Monday, May 18, 2015

Rais wa Msumbiji atembelea Chuo cha Diplomasia, afungua Kongamano la Uwekezaji na kuzungumza na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini



Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akiwajadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR),  Balozi Mwanaidi Maajar  huku Mkuu wa Chuo hicho Balozi Mohammed Maundi akisiskiliza wakati viongozi hao wakisubiri kumpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi alipotembelea Chuoni hapo leo tarehe 18 Mei, 2015 wakati akiendelea na ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini. Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini, Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 1978 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Maundi alipotembelea Chuoni hapo wakati wa ziara yake hapa nchini
Balozi Maundi akiwatambulisha baadhi ya Wahadhiri wa Chuo hicho kwa Mhe. Rais Nyusi
Juu na Chini:  Mhe. Rais Nyusi akizungumza na Wahadhiri, Wanafunzi na Wageni mbalimbali alipotembelea Chuo cha Diplomasia (CFR)
Wajumbe wakifurahia jambo wakati Rais Nyusi (hayupo pichani) alipozungumza nao 
Mhe. Rais Nyusi akifurahia zawadi ya picha ya kuchora inayowaonesha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel aliyozawadiwa alipotembelea Chuo cha Diplomasia
Rais Nyusi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Msumbiji pamoja na  Uongozi wa Chuo cha Diplomasia. Kushoto ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia (wa kwanza kushoto) ambaye ni Waziri anayeongozana nae kwenye ziara hii.
Mhe. Rais Nyusi akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia
Rais Nyusi akiangalia bango linalosomeka "CHUO HIKI KILIKUWA CHUO CHA ELIMU YA JUU KWA WAPIGANIA UHURU WA AFRIKA" ikiwa ni jina la awali kabla Chuo cha Diplomasia hakijaanzishwa.
Mhe. Rais Nyusi akiangalia Jiwe la Msingi la kuanzishwa kwa Chuo hicho



......Rais Nyusi alipozugumza na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini


Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akifurahia kikundi cha ngoma cha Raia kutoka Msumbiji wanaoishi hapa nchini alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kuzungumza nao.

Sehemu ya umati wa Raia wa Msumbiji wanaoishi hapa nchini wakimpokea kwa shangwe Rais Nyusi alipokutana  na kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini


Mhe. Rais Nyusi akizungumza na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini (hawapo pichani)


Mhe. Rais Nyusi akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa Raia wa Msumbiji wanaoishi hapa nchini



......Rais Nyusi aliposhiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji 


Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kushiriki na kufungua rasmi Kongamano la kukuza Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji. Wakati wa Kongamano hilo mada mbalimbali kuhusu fursa za uwekezaji baina ya nchi hizi mbili zilitolewa.

Mhe. Rais Nyusi kwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe. Christopher Chiza (kushoto) wakifuatilia mada za uwekezaji zilizowasilishwa wakati wa kongamano la kukuza uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji
Wajumbe waliohudhuria kongamano hilo.







Press Release


H.M King Harald V of  Norway
PRESS RELEASE

H.E President Jakaya Mrisho Kikwete of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.M. King Harald V of Norway on the occasion to celebrate the Norwegian Constitution Day on 17th May, 2015.

The message reads as follows: -

“Your Majesty King Harald V,
   The King of Norway,
   Oslo,
   NORWAY.

It is my pleasure and privilege to extend to you, my heartfelt congratulations on the occasion of your country’s Constitution Day.

Norway and Tanzania have been enjoying excellent bilateral relations over the years. It is my strong desire that these ties of cooperation are maintained and strengthened for the benefit of our two countries and peoples.

I would like to take this opportunity to reaffirm Tanzania’s commitment to working with Norway on matters of mutual interest.

