Monday, September 23, 2013

Mhe. Rais Kikwete ampigia simu Rais Kenyatta kuhusu shambulio la ugaidi Kenya


 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIADIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone:
 
255-22-2114512,2116898
 
E-mail:ikulumawasiliano@yahoo.com  press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425PRESIDENT’S OFFICE,THE STATE HOUSE,P.O. BOX 9120,DAR ES SALAAM.Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIRais Kikwete ampigia simu Rais Kenyatta kuhusushambulio la ugaidi Kenya, asema amekasirishwa nakitendo hicho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezungumza kwa simu na Rais UhuruKenyatta wa Kenya na kumpa pole na kutaka kujua jinsi gani Tanzania inaweza kusaidia kufuatia shambulio la kigaidikwenye KituchBiashara chWestgate katika eneo laWestlands, Nairobi, ambako watu 59 wameuawa na wengine175 wamejeruhiwa.Rais Kikwete alimpigia simu Rais Kenyatta jioni ya jana, Jumamosi, Septemba 21, 2013, kutokea mjini New York,Marekanimara baadya kuwasili mjinhumo akitokea Toronto, Canada, ambako alifanya ziara ya kikazi ya siku tatu.Katika mazungumzo kati ya viongozi hao, Rais Kikweteamemweleza Rais Kenyatta mshtuko na hasira yake kutokanana taarifa za kusikitisha za shambulio hilo la kigaidi lililofanywaasubuhi ya jana hiyo hiyo.Rais Kikwete amefuatilia mazungumzo hayo kwa salamurasmi za rambirambi ambazo Rais Kikwete amemtumia RaisKenyatta akielezea masikitiko na hasira yake kufuatia mauajihayo ya watu wasiokuwa na hatia akitaka kujua jinsi Tanzaniainaweza kusaidia juhudi za Serikali ya Kenya katika kukabilianana madhara ya tukio hilo na balaa la ugaidi kwa jumla.Katiksalamhizzrambirambi, Rais KikweteamemwelezRais Kenyatta:
“Nimekupigia simmapemaleo kuelezea mshtuko na hasira yangu baada ya kusikiahabari za kusitikisha za shambulio la kigaidi lililotokeaasubuhi ya leo, Jumamosi, Septemba 21, 2013, kwenyeKituchBiasharchWestgatkatikenela
 
Westlands na kusababisha vifo vya watu 59 na mamiaya majeruhi.”
 Katika salamu zake hizo za rambirambi RaisKikweteamesema:
KwniabySerikalyJamhuryaMuunganwa Tanzaniankwhakika, kwniabayangu mwenyewe, napenda kutuma salamu za dhati yamoyo wangu kwako wewe, kwa Serikali ya Jamhuri yaKenya na kwa familia zote zilizopotelewa na wapendwawao katika shambulio hili. Sala zetu na pole zetu nyingi  ziko pamoja na wale wote ambao wameathiriwa nashambulio hili la kutisha. Aidha, tunawatakia walioumiakasi ya kupona.”
AmeongezRais Kikwete:
“Shambulio hili linalengakuitisha Serikali nWananchhodari wKenynakudhoofishniyaykutimizwajibwawakihistoria wa kuunga mkono jitihada za kuleta amani katika nchi jirani na yenye matatizo ya Somalia.”“Kwa maana hiyo, shambulio hilo la woga na lisilona huruma kabisa dhidi ya watu wasiokuwa na hatia,lazimlilaaniwna kushutumiwa vikali na wapendaamani wote”
.
Tuna hakika kuwa chini ya uongozi wako imara,Serikali ya Kenya itahakikisha kuwa wote waliohusikakufanya kitendo hiki wanasakwa nakufikishwa mbele yavyombo vysheria kama ambavySerikali imepatakufanyhuknyuma,
RaiKikwete amesisitiznakuongeza:
“Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania wanasimama bega kwa bega na kaka na dada zao wa Kenya katika kipindi hiki kigumu. Aidha, Serikali ya Tanzania inapenda kuihakikishia Serikali ya Kenyaitaendelea kuiunga mkono na kushirikiana nayo katikakupambana na balaa la ugaidi katika sura zake zote.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Septemba, 2013

President Kikwete sends a Condolence Message to President Kenyatta



PRESS RELEASE

H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a Condolence Message to H.E. Uhuru Kenyatta, President of the Republic of Kenya following the devastating news of tragic terrorist attack at the Westgate Shopping Centre in Westlands, Nairobi.

The Message reads as follows:
“H.E. Uhuru Kenyatta,
President of the Republic of Kenya,
NAIROBI.


Your Excellency,

I have received with shock and anger the devastating news of tragic terrorist attack at the Westgate Shopping Centre in Westlands, Nairobi, on 21st September, 2013 and claimed 59 innocent lives, more than 175 injured and many more in traumatic condition.

