Saturday, September 8, 2012

Mhe. Rais Kikwete awasili nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Maziwa Makuu


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na mwenyeji wake Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda. Mhe. Rais Kikwete yupo nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika leo tarehe 8 Septemba, 2012 jijini Kampala.


 Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Mhe. Kalonzo Musyoka, Makamu wa Rais wa Kenya walipokutana mjini Kampala, Uganda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika jijini humo leo.


Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi, akimpatia taarifa fupi Mhe. Rais Kikwete kabla Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Maziwa Makuu kuanza jijini Kampala leo.


Mhe. Rais Kikwete akielekea kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika mjini Kampala leo. Wengine katika picha ni Mhe. Nahodha (kushoto kwa Mhe. Rais) na Balozi Rajab Gamaha (kulia kwa Mhe. Rais).

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Dkt. Tomaz Agusto Salomao, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano mjini Kamapala leo.


Balozi Naimi Aziz, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda na Mratibu wa Kitaifa wa masuala ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu akiwa na Bw. Samwel Shelukindo, Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika jijini Kampala leo.


Picha na Rosemary Malale


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.