Monday, June 24, 2024

MAANDALIZI YA MKUTANO WA 45 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC YAENDELEA JIJINI ARUSHA

 

Maandalizi ya Mkutano wa Kawaida wa 45 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yanaendelea jijini Arusha katika kikao ngazi ya Maafisa Waandamizi.

 

Mkutano huo wa Mawaziri utafanyika tarehe 28 Juni, 2024 na unatanguliwa na vikao vya awali vya maandalizi ambavyo ni; Kikao cha Maafisa Waandamizi kilichoanza tarehe 22 Juni 2024 na kitahitimishwa leo tarehe 24 Juni, 2024 na Kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 25 hadi 27 Juni 2024.

 

Pamoja na masuala mengine mkutano huo utapitia na kujadili taarifa mbalimbali kama ifuatavyo,  taarifa ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na baraza hilo kwenye vikao vilivyopita, taarifa kuhusu masuala ya forodha na biashara na taarifa ya miundombinu, sekta za uzalishaji, sekta za jamii na masuala ya kisiasa.

 

Taarifa nyingine ni, taarifa ya kamati na fedha na rasilimali watu, taarifa ya mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 17 Mei, 2024 pamoja na taarifa ya kalenda ya matukio ya jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba, 2024.

 

Mkutano huu unahudhuriwa na nchi zote wanachama ikiwemo, Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania akiwa mwenyeji, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Somalia imeshiriki kwa njia ya mtandao.

 

=============================

Meza kuu; Kushoto ni Mwenyekiti wa kikao cha Maafisa Waandamizi, Bw. Eulwango Ugo kutoka Jamhuri ya Sudan Kusini akiongoza kikao cha Maafisa Waandamizi na pembeni ni Mkuu wa masuala ya Sheria kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika mashariki(EAC), Dkt. Anthony Kafumbe.

Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Abdillah Mataka na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilson Gwoma wakifuatilia majadiliano.

Maafisa kutoka Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha Maafisa Waandamizi wa EAC, kutoka kulia ni Dkt. Elias Bagumhe na Bw. Othman Chanzi.

 Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Jasinta Mboneka na Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Abel Maganya wakifuatilia majadiliano.

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ukifuatilia majadiliano.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kenya.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Rwanda.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Burundi.

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Uganda.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.