Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeshauriwa kuangalia
uwezekano wa kujenga Kituo cha Kimataifa cha Mikutano jijini Dodoma kufuatia jiji
hilo kukua kwa kasi na Serikali kujenga miundombinu ya kisasa, yenye ubora wa
hali ya juu.
Ushauri
huo umetolewa leo Juni 19, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb)
alipotembelea Banda la Wizara katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Akitoa taarifa kuhusu ushiriki wa
Wizara katika Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Noel Kaganda alimwambia Mhe. Waziri Simbachawene kuwa Wizara kwa sasa, kwa kushirikiana
na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) inaendelea na mchakato wa
kujenga Kituo kipya cha Mikutano jijini Arusha ambacho kinatarajiwa kuwa
mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa APIMONDIA Unaohusu ufugaji wa nyuki unaotarajiwa
kufanyika Arusha mwaka 2027 na utahusisha wadau zaidi ya 6000.
Waziri Simbachawene ambaye alikuwa
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo alitoa wito kwa watumishi na wananchi
kwa ujumla kuwa na mwamko wa kutumia mifumo ya TEHAMA inayoanzishwa na taasisi
za umma kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma na kuondoa ukiritimba na urasimu.
“Taasisi za umma takribani zote nchini
zina mifumo ya TEHAMA ya kutoa huduma lakini mwamko kwa wananchi bado sio mzuri
wa kutumia mifumo hiyo ambayo lengo lake ni kuharakisha huduma na kuwaondolea
usumbufu wananchi” Waziri Simbachawene alisema.
Waziri Simbachawene alihitimisha
hotuba yake kwa kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo
ambayo yatafungwa tarehe 23 Juni 2024 ili waweze kupata huduma za papo kwa papo
na taasisi zinazoshiriki ikiwa ni pamoja na kupata hati za viwanja,
vitambulisho vya taifa na kupima afya.
Wizara na taasisi zake za AICC, Kituo
cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim na Mpango wa Afrika Kujitathimini
Kiutawala Bora (APRM-Tanzania) ni kati ya Wizara 14 na taasisi 60 zinazoshiriki
maonesho hayo.
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda (kushoto) alipowasili kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
|
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili kwenye Banda la Wizara lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma |
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda alipowasili kwenye Banda la Wizara lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma |
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akipokea zawadi ya Diary na Calendar kutoka kwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. |
|
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi zake wakijibu maswali ya mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. |
|
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijibu maswali ya mwananchi aliyotembelea Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. |
|
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda akipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara alipowasili kwenye Banda la Wizara hiyo lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. |
|
Afisa kutoka Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Nyanzobe Hemed akihudumia wananchi waliojitokeza katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
|
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Goerge Simbachawene (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.