Wednesday, September 5, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



   
Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu na ujumbe wake anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 5 Septemba, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Akiwa nchini, Mhe. Hui ataonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kufanya mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda yatakayofuatiwa na uwekaji saini mikataba minne ya ushirikiano kati ya Tanzania na China.

Mikataba hiyo itahusu ushirikiano katika sekta ya Kilimo, msaada wa ujenzi wa Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ujenzi wa Bomba la Gesi na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Tarehe 6 Septemba 2012, Mhe Hui atatembelea jengo la ukumbi wa  mikutano la Julius Nyerere lililojengwa kwa msaada wa Serikali ya China, Reli ya Tazara na Makaburi ya Wachina huko Majohe, Pugu.  Baadaye mchana Mhe.Hui ataelekea Zanzibar kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar.

Mhe Hui anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 7 Septemba 2012 saa 6 mchana.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

4 SEPTEMBA, 2012

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.