Mkutano wa ngazi ya wataalam ambao utafuatiwa na ule wa Makatibu Wakuu, pamoja na masuala mengine, unapitia na kujadili utekelezaji wa maagizo ya mikutano iliyopita, na hatua za utekelezaji wa miradi na programu za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Ngazi ya Wataalam umeongozwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Abdillah Mataka ambaye ameambatana na Wataalamu Waandamizi kutoka sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Abdillah Mataka akizungumza katika Mkutano Ngazi wa Wataalam unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024. |
Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Tanzania |
Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Uganda |
Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Kenya |
Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Tanzania |
Sehemu nyingine ya Ujumbe kutoka Tanzania |
Kikao kikiendelea |
Picha ya pamoja |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.