Thursday, May 12, 2022

MWAKILISHI MKAZI WA AfDB AWASILISHA BARUA ZA UTAMBULISHO

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley amewasilisha Barua za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea barua za utambulisho, viongozi hao pamoja na mambo mengine, walijadiliana masuala ya miundombinu endelevu pamoja na uboreshaji wa mazingira katika sekta binafsi.

Bibi. Laverley amemhakikishia Balozi Mulamula ushirikiano wa kutosha kutoka AfDB katika kuchochea utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na bank hiyo hapa nchini.

Nae Balozi Mulamula amemhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini na kuonmgeza kuwa AfDB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania jambo ambalo ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na bank hiyo. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akipokea barua za utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akiagana na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



TANZANIA, JAMAICA KUONGEZA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO

Na Mwandishi Wetu, Dar 

Serikali ya Tanzania na Jamaica zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji pamoja na elimu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina Smith katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Leo nimekutana na Mhe. Smith na tumejadili na kudhamiria kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji, elimu, uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na vijana 

Tanzania na Jamaica tumedhamiria kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora ya kufungua fursa mpya kwa maslahi ya mataifa yote mawili,” alisema Balozi Mulamula 

Nae Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina Smith amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Jamaica ambapo uhusiano huo umekuwa ni chachu ya maendeleo inayopelekea kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji na elimu.

“Ushirikiano uliopo baina ya mataifa yetu mawili umekuwa chachu ya maendeleo na lengo la ushirikiano huu ni kukuza, kuendeleza na kuimarisha uchumi wetu,” alisema Mhe. Smith

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa.  

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, elimu, pamoja na afya. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



WAZIRI WA ULINZI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA AU KUHUSU MASUALA YA ULINZI NA USALAMA

Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Kisekta wa Mawaziri wenye dhamana ya kusimamia Ulinzi, Amani na Usalama kutoka Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 12 Mei, 2022.

Mkutano huu ambao ni wa kwanza kufanyika ana kwa ana tangu mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19 mwaka 2020, ulitanguliwa na Mkutano wa Wataalam ambao ulifanyika tarehe 09 na 10 Mei, 2022 na kufuatiwa na Mkutano wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi, Amani na Usalama ambacho uliofanyika tarehe 11 Mei,   2022.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unafanyika kwa lengo la kujadili ushirikiano kati ya Umoja wa Afrika, Mashirika ya Kikanda na Nchi Wanachama kuhusu Majeshi ya Akiba ya Afrika. Pia, mkutano utapitia na kupitisha Sera mbili kuhusu umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa ulinzi wa watoto na haki zao wakati wa Operesheni za Kulinda Amani barani Afrika (Child Protection in African Union Peace Support Operations (2021) and Mainstreaming Child Protection in the African Peace and Security Architecture).

Kadhalika, mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Ugaidi na Mabadiliko ya Serikali kinyume cha Katiba ambao umepangwa kufanyika Malabo, Guinea ya Ikweta tarehe 28 Mei, 2022.

Ujumbe wa Mhe. Waziri Tax unamjumuisha pia Mhe. Hamad Masauni (Mb), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro na Maafisa wengine Waandamizi wa Serikali.

Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Kisekta wa Mawaziri wenye dhamana ya kusimamia Ulinzi, Amani na Usalama kutoka Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 12 Mei, 2022. Pichani ni Wajumbe walioshiriki Mkutano huo akiwemo Dkt.Tax

 

Wednesday, May 11, 2022

WADAU WA UTALII WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUTANGAZA UTALII

Na Mwandishi wetu, Dar

Wadau wa Utalii watakiwa kutumia ubunifu zaidi katika kutangaza vivutio vya utalii wa ndani ili kukuza sekta ya utalii na kuongezea pato la taifa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga alipotoa salamu za Wizara katika Kongamano la Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

“Kuna mambo yanayojitokeza katika mazingira ya sasa kwenye sekta ya utalii ambayo ni muhimu sana kuhusisha ubunifu wa teknolojia katika kutangaza vivutio vya utalii,” alisema Balozi Kasiga .

Balozi Kasiga ameeleza kuwa haiwezekani kuendelea kutangaza utalii kwa njia tulizokuwa tunatumia zamani, ndiyo maana wabunifu wa teknolojia wametuonesha mchango wa teknolojia katika kutangaza vivutio vya utalii na sasa tunaona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amejadiliwa sana kutokana na kutangaza uzinduzi wa filamu ya ‘Royal Tour’ ambayo imeelezea kwa undani vivutio vya utalii nchini kwa teknolojia ya juu zaidi.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mindi amewasihi wabunifu kuendelea kutumia teknolojia kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini. 

