maandalizi ya Baraza la Mawaziri litakalofanyika tarehe 10 - 11 Machi, 2024 jijini Luanda, Angola.

Aidha, pamoja na mambo mengine vikao hivi vya awali vitapokea na kujadili taarifa zifuatazo: Tathmini ya utekelezaji wa maamuzi ya Mikutano iliyopita, Hatua iliyofikiwa katika kugharamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo wa SADC wa 2020–2030, Taarifa  ya Kamati ya Fedha, Taarifa ya Kamati ya Rasilimali Watu na Utawala, Hatua iliyofikiwa katika kutafsiri nyaraka muhimu za SADC kwa lugha ya Kiswahili na nyinginezo.

Kauli mbiu ya Baraza la Mawaziri la mwaka huu ni ‘’Rasilimali Watu na Fedha: Nyenzo muhimu kwa ukuaji Endelevu wa Viwanda katika Kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”.


      Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024.

       Meza kuu ikiongoza majadiliano katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024. Katikati ni Katibu Mtendaji wa SADC, Bw. Elias Magosi na kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji wa SADC, Bi. Angele  Makombo N’tumba

   Ujumbe kutoka Eswatin ukifuatilia Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

Kikao kikiendelea.

     Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa SADC wanaoshiriki Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024.







WAZIRI MAKAMBA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE UJERUMANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayehusika na Afrika, Mhe. Katja Keul, jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani. Uhusiano baina ya Tanzania na Ujerumani ni ya kihistoria na yanaonekana katika sekta za utalii, elimu, afya, utamaduni, biashara na uwekezaji pamoja na ushirikiano kupitia miji dada (Twin sister city relations).

Mhe. Keul aliwasili nchini tarehe 29 Februari 2024 kwa ziara ya kikazi ya siku nne (4) ambapo amehitimisha ziara yake nchini leo tarehe 04 Machi, 2024. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayehusika na Afrika, Mhe. Katja Keul, jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayehusika na Afrika, Mhe. Katja Keul, walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam

Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayehusika na Afrika, Mhe. Katja Keul, kikiendelea jijini Dar es Salaam




Friday, March 1, 2024

WAZIRI KEUL AZINDUA KITABU CHA MAISHA NA TAMADUNI ZA KICHAGA KILICHOANDIKWA KWA LUGHA YA KISWAHILI.

Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore (kulia) na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo  Dkt. Resani Mnata wakizindua  kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili katika hafla iliyofanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 01 Machi 2024.

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili

 

 

 Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo  Dkt. Resani Mnata akimkabidhi nakala ya kitabu mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Naomi Zegezege katika hafla ya kuzindua kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta (katikati) aliposhiriki hafla ya uzinduzi wa  kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili iliyofanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro



Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili



Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo  Dkt. Resani Mnata , Balozi wa Tanzania Ujerumani (wa pili kulia) wakitoa heshima katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani wakati wa utawala wao
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiweka shada la maua katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani  wakati wa utawala wao



wananchi wa kabila la Kichaga wakicheza ngoma za asili wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili

 

 

 

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul ameshiriki uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la kichaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

 

Wakati wa uzinduzi ambao umefanyika katika kigango cha Kidia,  Old Moshi, imeelezwa kuwa kitabu hicho ambacho kimetafsiri kazi ya mwandishi mchungaji Bruno Gutmann, kinalenga kutambua utumishi wa mchungaji huyo raia wa Ujerumani ambaye aliishi eneo hilo kwa miaka 28 na kushirikiana na wananchi wa maeneo hayo huku akieneza injili.

 

 

Kitabu hicho ni miongoni mwa vitabu 400 vilivyoandikwa kwa lugha ya Kijerumani na mchungaji huyo ambapo mpaka sasa vitabu vitano vimeandikwa kwa  lugha nyingine ikiwemo kichaga na kiswahili.

 

Uzinduzi huo pia umeshuhudiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Mhe. Kısare Makore, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassan Mwamweta na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Resani Mnata.

