Thursday, August 22, 2013

Waziri wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Kenya

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Mutinda Mutiso akitembea sambamba na Bibi Zuhura Bundala. Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wakati alipokuwa anaingia kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro kwa ajili ya hafla ya kumuaga.
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kushoto akisalimiana na Balozi wa Kenya kabla ya kuanza kwa hafla ya kumuaga.
 

Mhe. Waziri akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency.
 

Bibi Bundala akitoa neno kwa ajili ya kumkaribisha Mhe. Waziri kutoa hotuba ya kumuaga Balozi wa Kenya.
 

Mhe. Membe akitoa hotuba ambayo ilisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya Tanzania na Kenya.
 

Balozi wa Kenya anayemaliza muda wake akitoa hotuba ambapo alishukuru kwa ushirikiano aliopata kutoka Serikali ya Tanzania uliomwezesha kutekeleza majukumu yake kwa wepesi.
 

picha ya pamoja
Picha na Reginald Kisaka

Mhe. Membe apokea msaada wa Magari ya kubebea wagonjwa kutoka Korea Kusini

Na Zainabu Abdalah

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Mheshimiwa Bernard Membe. Jana amekabidhiwa msaada wa magari manne ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya wananchi wa Majimbo ya Nchinga na Ruangwa ya mkoani Lindi na Balozi wa Korea nchini, Mhe. Chung Il.

Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwa Balozi huyo Osterbey Dar es Salaam na ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa naTawala za Mikoa (Tamisemi) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Mheshimiwa Kassim Majaaliwa na Mheshimiwa Said Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Lindi.

Magari hayo manne ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa ni kwa ajili ya vituo vinne vya Afya vilivyopo katika Majimbo hayo ambavyo ni Sokoine, Kitomani, Ruangwa na Milola.

Waziri Membe ameishukuru sana Serikali ya Korea Kusini kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika vizuri kama ulivokusudiwa. Aidha, alisema Serikali ya Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Korea Kusini ambao ulianza miaka mingi iliyopita.

 

 

 

Mhe. Membe apokea Magari ya msaada ya kubebea wagonjwa kutoka Korea Kusini


Magari ya wagonjwa yalitolewa na Korea Kusini kwa ajili ya majimbo ya vituo vya afya vinne vya majimbo ya Ruangwa na Nchinga Mkoani Lindi.

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akionyesha funguo ya moja ya magari ya msaada mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Chung IL.
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akipungia mkono watu waliohudhuria hafla ya makabidhiano huku akiendesha moja ya magari ya msaada kutoka Korea Kusini. 
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa pili kutoka kushoto akimpa funguo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa), Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ambaye jimbo lake la Ruangwa limepatiwa magari mawili.
 

Mhe. Kassim Majaliwa akifungua mlango wa  moja ya magari aliyokabidhiwa kwa ajili ya jimbo lake ili alijaribu.
 

Mbunge wa Nchinga, Mhe. Said Mtanda naye akijaribu moja ya magari aliyokabidhiwa kwa ajili ya wananchi wa jimbo lake la Nchinga.
 

Mhe. Membe kushoto akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini kabla ya shughuli ya kukabidhiana magari ya msaada.
 

Mhe. Naibu Waziri wa TAMISEMI wa kwanza kushoto, Mbunge wa Nchinga wa pili kutoka kushoto pamoja na Diwani wa moja ya Kata ya jimbo la Ruangwa wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi wa Korea Kusini. (hawapo pichani)
 

picha ya pamoja
 


Balozi wa Korea Kusini wa kwanza kulia akibadilishana mawazo na Bw. Khatibu Makenga wa kwanza kushoto Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakati wa hafla hiyo.
 
picha na Ally Kondo

Wednesday, August 21, 2013

Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Wapya


Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Ombeni Y. Sefue akijiandaa kuongea na Waandishi wa Habari waliokusanyika jioni hii kupata taarifa kuhusu Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Wapya, katika ofisi za Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu  - jijini Dar es Salaam.   Pembeni kushoto ni Bw. Salvatore Rweyemamu, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. 

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Ombeni Y. Sefue akisoma orodha mpya ya Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu Wapya jioni ya leo hii katika Ofisi ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.  Wapili kulia ni Bw. Salvatore Rweyemamu, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na watatu kulia Bw. Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni. 

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Sefue akiendelea kusoma orodha ya Makatibu Wakuu wapya na wanaohama.  Pembeni kushoto ni Bw. Salvatore Rweyemamu, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. 

 

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Ombeni Y. Sefue akijibu maswali ya waandishi kabla ya kuendelea kusoma orodha ya Uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wapya na uhamisho wa baadhi yao.



Picha zote na Tagie Daisy Mwakawago 



Tuesday, August 20, 2013

Katibu Mtendaji mpya wa SADC apokelewa kwa shangwe Wizara ya Mambo ya Nje


 

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimlaki kwa furaha Katibu Mtendaji mpya wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),  Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax mara baada ya kuwasili Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 

Mhe. Membe akimkabidhi shada la maua Dkt. Tax kwa niaba ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kuwasili Wizarani hapo.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule nae akimkarisha Dkt. Tax kwa furaha Wizarani.
 
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akimpongeza kwa shada la maua Dkt. Tax mara nbaada ya kuwasili Wizarani.
 
Mapokezi yakiendelea.
 
Dkt. Tax akipongezwa na kukaribishwa Wizarani na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha.
 
Balozi mpya  wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz, nae pia aliungana na Wafanyakazi wa Wizara kumpongeza dkt. Tax. Anayeshuhudia pembeni ni Bw. Ali Mwadini, Katibu wa Naibu Waziri. 
 
Dkt. Tax akipongezwa na Bw. Omar Mjenga, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na Australasia huku Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. James Lugaganya (kushoto) akishuhudia.
 
Balozi Bertha Semu-Somi, Mkurugenzi wa Diaspora akimlaki kwa shangwe Dkt. Tax wakati wa mapokezi.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya nae akitoa pongezi zake za dhati kwa Dkt. Tax
 
Maafisa mbalimbali wa Wizara nao pia walikuwa mstari wa mbele kumpongeza Dkt. Tax.
 
Dkt. Tax akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya mapokezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, huku Mhe. Membe akishuhudia.
 

Mhe. Membe akifurahia jambo na Makatibu Wakuu wakati Dkt. Tax akisaini Kitabu cha Wageni.

 
Picha na Reginald Philip.

Kikao cha Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge chafanyika


Mhe. Edward Lowassa (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na Mbunge wa Monduli akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika  Ofisi Ndogo za Bunge tarehe 19 Agosti, 2013.

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwasilisha  Taarifa ya Wizara ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge (hawapo pichani).
Baadhi ya Waheshimiwa wa Wabunge ambao pia  ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).

Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa karibu taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Membe (hayupo pichani).

Kikao kikiendelea.

Monday, August 19, 2013

The 33rd SADC Summit Communique


The outgoing SADC Executive Secretary Dr. Tomaz Augusto Salomão delivering 33rd SADC Summit Communique.  The 33rd Heads of State and Government of the Southern Africa Development Community (SADC) was hosted by H.E. Joyce Banda, President of Malawi and held at the Bingu International Conference Centre in Lilongwe, Malawi.  (Photo by Tagie Daisy Mwakawago)