Friday, May 6, 2016
Thursday, May 5, 2016
Wizara ya Mambo ya Nje yafanya Mkutano na Vyombo vya Habari
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bi. Mindi Kasiga, akiongea na waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, ambapo alizungumzia Mkutano wa Tume ya pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda uliofanyika nchini Rwanda pamoja tarehe 28 hadi 1 Mei, 2016 na Kikao cha Serikali ya Tanzania na Zambia kilichojadili utatuzi wa changamoto za mipaka kilichofanyika tarehe 27 Aprili, 2016.
Mkurugenzi wa Masomo katika Chuo cha Diplomasia, Dkt. Watengele Kitojo (kushoto) akiwa na Maafisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na Taasisi zake wakati wa Mkutano kati ya Wizara na Waandishi wa Habari.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Msemaji wa Wizara.
Wakati Mkutano ukiendelea.
================================================
================================================
Kikao cha Kumi na Nne
cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Jamhuri ya Rwanda, 29 Aprili – 1 Mei, 2016
Kikao
cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilifanyika
kuanzia tarehe 29 Aprili hadi Aprili, 2016, Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam
wa sekta mbalimbali waliazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi
hizi mbili.
Kikao
hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania
na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda
mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Wakati
wa ziara hiyo, wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano
ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi
baina ya nchi hizo mbili.
Wakati
wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi
Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania
aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa
kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za
ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya
mindombinu ya kikanda kuimarika.
Kwa
upande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo
yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili
kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka.
Pamoja
na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika
sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushoroba wa kati (central corridor),
kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (standard
gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya
ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na
teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.
Mkutano
huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji (Joint
Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya
ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo
itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili,
itakutana kila robo mwaka.
Aidha,
Serikali ya Rwanda imeonesha utayari wake wa kuleta nchini Maafisa na Watumishi
wa Serikali kwa lengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu
nchini kama vile Chuo cha Diplomasia
(CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).
Kwa
upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya
elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa
mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.
Mkutano
ujao wa kumi na tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya
Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.
WAKATI HUO HUO, Kikao cha pamoja cha
Makatibu Wakuu kati ya Tanzania na Zambia kwa ajili ya kujadili utatuzi wa
changamoto za mpaka wa Nakonde Tunduma kilifanyika Lusaka Zambia 25 hadi 27
Aprili, 2016.
Ujumbe
wa Tanzania katika Mkutano huo
uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius
Likwelile na kwa upande wa Zambia uliongozwa na Bw. Bright Nundwe, Katibu Mkuu
wa Jimbo la Muchinga.
Miongoni
mwa changamoto zilizojadiliwa na ufumbuzi wake wakati wa mkutano huo ni pamoja
na:- Msongamano wa magari ambapo kwa
upande wa Zambia huduma kwa
magari ya mizigo zinafanyika hadi saa nne usiku na kwa magari ya abiria
huduma inatolewa kwa masaa 24. Ili kupunguza msongamano, Tanzania imeiomba
Zambia kutoa huduma kwa magari ya aina zote kama Tanzania inavyotoa huduma ya
masaa 24; na Kuimarisha usalama mpakani ili kukabiliana na biashara haramu za
kubadilisha fedha, biashara za magendo na biashara haramu za binadamu.
Mwisho,
pande zote mbili zilikubaliana suala hilo lishughulikiwe kwa kufanya ukaguzi na
ulinzi wa pamoja na kubadilishana taarifa za kiusalama.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa,
05
Mei, 2016
Mhe. Kikwete asaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi wa Kenya
Mama Salama Kikwete naye akisaini Kitabu cha Maombolezo |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Aziz Mlima naye akisaini kitabu cha maombolezo. |
Dkt. Kikwete akiagana na Naibu Balozi, Mhe. Muhia |
Picha na Reginald Philip
Wednesday, May 4, 2016
Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait awasilisha Hati za Utambulisho
Tuesday, May 3, 2016
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati akutana na Balozi wa Palestina
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Abdalah Kilima akimkaribisha Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hazem Shabat alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo katika ofisi za Wizara.
Mabalozi walizungumza juu ya kudumisha na kuimarisha mahusiano na ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Mamlaka ya Palestina.
Saturday, April 30, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: TUME YA KUDUMU YA PAMOJA YA USHIRIKIANO TANZANIA-RWANDA
Kikao
cha Kumi na Nne cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda, 29 Aprili – 1 Mei, 2016
Gisenyi
RWANDA
Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu
ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30
Aprili, 2016, kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam wa sekta
mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi
mbili.
Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano
kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka
huu.
Wakati wa ziara hiyo, wakuu hao
walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua
maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha
wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande
zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi
hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za
wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika.
Kwa upande wake, Balozi Jeanine
Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda na mwenyeji wa kikao
hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo
kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo
ya haraka.
Pamoja na mambo mengine, pande
zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile
miundombinu ya ushoroba wa kati (central corridor), kuharakisha ujenzi wa reli
ya kati katika kiwango cha kimataifa (standard gauge), kukuza ushirikiano
katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL,
kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na
ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.
Mkutano huo pia umekubaliana
kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa
ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika
Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za
Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.
Aidha, Serikali ya Rwanda imeonesha
utayari wake wa kuleta nchini Maafisa na Watumishi wa Serikali kwa lengo la
kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha
Diplomasia (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii
na Wanyamapori (Mweka) na Chuo cha
Usafirishaji (NIT).
Kwa upande wa Tanzania, Serikali
imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la
kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya
tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.
Mkutano ujao wa kumi na tano wa
Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika
mwaka 2018, nchini Tanzania.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Gisenyi, Rwanda
30 Aprili, 2016
Friday, April 29, 2016
Ufunguzi wa Kikao cha 14 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania |
Thursday, April 28, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao cha Mwaka cha Menejimenti ya Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika cha UNICEF jijini Dar es Salaam (25 – 29 Aprili 2016)
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amelihakikishia Shirika La Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (The United Nations Children's Emergency Fund-UNICEF) kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na shirika hilo katika harakati zake za kuboresha ustawi, kutetea na kulinda haki za watoto duniani.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika cha Shirika hilo kilichoanza tarehe 25 Aprili na kinahitimishwa leo kwenye Hoteli ya Ramada.
Dkt. Mahiga alisema kuwa UNICEF ni shirika kubwa linalojulikana duniani kwa mchango wake katika ustawi wa nchi zinazoendelea, hususan katika kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao za kimsingi.
Waziri Mahiga aliendelea kueleza kuwa katika kuhakikisha kuwa watoto wanapatiwa haki zao ipasavyo, hakuna budi UNICEF ikashirikiana na Serikali husika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazorudisha nyuma harakati hizo. Alizitaja changamoto kubwa kwa ustawi wa watoto ni pamoja na sera, mifumo ya kisheria, ufinyu wa bajeti na urasimu katika taasisi za Serikali. “Tunakabiliwa na changamoto nyingi katika harakati za kuimarisha ustawi, kutetea na kulinda haki za watoto ambazo ili ziweze kutatuliwa kwa wepesi lazima Serikali, UNICEF na wadau wengine tufanye kazi kwa pamoja”.
Waziri wa Mambo ya Nje aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kuna masuala mengi yanayosababisha matatizo kwa watoto duniani ambayo yanatakiwa yatafutiwe ufumbuzi kwa pamoja. Masuala hayo ni pamoja na usafirishaji haramu wa watoto, biashara haramu ya dawa za kulevya, unyanyasaji dhidi ya wanawake, machafuko ya kisiasa, kushindwa kuwawezesha wanawake na kuwahudumia watoto. Alisema hayo na masuala mengine yanasababisha changamoto kubwa kwa watoto.
Aidha, Dkt. Mahiga alizungumzia changamoto zinazowakabili watoto wa Tanzania ambazo ni pamoja na mauaji ya watoto, hususan wenye ualbino, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, kuongezeka kwa haraka kwa idadi ya watoto ambako kunasababisha ukosefu wa ajira, ukatili dhidi ya watoto na ukandamizaji wa haki nyingine za watoto.
Alishauri UNICEF iwe na mikakati mahsusi ya kushughulikia changamoto zinazoikabili nchi husika kwa kushirikiana na taasisi za nchi hiyo. Kwa upande wa Tanzania, alisema kuwa inakabiliwa na changamoto ya mauaji ya watu wenye ualbino na kuongezeka kwa mahitaji katika sekta ya elimu ili kuboresha ubora wa elimu, kufuatia kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi kwa sababu ya Serikali ya awamu ya tano kutangaza elimu ya awali hadi ya sekondari bure.
