Monday, June 8, 2015

Balozi wa China amtembelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youquig alipomtembelea Wizarani kwa mazungumzo ya kudumisha ushirikiano wa nchi hizi mbili.
 Mkalimani wa Balozi wa China Bi.Wang Fang akisalimiana na Katibu Mkuu 

Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youqing akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa China huku Maafisa wa pande zote mbili wakinukuu kile kinachozungumzwa.
 Balozi wa China, Mhe.Lu akifurahia jambo na Balozi Mulamula
Balozi Lu Youqing akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Maafisa kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Mr.Dong (kulia), Mr.Lin Liang (katikati) na Bi.Wang Fang wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw.Nathaniel Kaaya (wa kwanza kushoto) kwa pamoja na  Maafisa  Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza (wa kwanza kulia) pamoja na Bi.Ramla Hamis wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu (hawapo pichani).

 Picha na Reuben Mchome

Friday, June 5, 2015

Tanzania yachaguliwa Mjumbe Baraza la Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (mwenye suti nyeusi) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa 17 wa Shririka la Hali ya Hewa Duniani unaofanyika Mjini Geneva, Uswisi. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Celestine Mushy (Kulia)
===================================
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TANZANIA YACHAGULIWA KUWA MJUMBE KATIKA BARAZA LA UTENDAJI (EXECUTIVE COUNCIL) LA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI–WORLD METEOROLOGICAL ORGANIZATION (WMO).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi, amechaguliwa kuwa Mjumbe katika Baraza la Utendaji (Executive Council) la Shirika la Hali ya Hewa Duniani–World Meteorological Organization (WMO) kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2015 hadi 2019. Dr. Kijazi amechaguliwa tarehe 4 June 2015 wakati wa Mkutano Mkuu wa Kumi na Saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Congress wa 17) ulioanza tarehe 25 Mei 2015 na unatarajiwa kumalizika tarehe 12 Juni, 2015 Jijini Geneva, Uswisi.

Kuchaguliwa kwa Dr. Agnes Kijazi kumetokana na jitihada zilizofanywa na Ubalozi wetu wa Kudumu Umoja wa Mataifa wa Geneva na Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambazo kwa pamoja zilisimamia zoezi la kuomba kura kutoka kwa wanachama na kampeni wakati wa uchaguzi. 

Dr. Kijazi ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika ushiriki Mkutano huo ambao una washiriki kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Maji na Ubalozi wa Tanzania Nchini Uswisi.

WMO ni Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya hali ya hewa duniani na mabadiliko ya tabianchi. WMO inatekeleza majukumu na maamuzi kuhusu maendeleo ya sayansi ya hali ya hewa na uboreshaji wake ikiwa ni pamoja na kusimamia viwango katika upimaji na utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa nchi wanachama.

Hadi wakati wa Mkutano huu huko nchini Uswisi, WMO ilikuwa na nchi wanachama 191. Katika Mkutano huu nchi za Sudan Kusini na Tuvalu zilikaribishwa rasmi kama wanachama wapya wa WMO. Kati ya nchi hizi 191 ni nchi 37 tu ambazo zina wajumbe katika Baraza hilo kuu. Hivyo hii ni nafasi adhimu na heshima kwa Tanzania, TMA na Dr Kijazi ambaye ni msomi mwenye utaalamu wa kutosha akiwa na Shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika Sayansi ya Hali ya hewa.

Kazi kuu ya Baraza la Utendaji la WMO, ambalo Tanzania imefanikiwa kuwa mjumbe ni kuchukua hatua zinazostahili, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Shirika hilo kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mkutano Mkuu (WMO-Congress) ambao hukutana mara moja kila baada ya miaka minne.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alielezea sababu ya Tanzania kugombea nafasi hiyo muhimu kuwa ni pamoja na  kuwa ndani ya chombo cha maamuzi na hivyo kushawishi maamuzi yatakayoinufaisha jamii nzima ya kimataifa ikiwemo Tanzania katika masuala ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kutoa mwelekeo wa kisayansi katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea katika maeneo mengi Duniani.

Kwa upande wake, Dkt. Kijazi alieleza kuridhishwa kwake na jinsi ambavyo nchi wanachama 190 walivyoridhishwa na utendaji wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu (2012-2015) ambacho alikuwa mjumbe wa Baraza hili na hivyo kumchagua tena katika kipindi kingine cha miaka minne. “Hii ni heshima kubwa kwa nchi yangu ya Tanzania na ninaahidi kutumia uwezo wangu wote kutekeleza majukumu ya nafasi hii” alisema Dkt. Kijazi.

Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam

05 Juni, 2015


Balozi Hamza awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme wa Jordan

Balozi wa Tanzania nchini Jordani mwenye makazi yake Kairo Misri Mhe. Mohammed Hamza Mohammed akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme Abdallah II wa Jordan
Balozi Hamza akimsikiliza Mfalme Abdallah II mara baada ya kumaliza kuwasilisha Hati za Utambulisho.