 

Naibu Waziri Keul yuko nchini kwa ziara ya siku nne ya kikazi kuanzia tarehe 29 Februari hadi Machi 4 2024.

TANZANIA NA ETHIOPIA ZASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA ZA KILIMO, NISHATI NA UTAMADUNI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia la Ethiopia zimesaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta za kilimo, nishati na utamaduni katika haflabiliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 01 Machi 2023.

Utiaji saini huo ambao umeshuhudiwa na Viongozi Wakuu  wa Nchi hizo mbili, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia la Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali ni matokeo chanya ya ziara ya Mhe. Dkt. Abiy ambaye yupo nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu. 

Kwa upande wa Tanzania, makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na kwa upande wa Serikali ya Ethiopia makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo, Mhe.  Balozi Taye Atseke Selassie.

Hati za Makubaliano zilizosainiwa na  Mhe. Makamba ni Hati ya Ushirikiano katika sekta ya Kilimo ambayo itaanzisha ushirikiano katika utafiti wa mbegu za ngano, kubadilishana uzoefu katika teknolojia ya kilimo, kilimo cha umwagiliaji, kuhudumia mazao baada ya mavuno, kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao na Kilimo cha biashara.

Pia, amesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kuhusu Biashara ya Umeme katika utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA). Hati hii imeanzisha ushirikiano katika usambazaji, biashara ya umeme na kuanzisha jukwaa la majadiliano la kuwezesha na kuanzisha biashara ya umeme utokanao na vyanzo vya maji.

Aidha, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya Sanaa na Utamaduni ambapo hati hii itaanzisha ushirikiano wa pamoja katika kuendeleza sekta ya Sanaa na utamaduni ikiwemo kushirikiana katika  matamasha ya kitamaduni,  utafiti, filamu, kuongeza ujuzi kwa wadau wa sekta hiyo na   kuandaa maonesho ya Sanaa.

Tanzania na Ethiopia zinashirikiana katika sekta za usafiri wa anga, nishati, Kilimo, mifugo, uhamiaji, biashara na uwekezaji, elimu, ulinzi na usalama.

    Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Ethiopia wakisaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta za kilimo na nishati kulia ni Mhe. January Makamba (Mb.) na kushoto Mhe.  Balozi Taye Atseke Selassie akisainiIkulu jijini Dar es Salaam tarehe 1 Machi, 2024..

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiaopia, Mhe.  Balozi Taye Atseke Selassie wakisaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya Sanaa na Utamaduni Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 1 Machi, 2024.








NAIBU WAZIRI WA MAMBO NJE UJERUMANI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Makore alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)  tarehe 29 Februari, 2024. Mhe. Keul yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku Nne.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)  tarehe 29 Februari, 2024.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya America na Ulaya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Naomi Zegezege  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)  tarehe 29 Februari, 2024.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Makore (kuli) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) tarehe 29 Februari, 2024.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Bw. Tixon Nzunda (wa pili) kulia na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta ( wa pili kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)  tarehe 29 Februari, 2024

Mazungumzo yakiendelea katika chumba cha kupumzikia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)

 

 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul amewasili nchini tarehe 29 Februari, 2024. Mhe. Keul yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku Nne.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Keul amelakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta na viongozi wengine wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Akiwa nchini Mhe. Keul atatembelea Hospitali ya KCMC, kuzuru kaburi la Mangi Meli na kutembelea Parish ya kidia ambako atahudhuria sherehe za kukumbuka maisha ya kazi za mwandishi wa Ujerumani mchungaji Bruno Gutmann aliyeishi eneo hilo kwa miaka 28 na kuzindua kitabu cha maisha ya kiutamaduni ya wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya kiswahili.

Mhe. Keul pia anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

Ziara ya Mhe. Keul pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha pia inalenga kuendelea kuimarisha Uhusiano na ushirikiano Kati ya Tanzania na Ujerumani.