Kupitia kongamano hilo washiriki wamejadili namna  ubunifu na teknolojia vinaweza kutumika kama njia mbadala ya kutangaza vivutio vya utalii na kuwavutia watanzania waweze kutembelea vivutio hivyo. 

Aidha, kupitia Kongamano la Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022, teknolojia ya ‘Safari Wallet’ imezinduliwa na kijana wa Kitanzania ambapo inapatikana katika tovuti ya ‘Safari Wallet’ na inatumika kuwasaidia wadau wa utalii kuchagua sehemu za kutembelea kwa urahisi na haraka zaidi vivutio vya utalii nchini

Balozi Kasiga ameeleza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itajitahidi kuiwasilisha teknolojia ya ‘safari wallet’ katika nyanja za kimataifa ikiwemo ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ukanda wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na mataifa mengine ili kuweza kutangaza zaidi vivutio vya utalii nchini.

Naye Naibu Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Job Runhaar amesema teknolojia ni nyenzo muhimu katika kutangaza sekta ya utalii nchini.

Sisi kama wadau wa teknolojia tumefurahishwa sana na uzinduzi wa teknolojia ya Safari Wallet. Teknolojia hii ikitumika vizuri  kutangaza vivutio vya utalii itasaidia  kuchangia ongezeko la mapato ya serikali na maendeleo ya wabunifu kwa ujumla,” amesema Mhe. Runhaar  

Kongamano la ubunifu limeandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) linaloendelea katika wiki ya Ubunifu lililozinduliwa Mei 10, 2022 Jijini Dar es Salaam ambapo wadau wa ubunifu walipata nafasi ya kujadili masuala yanayohusu ubunifu na hatua wanazochukua kuendeleza sekta ya ubunifu ili kuwa na tija kwa Watanzania.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akisalimiana na Naibu Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Job Runhaar katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Job Runhaar akiongea na washiriki wa Kongamano la Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akiongea na washiriki wa Kongamano la Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akiongea na waandishi wa Habari katika Kongamano la Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 


Baadhi ya wanajopo walioshiriki Kongamano la Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 



BALOZI ADELARDUS KILANGI AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA BRAZIL

Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Prof. Adelardus Kilangi akiwasilisha Hati za Utambulisho  kwa  Rais wa Brazil, Mhe. Jair Bolsonaro wakati wa hafla iliyofanyika  hivi karibuni katika Ofisi za Rais za Palacio Do Planalto zilizopo Brasilia, Brazil
Mhe. Rais  Bolsonaro akionesha Hati za Utambulisho za Mhe. Balozi Kilangi mara baada ya kuzipokea wakati wa hafla iliyofanyika  hivi karibuni katika Ofisi za Rais za Palacio Do Planalto zilizopo Brasilia, Brazil
Mhe. Balozi Kilangi akiwa katika mazungumzo na Mhe. Rais Bolsonaro mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho
Mhe. Balozi Kilangi akiwa na Mhe. Rais Bolsonaro 

 

Tuesday, May 10, 2022

BALOZI SOKOINE ATETA NA BALOZI MALAWI, COMORO

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana kwa mazungumzo Balozi wa Malawi nchini, Mhe. Andrew Kumwenda pamoja na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Dkt. Ahamada El Badaoui leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Awali akizungumza na Balozi wa Malawi nchini, Balozi Sokoine amemhakikishia ushirikiano wa Wizara na Serikali kwa ujumla wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.  

Kwa Upande wake Balozi wa Malawi nchini, Mhe. Kumwenda ameishukuru Serikali kwa ushirikano inaompatia tangu alipowasili nchini na ameahidi kuendeleza uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Malawi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Katika tukio jingine, Balozi Sokoine amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Dkt. Ahamada El Badaoui ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Comoro.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Balozi wa Malawi nchini, Mhe. Andrew Kumwenda katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Malawi nchini, Mhe. Andrew Kumwenda yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Dkt. Ahamada El Badaoui leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiagana na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Dkt. Ahamada El Badaoui baada ya kumaliza mazungumzo yao  


TANZANIA YAJIVUNIA USHIRIKIANO IMARA NA UMOJA WA ULAYA

Na Mwandishi wetu, Dar

Serikali imesema inajivunia uhusiano na ushirikiano imara baina yake na Umoja wa Ulaya (EU) ambapo mpaka sasa zaidi ya kampuni 100 za nchi wanachama wa umoja huo zimewekeza Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alitoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Ulaya iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Balozi Mulamula alisema kuwa EU umesimama na Tanzania wakati wote na umeendelea kuunga mkono ajenda ya maendeleo.

“Serikali ya Tanzania inaushukuru Umoja wa Ulaya kwa uhusiano huu imara ambao umedumu kwa muda mrefu pamoja na msaada ambao umekuwa ukitolewa kwa miaka mingi. 