Please accept, Your Majesty, my personal best wishes for your continued good health and peace and prosperity for the people of Norway”.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International

Co-operation, Dar es Salaam


18th May, 2015

Sunday, May 17, 2015

Rais wa Msumbiji awasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Mhe. FilipeJacinto Nyusi mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Rais Nyusi ameanza ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini kuanzia tarehe 17 hadi 19 Mei, 2015.
Rais Kikwete akiwa na Rais Nyusi kwenye Jukwaa Maalum wakati nyimbo za Taifa la Tanzania na Msumbiji zikipigwa kwa heshima ya Rais Nyusi
Mhe. Rais Nyusi akikagua Gwaride la Heshima
Gwaride la Heshima likipita mbele ya Marais
JUU na CHINI: Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na mgeni wake Mhe. Rais Nyusi wakifurahia burudani kutoka kwenye vikundi vya ngoma vilivyokuwepo uwanjani hapo wakati wa mapokezi. Wengine wanaoonekana kwenye picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (mwenye tai nyekundu), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Mhe. Oldemiro Baloi (mwenye miwani myeusi)
Shamrashamra za mapokezi kama inavyoonekana.




  




Saturday, May 16, 2015

Rais wa Msumbiji kufanya ziara ya kitaifa nchini


Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 17 Mei, 2015 kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Rais Nyussi atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Rais Nyusi atakagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21.

Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Nyusi atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete yakifuatiwa na mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji.

Baadaye siku hiyo ya Mei 17, Mhe. Rais Nyusi atakutana kwa mazungumzo na Mabalozi kutoka Nchi za Afrika waliopo hapa nchini mkutano utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam na kushiriki Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete, Ikulu.

Mhe. Rais Nyusi ambaye ataongozana na Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Msumbiji atahutubia Kongamano la Biashara litakalowakutanisha Wafanyabiashara wa nchi hizi mbili ambalo litafanyika tarehe 18 Mei, 2015 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Aidha, siku hiyo ya tarehe 18 Mei, Mhe. Nyusi atapata fursa ya kukitembelea Chuo cha Diplomasia kinachotambulika kama “Tanzania-Mozambique Centre for Foreign Relations” kilichopo Kurasini ambacho kilianzishwa mwaka 1978 kama mradi wa ubia ili kuendeleza mahusiano ya kindugu ya muda mrefu kwa lengo la kutoa mafunzo ya diplomasia na masuala ya kimataifa kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.

Mhe. Nyusi atakutana na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini kabla ya kuelekea Zanzibar ambako atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia kuzungumza na raia wa Msumbiji waliopo Zanzibar.

Akiendelea na ziara yake hapa nchini, Mhe. Rais Nyusi ataondoka Zanzibar tarehe 19 Mei, 2015 kuelekea Dodoma. Akiwa Mkoani humo atatembelea Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mhe. Rais Nyusi atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mhe. Rais Nyusi anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 19 Mei, 2015 na kuondokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kurejea Msumbiji.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam.
16 Mei, 2015



Thursday, May 14, 2015

Waziri Membe afungua Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akifungua Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo. Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2015. Katika hotuba yake, Waziri Membe aliwahimiza Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma
 Sehemu ya Wajumbe wa Baraza  wakifuatilia hotuba ya Waziri Membe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tisa wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Mkutano ukiendelea huku Wajumbe wa Baraza wakiwa makini kumsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mhe. Waziri Membe akiendelea na hotuba ya ufunguzi wa baraza hilo.
  Sekretarieti ya Baraza hilo wakiendelea na kazi ya kunukuu kile kinachozungumzwa na Waziri Membe kwa kumbukumbu

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya naye akizungumza machache wakati wa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, BibiRosemary Jairo akitoa neno la shukrani kwa Waziri Membe kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi.Mindi Kasiga ambaye pia alikuwa Mshereheshaji wakati wa mkutano huo
Waziri Membe akiwa kwenye  Picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Wawakilishi wa TUGHE Taifa na Mkoa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa Mhe.Bernard Membe (Mb) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua baraza la wafanyakazi wa wizara ya Nje na ushirikiano wa kimataifa.


