Thursday, June 20, 2024

RAIS WA GUINEA BISSAU KUFANYA ZIARA RASMI NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akitangaza rasmi ziara ya Rais wa Guinea Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embaro itakayofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Juni 2024. Ziara hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Guinea Bissau. Balozi Shelukindo ametangaza ziara wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofamyika jijini Dar es Salaam tarehe 20 Juni 2024

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ali Sakila (kulia) akifuatilia Mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Shelukindo (hayupo pichani) na Wandishi wa Habari akitangaza kuhusu ziara ya Rais wa Guinea Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embalo itakayofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Juni 2024

Mkutano ukiendelea


 

Wednesday, June 19, 2024

WIZARA YA MAMBO YA NJE NI KATI YA WIZARA 14 NA TAASISI 60 ZINAZOSHIRIKI MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kujenga Kituo cha Kimataifa cha Mikutano jijini Dodoma kufuatia jiji hilo kukua kwa kasi na Serikali kujenga miundombinu ya kisasa, yenye ubora wa hali ya juu.

Ushauri huo umetolewa leo Juni 19, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) alipotembelea Banda la Wizara katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Akitoa taarifa kuhusu ushiriki wa Wizara katika Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Noel Kaganda alimwambia Mhe. Waziri Simbachawene kuwa Wizara kwa sasa, kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) inaendelea na mchakato wa kujenga Kituo kipya cha Mikutano jijini Arusha ambacho kinatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa APIMONDIA Unaohusu ufugaji wa nyuki unaotarajiwa kufanyika Arusha mwaka 2027 na utahusisha wadau zaidi ya 6000.

 

Waziri Simbachawene ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo alitoa wito kwa watumishi na wananchi kwa ujumla kuwa na mwamko wa kutumia mifumo ya TEHAMA inayoanzishwa na taasisi za umma kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma na kuondoa ukiritimba na urasimu.

 

“Taasisi za umma takribani zote nchini zina mifumo ya TEHAMA ya kutoa huduma lakini mwamko kwa wananchi bado sio mzuri wa kutumia mifumo hiyo ambayo lengo lake ni kuharakisha huduma na kuwaondolea usumbufu wananchi” Waziri Simbachawene alisema.

 

Waziri Simbachawene alihitimisha hotuba yake kwa kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ambayo yatafungwa tarehe 23 Juni 2024 ili waweze kupata huduma za papo kwa papo na taasisi zinazoshiriki ikiwa ni pamoja na kupata hati za viwanja, vitambulisho vya taifa na kupima afya.

 

Wizara na taasisi zake za AICC, Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim na Mpango wa Afrika Kujitathimini Kiutawala Bora (APRM-Tanzania) ni kati ya Wizara 14 na taasisi 60 zinazoshiriki maonesho hayo. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda (kushoto) alipowasili kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili kwenye Banda la Wizara lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda alipowasili kwenye Banda la Wizara lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akipokea zawadi ya Diary na Calendar kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi zake wakijibu maswali ya mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijibu maswali ya mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda akipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara alipowasili kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Afisa kutoka Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Nyanzobe Hemed akihudumia wananchi waliojitokeza katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma


 

Tuesday, June 18, 2024

TANZANIA YAZINDUA MKAKATI WA KUJENGA MAJENGO YA BALOZI ZAKE NA VITEGA UCHUMI KUONGEZA MAPATO NCHINI


Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Musalia Mudavadi kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu), Mhe. Deo Ndejembi, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa  na wajumbe wengine wakizindua rasmi ujenzi wa Majengo Pacha ya ghorofa 22 kila moja yatakayojengwa jijini Nairobi, Kenya na kutumika kama Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo na Kitega uchumi kwa ajili ya kuongeza mapato na fedha za kigeni nchini.
Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Musalia Mudavadi akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Majengo Pacha ya ghorofa 22 kila moja yatakayojengwa jijini Nairobi, Kenya na kutumika kama Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo na Kitega uchumi kwa ajili ya kuongeza mapato na fedha za kigeni nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Majengo Pacha ya ghorofa 22 kila moja yatakayojengwa jijini Nairobi, Kenya na kutumika kama Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo na Kitega uchumi kwa ajili ya kuongeza mapato na fedha za kigeni nchini.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Bernard Kibesse akizungumza wakati wa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Majengo Pacha ya ghorofa 22 kila moja yatakayojengwa jijini Nairobi, Kenya na kutumika kama Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo na Kitega uchumi kwa ajili ya kuongeza mapato na fedha za kigeni nchini.
Mhe. Makamba akiteta jambo na Mhe. Mudavadi wakati wa hafla ya wakati wa uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Majengo Pacha ya ghorofa 22 kila moja yatakayojengwa jijini Nairobi, Kenya na kutumika kama Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo na Kitega uchumi kwa ajili ya kuongeza mapato na fedha za kigeni nchini.

