Wednesday, September 12, 2012

Rais Kikwete na Rais Kibaki wa Kenya waanza mazungumzo

   
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  pamoja na ujumbe wake na wenyeji wao wakianza Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.  Kulia kwa Rais Kikwete ni Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakipata picha ya kumbukumbu  Ikulu ya Nairobi, Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe Bernard Membe na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Profesa Sam K. Ongeri.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipongezana na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya, baada ya kuongea na wanahabari wakati wa Mazungumzo yao Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wao baada ya Mazungumzo yao Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.


Picha zote na Ikulu


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.