Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki-anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi ameongoza kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichofanyika tarehe 25 Juni, 2024 jijini Arusha.
Kikao hicho cha ndani pamoja na masuala mengine kimepitia agenda, taarifa na maagizo mbalimbali yaliyotolewa katika mikutano iliyopita ili kuona hali ya utekelezaji sambamba na kujenga msimamo wa Nchi katika masuala yenye maslahi mapana kwa ustawi wa watanzania na Taifa kwa ujumla.
Mkutano huo wa Makatibu Wakuu wa EAC utafanyika tarehe 26 na 27 Juni, 2024 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 45 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri utakaofanyika tarehe 28 Juni 2024 jijini Arusha.
=================================
|
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika tarehe 25 Juni, 2024 jijini Arusha. |
|
Naibu
Katibu Mkuu, Afisi ya Rais - Kazi, Uchumi na Uwekezaji (Uchumi na Uwekezaji)
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na
Biashara, Balozi Dkt. John Simbachawene wakifatilia kikao cha ndani wa ujumbe
wa Tanzania kilichofanyika tarehe 25 Juni, 2024 jijini Arusha. |
|
Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Bw. Cyrus Kapinga akifatilia kikao. |
|
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii, Mhandisi
Abdillah Mataka akiwasilisha taarifa ya mkutano wa Maafisa Waandamizi uliomalizika
leo tarehe 25 Juni, 2024. ======================= Maafisa waandamizi wakifatilia kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa Makatibu Wakuu kiliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni, 2024. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.