During this time of grief, I wish, on behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, to convey our deepest condolences to you and through you to the Government and People of the Republic of Kenya as well as bereave families who have been robbed of their loved ones by this heinous attack. I also send our prayer and sympathy for the speed recovery, comfort, courage and consolation of all those affected by this horrendous attack.

This attack not only aimed at bringing fear and hatred among Kenyans, but also to deviate the Government of Kenya from fulfilling its international obligation to support peace processes on the continent. In this respect, this cowardly and senseless attack on innocent people must be condemned by all peace loving people in no an uncertain terms.

We are convinced that under your able leadership, the Government of Kenya will leave no stone unturned and bring the perpetrators to justice as it has been done before. The Government and people of the United Republic of Tanzania stand together with the people of Kenya during this trying moment. My Government pledge our unreserved support to the Kenyan Government in working together to fight the scourge of terrorism in all its forms.

Please accept, Your Excellency the assurances of my highest consideration.


Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA”



Issued by:

The Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation,

Dar es Salaam


22nd September, 2013


Mabalozi wetu wawe chachu ya kuwavuta wawekezaji




Mabalozi wetu wawe chachu ya kuwavuta wawekezaji


NA Maoni ya MHARIRI wa Gazeti la NIPASHE JUMAPILI,
22 Septemba 2013

Moja ya sera na mikakati ya kuinua uchumi wa nchi ni pamoja na kuwahamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje katika miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo itasaidia kuinua pato la taifa.

Ni rahisi zaidi kuwahamasisha wawekezaji wa ndani kwa vile wao nao ni sehemu ya jamii inayopambana na kujikwamua kutoka uchumi uliopo ambao ni tegemezi na unaoonekana kuwa dhaifu.

Kikwazo kinachojitokeza kwenye sera ya uwekezaji ni pamoja na umaskini wa wananchi wengi ambao kimsingi wanakosa mitaji mikubwa ya kuwafanya wawekeze katika sekta zinazohitaji mitaji mikubwa.

Wenye uwezo wa kuwekeza kwa mitaji inayoweza kuzalisha faida kubwa ni wageni wa nchi mbalimbali za duniani, ambako pia kuna wawakilishi wetu ambao ni mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania kwa masuala ya kidiplomasia.

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika ziara ya Marekani jijini Washington mwishoni mwa wiki hii, alisema kazi kubwa ya mabalozi wa Tanzania katika nchi za nje, ni kutetea maslahi na kuijengea marafiki katika nchi na maeneo ambako wanaiwakilisha nchi.

Rais alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila balozi wa Tanzania popote alipo, kuonyesha sura nzuri ya Tanzania, kuvutia wawekezaji katika maeneo mbalimbali na kutangaza nafasi nyingi za uwekezaji nchini.

Tanzania ina utajiri mkubwa wa utalii duniani, na mojawapo ya majukumu ya mabalozi wetu hao ni kutangaza utajiri huo, na hasa Marekani ambayo kwa sasa ndiyo nchi inayoongoza kwa kuleta watalii wengi nchini.

Rais Kikwete alipata fursa ya kuongea na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje, ilikuwa wakati alipozungumza kwenye hafla ya kutiwa saini kwa makubaliano kati ya Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula na mabalozi saba wa heshima ambao wataiwakilisha Tanzania katika maeneo mbalimbali nchini Marekani.

Katika hafla hiyo, Rais Kikwete aliwaasa mabalozi hao wa heshima kuwa wanawajibika kulijenga jina la Tanzania katika maeneo yao, na kuitengenezea nchi yetu marafiki wa kila aina ikiwa ni pamoja na kuwavutia wawekezaji kuja nchini kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.

Watu wenye fedha na rasilimali za kuwekeza wanatakiwa waelimishwe kuwa Tanzania ni nchi nzuri kupeleka mitaji yao na kuwa mitaji hiyo itabakia kuwa salama. Rais aliwasisitizia mabalozi hao wa heshima kuwa pia watangaze utajiri mkubwa wa utalii uliopo nchini.

Tuna imani kubwa kuwa wito alioutoa Rais Kikwete kwa mabalozi wetu utatekelezwa kwa umakini, na pia tuaamini kuwa muda si mrefu Tanzania itanufaika na fedha za kigeni ambazo zitatokana na utalii pamoja na uwekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani.

Wapo wawekezaji wazalendo ambao baadhi wamewekeza katika sekta mbalimbali kama za hoteli za kitalii, mashamba ya mazao ya biashara na chakula, viwanda vidogo vidogo pamoja na katika masuala ya elimu. Bado jitihada zinatakiwa zifanyike ili kutanua wigo wa uwekezaji katika maeneo mengine ya kiuchumi.

Faida kubwa za uwekezaji si kwa ajili ya serikali kuongeza pato peke yake, bali hata ajira kwa vijana huongezeka. Uchumi wa nchi unapokua, unatoa pia fursa nyingi za ajira kwa vijana, na vijana ndiyo nguvu kazi inayotegemewa na nchi.

