Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amesema
maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe 23 Juni kila
mwaka yanalenga kuhamasisha uwajibikaji, uwazi na ufanisi katika utumishi wa umma
barani Afrika
Waziri Mkuu alisema
hayo wakati wa hafla ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na ufunguzi
wa mifumo ya kielekitroniki ya uwajibikaji katika utumishi wa umma (E-UTUMISHI)
iliyofanyika juni 23, 2024 kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Taasisi za Umma
ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo
ilishiriki maadhimisho hayo zilielekezwa kuhakikisha kuwa zinajiunga kwenye
mifumo hiyo na kuwa na mpango endelevu wa kuwaelimisha watumishi namna ya kuitumia.
Mifumo hiyo ni pamoja
na mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (HCMIS); Mfumo wa Utumishi wa
Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma ((PEPMIS/PIPMIS), Mfumo wa Tathmini ya Rasilimaliwatu
(HRA) na Mfumo wa Kushughulikia Mrejesho
wa Wananchi kuhusu Huduma Zinazotolewa
na Serikali (e-MREJESHO).
Amesema mifumo hiyo
ni muhimu kwa kuwa inarahisisha na kuharikisha huduma kwa wananchi pamoja na kuondoa
kero kama vile za rushwa na urasimu. Waziri Mkuu ametoa wito kwa watumishi wa
umma na wananchi kwa ujumla kuchangamkia mifumo hiyo ambayo imeunganishwa na
taasisi nyingine kama za huduma za kifedha, mifuko ya pensheni na Mamlaka ya
Taifa ya Vitambulisho.
Waziri Mkuu
aliwapongeza wabunifu wa mifumo hiyo ambao wote ni Watanzania kwa kubuni mifumo
yenye tija na ubora mkubwa ambayo imetambuliwa na taasisi ya umoja wa mataifa ya
“United Nations Public Services Awards”.
Waziri Mkuu
alihitimisha hotuba yake kwa kuagiza kila Mkuu wa taasisi aweke mipango ya
usimamizi na uongozi wa mifumo hiyo ili iweze kutumika kwa ufanisi katika ngazi
ya taasisi yake; taasisi za umma zihakikishe usalama wa takwimu na taarifa
zinazowekwa kwenye mifumo hiyo. Alisema mifumo hiyo ina taarifa muhimu na
nyeti, hivyo ni muhimu kuhakikisha taarifa hizo zinalindwa ipasavyo ili kuepuka
uhalifu wa kimtandao pamoja na kutoa mafunzo na kuhamasisha matumizi ya mifumo
hiyo ambayo ni migeni kwa watumishi.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.