Monday, September 3, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo jioni Jumatatu, 3 Agosti, 2012 amempokea Rais wa Msumbiji  Mheshimiwa Armando Emilio Guebuza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC).
Rais Guebuza amefika nchini kuhudhuria kikao cha siku moja cha nchi tatu ambazo zinaunda Chombo cha Siasa, Ulinzi na Usalama cha SADC (TROIKA) kinachofanyika jijini Dar-Es-Salaam, kesho tarehe 4 Septemba, 2012, chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria ni Rais Jacob Zuma wa Afrika  Kusini, Rais Hifikepunye  Pohamba wa Namibia ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Troika na Rais Joseph Kabila wa DRC.
Hiki ni kikao cha kwanza tangu Tanzania ichaguliwe kushika nafasi ya uenyekiti wa TROIKA katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za SADC kilichofanyika tarehe 16 -17 Agosti, 2012  nchini Msumbiji.
Nchi tatu za TROIKA ni Afrika Kusini, Namibia na Tanzania, ambaye ndiye Mwenyekiti.
Kikao hiki ni cha mpango kazi wa TROIKA kwa mwaka mzima wa uenyekiti wa Tanzania.
Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika mpango kazi huo na ambayo Tanzania imerithi kutoka kamati iliyomaliza muda wake  ni pamoja na mgogoro wa Mashariki ya Congo DRC, mchakato wa Katiba na Uchaguzi wa Zimbabwe na suala la Madagascar.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu – Dar-Es-Salaam
3 Septemba, 2012

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.