Mhe. Mudavadi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Vita Kawawa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Majengo Pacha ya ghorofa 22 kila moja yatakayojengwa jijini Nairobi, Kenya na kutumika kama Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo na Kitega uchumi kwa ajili ya kuongeza mapato na fedha za kigeni nchini.Wengine wanaoshuhudia ni Wajumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Fatma Toufiq (kushoto kwa Mhe. Kawawa) na Mhe. Felista Njau (kulia kwa Mhe. Kawawa).

Viongozi kutoka Kenya na Tanzania pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Majengo Pacha ya ghorofa 22 kila moja yatakayojengwa jijini Nairobi, Kenya na kutumika kama Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo na Kitega uchumi kwa ajili ya kuongeza mapato na fedha za kigeni nchini. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga

WAATALAM WA SEKTA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, UTAMADUNI NA MICHEZO KUTOKA NCHI ZA EAC WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

Wataalam wa Sekta wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekutana leo tarehe 18 Juni 2024 jijini Dar es Salaam katika kikao cha maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Juni, 2024.

Mkutano wa ngazi ya wataalam ambao utafuatiwa na ule wa Makatibu Wakuu, pamoja na masuala mengine, unapitia na kujadili utekelezaji wa maagizo ya mikutano iliyopita, na hatua za utekelezaji wa miradi na programu za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo. 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Ngazi ya Wataalam umeongozwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Abdillah Mataka ambaye ameambatana na Wataalamu Waandamizi kutoka sekta ya  Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo.

 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Abdillah Mataka akizungumza katika Mkutano Ngazi wa Wataalam unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.


Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Irene Isaka (kati) akitoa hotuba ya ufunguzi katika Mkutano Ngazi ya Wataalam unaofanyika tarehe 18 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam

Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Tanzania



Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Uganda

Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Kenya

Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Tanzania

Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Tanzania

Kikao kikiendelea

Picha ya pamoja

 

Sunday, June 16, 2024

DKT. MPANGO AMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MAZISHI YA KITAIFA YA MAKAMU WA RAIS WA MALAWI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi, Hayati Dkt. Saulos Klaus Chilima. Ibada ya Mazishi hayo imefanyika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi leo Jumapili tarehe 16 Juni 2024.

Akitoa salamu za rambirambi, Dkt. Mpango amesema Tanzania inatoa salamu za pole na kuungana na waombolezaji wote walioguswa na musiba katika kipindi hiki kigumu.

Dkt. Mpango amesema Hayati Dkt. Chilima alikuwa kiongozi imara, mwanamajumui wa kweli wa Afrika ambaye wakati wote alitanguliza mbele masilahi ya wananchi anaowaongoza na Afrika kwa ujumla.

Ametoa wito kwa wananchi wa Malawi na Afrika kwa ujumla kuenzi mambo ambayo Hayati Dkt. Chilima aliyaamini na kiyasimamia. 

Katika safari hiyo Dkt. Mpango ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb.), pamoja na Balozi wa Tanzania, Mhe. Agnes Richard Kayola.

Hayati Dkt. Chilima alifariki dunia katika ajali ya ndege na watu wengine nane iliyotokea tarehe 10 Juni 2024 kutokana na hali mbaya ya hewa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akitoa heshima kwenye jeneza la mwili wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi, Hayati Dkt. Saulos Klaus Chilima, katika Ibada ya Mazishi iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu jijini Lilongwe, Malawi tarehe 16 Juni 2024.








Saturday, June 15, 2024

NAIBU KATIBU MKUU MAMBIO YA NJE ATOA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU DKT. SHOGO


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameungana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kutoa salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa familia ya Marehemu Dkt. Shogo Mlozi  tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa familia ya Marehemu Dkt. Shogo Mlozi  tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.

Balozi Mussa na Mhe. Kawawa wakimfariji Prof. Eliamani Sedoyoka ambaye ni mume wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi.

Balozi Mussa na Mhe. Kawawa wakitoa faraja kwa wazazi wa marehemu.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipoungana na waombolezaji wengine katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.