Picha na Reuben Mchome


Wednesday, May 13, 2015

Rais Kikwete aongoza Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC uliofanyika Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa  Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam kujadili hali nchini Burundi. Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulilaani vikali jaribio la mapinduzi nchini Burundi na kuzitaka pande zote nchini humo kuhakikisha hali ya uvunjifu wa amani inakoma mara moja. 
Wajumbe wa mkutano wakimsikiliza Rais  Kikwete (hayupo pichani).
Wajumbe mbalimbali wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsiki
Wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais Kikwete (hayupo pichani).
Mkutano ukiendelea
Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Watatu  kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni, (aliyeshikilia kofia),  Rais wa Rwanda, Mhe. Poul Kagame, (Wa tatu kulia), Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta (wapili kulia), Naibu Rais wa Afrika Kusini, Mhe.Cyril Ramaphosa (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Bibi Nkosazana Dlamini-zuma
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Simba Yahya (aliyesimama) akijadiliana jambo na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Ladislaus Komba (Kushoto) baada ya mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC kumalizika.
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji  Joseph Sinde Warioba (Katikati) akizungumza jambo huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bibi. Joyce Mapunjo  pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Bwa. Innocent Shiyo wakimsikiliza 

Picha na Reginald Philip

EAC SUMMIT DISCUSSES THE SITUATION IN BURUNDI 13TH MAY 2015


Tuesday, May 12, 2015

Waziri Membe aongoza Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa EAC


Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri  wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujadili mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera 

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Watu Mashuhuri wanaofuatilia hali ya usalama nchini Burundi akijadili jambo na Mjumbe wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika kujadili hali nchini Burundi
Wajumbe mbalimbali wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani). 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Louise Mushikiwabo  
 Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi Bi. Victoria Mwakasege akinukuu yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.) akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba kabla ya kuanza kwa  mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Mushikiwabo (aliyetangulia), akiongozana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Picha na Reginald Philip.
==============================


Waziri Membe aongoza Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa EAC

Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umefanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa agenda za Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi  wa Jumuiya  hiyo utakaofanyika tarehe 13 Mei, 2015 kujadili hali ya usalama nchini Burundi.

Akifungua Mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) alisema kuwa nchi ya Burundi inapita kwenye wakati mgumu wakati ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameitisha mkutano huo wa dharura kujadili suala hilo na kutafuta ufumbuzi.

Waziri Membe alieleza kuwa, hali ya usalama nchini humo kwa sasa si shwari huku kukiwa na mfululizo wa maandamano ya wananchi na tayari zaidi ya Wakimbizi 50,000 wamekimbilia nchi  jirani ikiwemo Tanzania, Rwanda na Uganda.

“Lengo mojawapo la Jumuiya ya EAC ni kuhakikisha nchi zote wanachama zinakuwa katika hali ya amani, usalama na utulivu hivyo ni wakati muafaka mkutano huu kufanyika” alisisitiza Waziri Membe

Mhe. Membe aliongeza kuwa Mkutano huo ambao umehudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa EAC yaani Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili Taarifa ya Timu ya Watu Mashuhuri (Eminent Persons) walioteuliwa kufuatilia hali ya usalama nchini Burundi kutoka EAC na Jumuiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba.

Aidha, Mkutano huo pia utapokea na kujadili Taarifa ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje waliotembelea Burundi hivi karibuni kwa ajili ya kupata taarifa za ndani za hali ilivyo nchini humo; Taarifa ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Eneo la Maziwa Makuu; Taarifa ya Kamishna wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika na Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya Uenyekiti wa Rais Kikwete utafanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Mei, 2015 na utahudhuriwa na Marais wan chi wanachama wa Jumuiya hiyo akiwemo Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda, Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda, Mhe. Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi na Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya.

Viongozi wengine walioalikwa kushiriki Mkutano huo ni pamoja na Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma ambaye atawakilishwa na Naibu Rais, Mhe. Cyril Ramaphosa, Kamishna wa Umoja wa Afrika, Mhe. Bibi Nkosazana Dlamini Zuma, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Said Djinnit; Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR), Prof. Ntumba Luaba, Kamishna wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika na Wawakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU).

-Mwisho-