“Umoja wa Ulaya ni wadau wetu wakubwa wa maendeleo, wanagusa kila sekta, mwezi Februari, mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan, alitembelea Umoja wa Ulaya Brussels na alikutana na wafanyabishara, tulipata ahadi ya kampuni nyingi zilionyesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania.” alisema Balozi Mulamula

Alisema kuwa hadi sasa wana kampuni zaidi ya 100 kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya ambazo zimewekeza Tanzania.

Balozi Mulamula aliongeza kuwa wawekezaji wengi kutoka nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya zimeonyesha nia ya kuwekeza hapa nchini na wameridhishwa na mazingira ya biashara yaliyopo.

Nae Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti alisema wataendelea kushirikiana na Tanzania kuimarisha maendeleo katika sekta ya biashara na uwekezaji, utamaduni, uongozi kwa wanawake katika masuala ya siasa, elimu na afya kwa maslahi ya mataifa yote mawili.

“Tunaiona Tanzania ikiendelea kubadilika, mara kwa mara tunakutana na vijana na watu wenye vipaji wakitekeleza malengo na miradi yao, hivyo muundo wa kijamii unabadilika.

“Hii ni dhahiri kabisa kuwa Watanzania ndiyo waamuzi wa mustakabali wa jamii yao, Umoja wa Ulaya utaendelea kuunga mkono jitihada za mabadiliko katika jamii ya Watanzania kwa kuwa huo ndiyo ushirikiano na urafiki,”Balozi Fanti alisema.

Balozi Fanti pia aliipongeza Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuongeza mwanachama mpya ambaye ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa jambo hilo ni jema linaongeza nguvu ya ushirikiano katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Alisema Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kukuza na kuendeleza uchumi wa mataifa hayo kwa maslahi ya pande zote mbili.

Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui ambaye alimuwakilisha Rais wa Umoja wa Ulaya katika maadhimisho hayo, alisema Jumuiya ya Ulaya imelenga pamoja na mambo mengine, kuendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania, kuongeza mshikamano, amani na uhuru pamoja kukuza demokrasia.   

Kwa Upande wake, Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dkt. Peter Mathuki alisema Umoja wa Ulaya umekuwa mshirika mkuu wa nchi wanachama wa EAC kutokana na uhusiano mzuri na wa kishistoria uliojengewa misingi imara tangu 1975.

“EAC tunaishukuru Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa misaada endelevu kwa miradi na programu za Jumuiya yetu ambazo zimekuwa zikiwanufaisha wananchi kwa miaka mingi,” Dk. Mathuki alisema.

Pia alizipongeza nchi wanachama wa Jumuiya Umoja wa Ulaya kwa umoja ambao umekuwa mfano wa kuigwa wa kiuchumi duniani kote.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti akiwasilisha hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Ulaya yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Mgeni rasmi wamaadhimisho ya Siku ya Umoja wa Ulaya Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha hotuba yake katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui atoa salamu kwa niaba ya Rais wa Umoja wa Ulaya wakati wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Ulaya

Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dkt. Peter Mathuki akizungumza na wageni waalikwa katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Ulaya 

Sehemu ya Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Ulaya

Baadhi ya Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya



UFARANSA YARIDHISHWA NA MAZINGIRA YA BIASHARA, UWEKEZAJI NCHINI

Na Mwandishi wetu, Dar 

Ufaransa imeonesha kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Seneta wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya Wafaransa waishio Nje ya Ufaransa, Mhe. Olivier Cadic wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Seneta, Cadic amesema kuwa kwa sasa mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini Tanzania yameboreshwa sana na yanashawishi wafanyabiashara wengi kuja kufanya biashara nchini.

“Tumepata wasaa mzuri wa kujadili fursa za biashara na uwekezaji ambazo zinapatikana nchini Tanzania ambapo wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa wanaweza kuja kuwekeza……kwangu mimi imekuwa fursa ya kuona mazingira haya ya uwekezaji ambayo yanapatikana hapa Tanzania,” 

“Serikali ya Tanzania imejiwekea mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji kwa sasa, haya ni mabadiliko makubwa ambayo yataendeleza urafiki wa Tanzania na mataifa mbalimbali ikiwemo Ufaransa. Kwangu mimi imekuwa fursa kubwa ya kujionea mazingira haya mazuri ya biashara na nitawaelezea wafanyabioashara na wawekezaji kutoka Ufaransa kuja kuwekeza hapa,” amesema Seneta Cadic 

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa ziara ya Seneta Olivier Cadic hapa nchini ni matunda ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Ufaransa hivyo Seneta Olivier amekuja nchini kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuhamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa kuja kuwekeza Tanzania katika sekta za Uchukuzi, Nishati, Utalii, Elimu na Kilimo.

