Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana
na kupokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule wasio na makazi hapa
nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Mabalozi waliowasilisha
nakala za hati za utambulisho ni Balozi wa Ureno Mhe. Balozi Maria Amelia Maio
de Paiva mwenye makazi jijini Maputo, Balozi wa Ufilipino, Mhe. Balozi Alex G.
Chua ambae makazi yake yapo jijini Nairobi, Balozi wa Jamaica Mhe. Balozi Angela
Veronica Comfort mwenye makazi jijini Pretoria na Balozi wa Austria, Mhe.
Balozi Dkt. Christian Fellner ambae makazi yake ni Nairobi.
Wengine
ni Balozi wa Ghana Mhe. Fransisca Ashietey-Odunton mwenye makazi Jijini
Nairobi, Balozi wa Venezuele, Mhe. Jesús Agustin Manzanilla Puppo ambae makazi
yake yapo Jijini Nairobi pamoja na Balozi wa Djibouti Mhe. Balozi Yacin Elmi
Bouh mwenye makazi Nairobi.
Awali
kabla ya kukabidhi hati za utambulisho kwa Mhe. Waziri, Mabalozi wateule
walipata semina kutoka kwa Mkuu wa Itifaki, wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge.
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiangalia nakala ya hati ya utambulisho ya
Balozi wa Ureno Mhe. Balozi, Maria Amelia Maio de Paiva
|
Balozi wa
Ghana Mhe. Fransisca Ashietey-Odunton akimkabidhi Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi
(Mb) nakala ya hati ya utambulisho
|
|
Balozi wa Ufilipino, Mhe. Balozi Alex G. Chua akimsikiliza
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
Kabudi (Mb) wakati alipokuwa akipatiwa ufafanuzi wakati wa mazungumzo mara
baada ya kumkabidhi Waziri nakala ya hati ya utambulisho
|
Balozi wa
Jamaica Mhe. Balozi Angela Veronica Comfort akimkabidhi nakala ya utambulisho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akikagua nakala ya hati ya utambulisho ya Balozi
wa Austria, Mhe. Balozi, Dkt. Christian Fellner
Balozi wa
Venezuele, Mhe. Jesús Agustin Manzanilla Puppo akimfafanulia baadhi ya
maneno yaliyopo kwenye nakala ya hati ya
utambulisho Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiangalia nakala ya hati ya utambulisho kutoka
kwa Balozi wa
Djibouti Mhe. Balozi Yacin Elmi Bouh
Mkuu Mkuu
wa Itifaki, wa Wizara hiyo Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (mwenye tai ya rangi
ya chungwa) akiwapa Semina Mabalozi wateule kabla ya kuwasilisha nakala za Hati
zao kwa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mkuu Mkuu
wa Itifaki, wa Wizara hiyo Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (mwenye tai ya rangi
ya chungwa) akiwapa Semina Mabalozi Wateule
|
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.