Dkt. Mahiga alihitimisha hotuba yake kwa kueleza kuwa jambo kubwa linalomsumbua ni kuhakikisha kuwa watoto katika kipindi cha ujauzito hadi miaka mitano wanaishi bila kupoteza maisha kutokana na magonjwa na ukosefu wa lishe bora pamoja na kuwalinda hususan katika maeneo ya machafuko.
Ziara ya Waziri wa Nchi wa Viwanda na Biashara wa Singapore, Mhe Dkt. Koh Poh Kun nchini Tanzania tarehe 27 Aprili 2016.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi wa Viwanda na Biashara wa Singapore Mhe Dkt. Koh Poh Kun amefanya ziara ya kikazi nchini tarehe 27 Aprili 2016. Pamoja na mambo mengine, Dkt. Koh amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) mjini Dodoma. Katika mazungumzo yao, Dkt. Koh amemhakikishia Mhe. Waziri Mkuu kwamba makampuni ya Singapore yataendelea kufanya uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini. Hadi hivi sasa Makampuni ya Singapore yaliyokwishawekeza nchini ni pamoja na Pavillion Energy ambayo imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 1.2 katika sekta ya gesi na inatarajia kuwekeza zaidi dola za kimarekani Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa kinu cha kuchakata gesi (LNG plant) kitakachojengwa kwa ubia na makampuni ya gesi kutoka Ulaya na Marekani. Aidha, kampuni ya PIL ya Singapore inatarajia kuwekeza Dola za Kimarekani Milioni 400 kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kutoa huduma kwa makampuni ya gesi. Dkt. Koh pia alimfahamisha Mhe. Waziri Mkuu kwamba kampuni ya Hyflux ya Singapore imeanza kuwekeza nchini kwa kujenga eneo maalum la uchumi (Special Economic Zone) mkoani Morogoro ambapo ndani ya kipindi cha miaka mitano wanatarajia kujenga miundombinu wezeshi ya kuweka viwanda vya kati (light industries), maeneo ya biashara na nyumba za makazi zipatazo 37,000. Jiwe la Msingi la Mradi huo litawekwa tarehe 29 Aprili 2016 na Waziri wa Biashara,Viwanda na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage (Mb).
Mbali na ushirikiano katika sekta ya Biashara na Uwekezaji, Dkt. Koh amemfahamisha Mhe Waziri Mkuu kwamba nchi yake itaisaidia Tanzania kujenga uwezo wa kiufundi katika maeneo mbalimbali ya menejimenti na uendeshaji wa bandari na ufundi katika sekta ya gesi na mafuta. Alisema Singapore ipo tayari kutoa fursa kwa wataalam wa Tanzania kwenda kufanya kazi katika Bandari ya Singapore ili kupata uzoefu utakaosaidia uendeshaji wa bandari za Tanzania. Vilevile, Singapore imeahidi kuandaa mafunzo mahususi kwa ajili ya Makatibu Wakuu wa Tanzania. Mafunzo hayo ya wiki moja yatatumika kubadilishana uzoefu na makatibu wakuu wa Singapore pamoja na Mawaziri. Dkt. Koh alisema Serikali ya Singapore inatoa kipaumbele cha juu katika kuwajengea ujuzi watumishi wa umma kwasababu msingi wa mafanikio ya Taifa lao ni kuwa na rasilimali watu walio na weledi,ujuzi,uzoefu na uadilifu.
Kwa upande wake, Mhe Waziri Mkuu aliishukuru Serikali ya Singapore kwa uwekezaji unaofanywa na makampuni yake nchini na kwa misaada ya kiufundi ambayo wameitoa kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali.
Ili kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kukuza uchumi, Mhe Waziri Mkuu ameyakaribisha makampuni mengine ya Singapore kuja nchini kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda, hoteli, kilimo na nishati. Aidha, alimuahidi Dkt. Koh kwamba Tanzania ipo tayari kukamilisha mazungumzo ya kusaini Mkataba wa Kuvutia na kulinda uwekezaji baina ya nchi hizi mbili (Bilateral Investment Protection and Promotion Agreement) na Mkataba wa Kuepuka kutoza ushuru mara mbili (Avoidance of Double Taxation Agreement) ili kuvutia uwekezaji zaidi kati ya mataifa hayo mawili.
Kuhusu fursa za mafunzo, Mhe Waziri Mkuu ameiomba Serikali ya Singapore itoe fursa zaidi katika mafunzo ya wataalam wa sekta za gesi na uchukuzi.
Awali, Dkt. Koh alifanya mazungumzo na: Mwenyeji wake Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb), Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa (Mb), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb).
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam, 28 Aprili, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)