Wednesday, September 5, 2012

Hafla ya kumuaga Balozi wa Korea Kusini hapa nchini‏



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akimtakia heri na uzima wa afya Balozi wa Korea Kusini aliyemaliza muda wake wa kazi nchini, Mhe. Young-Hoon Kim, wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika kwenye Hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam.

Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia hapa Wizarani, akisalimiana na Bibi Moon Jim Kim, mke wa Balozi wa Korea Kusini aliyemaliza muda wake wa kazi nchini.  Pichani ni Mhe. Balozi Kim.  

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akimzawadia Balozi wa Korea Kusini aliyemaliza muda wake wa kazi nchini, Mhe. Young-Hoon Kim, wakati wa hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara hiyo na kufanyika kwenye Hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam. Katikati ni mke wa Balozi Kim, Moon Jim Kim.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.