“Seneta amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha zaidi na kuendeleza mazingira bora ya biashara nchini,” amesema Balozi Mulamula

Balozi Mulamula pamoja na mambo mengine, amemhakikishia Seneta Cadic kuwa Serikali bado inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vilivyokuwa vinahatarisha ukuaji wa biashara kati ya Tanzania na mataifa mengine.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Seneta wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya Wafaransa waishio Nje ya Ufaransa, Mhe. Olivier Cadic katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Seneta wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya Wafaransa waishio Nje ya Ufaransa, Mhe. Olivier Cadic akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Seneta wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya Wafaransa waishio Nje ya Ufaransa, Mhe. Olivier Cadic yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiagana na Seneta wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya Wafaransa waishio Nje ya Ufaransa, Mhe. Olivier Cadic yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Monday, May 9, 2022

BALOZI WA TANZANIA NCHINI ETHIOPIA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO UNECA

Mhe. Innocent Eugene Shiyo, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Kamisheni Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA) amewasilisha Hati  za Utambulisho kwa Mhe.Dkt. Vera Songwe, Katibu Mtendaji wa Kamisheni Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA).

Wakati wa hafla hiyo, Mhe. Dkt. Vera Songwe alimpongeza Balozi Shiyo kwa kuteuliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA) yenye Makao Makuu Jijini Addis Ababa, Ethiopia na amemkaribisha na kumtakia heri katika utekelezaji wa majukumu yake.

Wakati wa mazungumzo yao, Balozi Shiyo na Dkt. Vera Songwe wamekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na UNECA katika masuala ya kipaumbele ikiwemo utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, Mpango wa Maendeleo wa Afrika wa Agenda 2063 na juhudi za kukwamua uchumi dhidi ya madhara ya UVIKO-19.

Dkt, Vera Songwe ameeleza utayari wa UNECA kuisadia Tanzania kujenga na kuimarisha uwezo katika mikakati ya kukuza sekta za utalii,afya, kilimo,sekta binafsi, ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA), mapambano dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi na uwezeshaji Wanawake kwenye matumizi ya Teknolojia.

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika ilianzishwa mwaka 1958 kwa ajili ya kukuza maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii katika nchi za Afrika, kukuza Mtangamano wa Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.

 Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Kamisheni Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika, Mhe. Innocent Eugene Shiyo akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA), Mhe. Dkt. Vera Songwe. 

Mhe. Balozi Shiyo akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Songwe mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho

Friday, May 6, 2022

VACANCY ANNOUNCEMENT










 

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA SERIKALI YA CZECH


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Joseph Sokoine akipokea ujumbe kutoka kwa Mjumbe Maalum wa Serikali ya Jamhuri ya Czech Balozi Miloslav Machalek alipokutana naye katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 06 Mei, 2022. 

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Joseph Sokoine akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Martin Klepetko (katikati) walipokutana katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 06 Mei, 2022 wakati Mjumbe Maalum wa Serikali ya Jamhuri ya Czech Balozi Miloslav Machalek (kushoto) alipowasilisha ujumbe wake kwa Katibu Mkuu.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Martin Klepetko walipokutana katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 06 Mei, 2022.  

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Martin Klepetko (katikati) walipokutana katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 06 Mei, 2022. Pembeni ya Balozi Sokoine ni  Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme akiwa na afisa dawati Bi Agness Kiama.


 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Serikali ya Jamhuri ya Czech Balozi Miloslav Machalek katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Mjumbe huyo maalum wa Serikali ya Czech Balozi Machalek amewasilisha andiko la Serikali ya nchi hiyo la kutaka kushirikiana na Tanzania katika maeneo ya usimamizi wa maji, kilimo,  afya, ICT na biashara.

Akizungumza katika kikao hicho Balozi Sokoine ameongelea kufurahishwa na wazo la kuihusisha Tanzania katika mradi huo ambao alisema kuwa utaimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Czech.  

Balozi Machalek amesema andiko aliloliwaasilisha katika kikao hiko ni mradi wa maendeleo ambao nchi yake unakusudia kuutekeleza katika nchi tano za Afrika za Tanzania, Tunisia, Kenya, Ghana na Ivory Coast.

Balozi Machalek aliambatana na Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania  mwenye makazi yake nchini Kenya  Mhe. Martin Klepetko ambaye pia alitumia fursa hiyo kuzungumza na Balzoi Sokoine katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Czech.

Naye Balozi  wa Jamhuri ya Czech ameelezea nia ya Serikali ya Czech kushirikiana zaidi na Tanzania kupitia Nyanja za biashara na uwekezaji ili kukuza ushusiano na ushirikiano kwa faida  ya pande zote mbili na kuongeza kuwa ni matumaini yake kuwa uhusiano mzuri ulipo baina ya nchi hizo utaendelea kuimarika.