Mabalozi popote w alipo duniani, wanawajibu kutambua jukumu hili kubwa ambalo ni msingi mkubwa wa kuongeza pato la taifa na kuinua uchumi wa nchi. Wawekezaji wengi walioko nchini wamejikita katika uchimbaji wa madini, na sasa wameanza kuonyesha nia ya kuwekeza katika maliasili nyingine kama gesi asilia na mafuta.

Tunampongeza Rais Kikwete kwa kuwahamasisha mabalozi kuinadi Tanzania katika maeneo ya uwekezaji pamoja na utalii, tunaamini kasi ya kujituma kwa kazi hiyo ikifanyika kwa uadilifu, Tanzania itakuwa moja ya nchi itakayojizolea fedha nyingi za kigeni zitakazosaidia maendeleo ya taifa.


Mhe. Rais aongoza kikao cha maandalizi ya ushiriki wa Tanzania kwenye UNGA



 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete  akiongoza kikao cha kupokea taarifa za maandalizi kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (Mb.) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (Mb.)
 
Mhe. Rais  Kikwete  akizungumza wakati wa kikao hicho huku Mhe. Membe akisikiliza. Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Tuvako Manongi (kulia kwa Mhe. Rais), Mhe. Haroun Suleiman, Waziri wa Kazi, Zanzibar, Mhe. Terezya Huvisa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Annastazia Wambura (Mb. )na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberatta Mulamula.
 
Mhe. Balozi Manongi akitoa taarifa fupi kwa Mhe. Rais Kikwete kuhusu maandalizi ya ushiriki wa Tanzania kwenye kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushierikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara  ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Robert Kahendaguza wakati wa kikao na Mhe. Rais Kikwete.
 
Maafisa wakati wa kikao hicho.
 




Sunday, September 22, 2013

Mhe. Rais Kikwete awasili New York kuhudhuria Kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya JW Marriot ya Jijini New York, Marekani. Mhe. Rais Kikwete na Ujumbe wake yupo nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kinachofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.


Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Mhe. Haroun A. Suleiman

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) naye akiwasili katika Hoteli ya JW Marriot akiwa amefuatana na Balozi Mushy (kulia) pamoja na Msaidizi wake Bw. Togolani Mavura.





 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika Ubalozi wa Tanzania, New York, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Iadara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.






Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Robert Kahendaguza.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  , Bw. Yusuph Tugutu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York waliofika kumpokea Hotelini hapo.
 

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  m Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
 

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Ramla Khamis mmoja wa Maafisa utoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Tully Mwaipopo mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bibi. Ellen Maduhu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bibi Maura Mwingira mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah, Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Daily News

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Anna Nkinda, Afisa Kutoka Idara ya Habari (MAELEZO).
 

Na Rosemary Malale, New York
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini New York, Marekani tarehe 21 Septemba, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (The 68th Session of the United Nations General Assembly (UNGA 68TH) kinachoendela mjini hapa kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.
 
Kikao hicho kimeazimia kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kiusalama, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kaulimbiu ya Mjadala Mkuu (General Debate) ni “Post-2015 Development Agenda: Setting the Stage”. Aidha, Mhe. Rais Kikwete, anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 Septemba, 2013.
 
Pamoja na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kulihutubia Baraza hilo, Mhe. Rais atashiriki mikutano mingine yenye manufaa kwa maendeleo ya Taifa ikiwemo:-  Mkutano wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya Awamu ya Pili baada ya Awamu ya Kwanza kumalizika; Mkutano kuhusu Usalama wa Chakula na Lishe; Mkutano wa Kamati ya Marais wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.
 
Mingine ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu biashara haramu ya Wanyamapori na uvunaji haramu wa Magogo; Mkutano kuhusu maendeleo ya Wanawake na Watoto; Mkutano wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC); na Mkutano kuhusu kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia.
 
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais atapata nafasi ya kukutana na Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama; Waziri Mkuu wa Norway, Mhe. Jes Stoltenberg; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-moon; Mkurugenzi Mtendaji wa MCC, Bw. Daniel Yohannes na Viongozi wa Makampuni mbalimbali.
 
Aidha, pamoja na mikutano ya ngazi ya juu, Kikao cha Baraza Kuu pia hujumuisha mikutano ya Wataalam kupitia Kamati Sita za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kamati inayoshughulikia masuala ya Upokonyaji na Upunguzaji Silaha Duniani; Kamati ya Uchumi na Fedha; Kamati ya Kijamii na Haki za Binadamu; Kamati inayoshughulikia masuala ya Ukombozi Duniani; Kamati ya Bajeti na Utawala; na Kamati ya masuala ya Sheria.
 
Viongozi wengine watakaoambatana na Mhe. Rais Kikwete ni pamoja na Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.); Waziri wa Kazi Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman; Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (Mb.); Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Hussein Mwinyi (Mb); na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhe. Terezya Huvisa (Mb.).
 
Wengine ni Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa (Mb.), Mhe. Anastazia Wambura (Mb); Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango; na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.
 
-Mwisho-