Thursday, June 4, 2015

Balozi wa China Nchini amtembelea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akimsikiliza Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youqing alipomtembelea Wizarani leo.
 Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu akifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje Balozi Simba huku Maofisa wa Ubalozi wa China waliofuatana na Balozi wakifuatilia mazungumzo hayo.
 Balozi Simba akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea huku Maofisa wa Ubalozi wa China hapa nchini wakiendelea kunukuu kile kinachozungumzwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia Bw.Nathaniel Kaaya (wa pili kushoto) akifuatilia mazungumzo hayo huku Maofisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza (wa kwanza kulia) pamoja na Bi.Ramla Hamis wakiendelea kunukuu kile kinachozungumzwa.
 Mkutano ukiendelea

Monday, June 1, 2015

Balozi Mulamula akabidhiwa rasmi Ofisi

Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Liberata Mulamula akikabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Balozi John Haule. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mulamula alikuwa Balozi  wa Tanzania nchini Marekani na Mhe.  Haule kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya. Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani leo tarehe 01 Juni, 2015.
Balozi Mulamula akizungumza huku Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya, (kulia kwa Balozi Mulamula), Mhasibu Mkuu Bw. Paul Kabale (wa tatu kutoka kushoto), Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mambo ya Nje, Bw. Mathias Abisai na Afisa Habari wa Mambo ya Nje Bw. Ally Kondo
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Nigel Msangi (wa kwanza kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango Bw. James Lugaganya na  Balozi Haule wakimsikiliza Balozi Mulamula  (hayupo pichani)
Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akiwa kwenye Mkutano na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Balozi Haule.


Picha na Reginald Philip

Mabalozi wa Tanzania nchi za Nje wafanya ziara maalum Chuo Kikuu Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga ambaye pia alikuwa Mkuu wa Msafara wa ziara ya  Mabalozi wa Tanzania walipotembelea Chuo Kikuu cha Dodoma akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof.Shaaban Mlacha mara baada ya kuwasili chuoni hapo.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Begum Taj akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Mlacha mara baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ziara maalum.
Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Mhe. Modest Mero akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Mlacha mara baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ziara maalum.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma akiwaongoza  Mabalozi wa Tanzania na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  mara baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ziara maalum.
 Mabalozi wa Tanzania wakisikiliza kwa makini historia fupi ya Chuo hicho kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Prof. Mlacha muda mfupi baada ya kuwasili chuoni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia alikuwa Mkuu wa Msafara wa ziara ya Mabalozi, Bi. Mindi Kasiga  akizungumza machache kuwakaribisha Waheshimiwa Mabalozi   kuanza kikao na uongozi wa chuo hicho.
Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa,  Mhe.Tuvako Manongi akichangia jambo katika mkutano huo.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Peter Kalaghe naye akitoa mchango wake wakati wa mkutano huo.
Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. John Kijazi akichangia mada wakati wa mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe.Radhia Msuya na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe.Philip Marmo
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma Prof. Mlacha ( aliyesimama mbele)akizungumza wakati wa  kikao chake na Mabalozi wa Tanzania walipotembelea chuoni hapo.
Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Dodoma(aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo wakati wa ziara fupi ya kuzunguka Chuo hicho huku Waheshimiwa Mabalozi wakiangalia kwa makini maeneo ya chuo hicho.
Balozi Tanzania nchini Uganda, Mhe. Ladislaus Komba (kulia) na Mhe.Anthony Cheche wakiangalia mazingira na majengo ya aina yake ya  chuo hicho kama yanavyoonekana kwa mbali.
Picha ya Pamoja.
===============

Picha na Reuben Mchome na Reginald Philip.

WAZIRI MEMBE AWASIHI WATANZANIA KUTOCHAGUA VIONGOZI WANAOSAKA UONGOZI KWA KUTOA RUSHWA

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe (Mb) akimkabidhi Bi. Shamim Khan tuzo ya heshima ya kujishughulisha na kazi za kijamii hapa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe  akizungumza katika tamasha hilo la kwanza Qaswida, lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa,Mh Membe amewataka Watanzania kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,

Alisema siku hiyo ya Juni 6, wananchi wasikilize nini anataka kuifanya nchi iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo. “Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa nchi ni ule wa kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, maadili kwa viongozi ni muhimu,” alisema Waziri Membe.

Mhe.Membe alitumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania kuacha kuchagua viongozi ambao kwa nje, wanajinadi  wana dini, lakini matendo hayaendani na maadili ya  dini zao. Alisema ili mtu aweze kuaminika kuwa ana dini, jamii ifuatilie katika madhehebu yao, hivyo amewasihi wasichague viongozi wanaosaka uongozi kwa kutoa rushwa.

“Msikubali kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi kuwa na dini kinyume na matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu ambayo husisitizwa na dini zote,” Alisema uongozi wa heshima ni ule unaochukia rushwa ambayo ni adui wa haki, hivyo amewataka wananchi kuwaogopa wapenda rushwa kama ukoma. 
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria tamasha hilo.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.
Mmoja wa washiriki wa tamasha la Qaswida kutoka Madrasa ya Nur-Pugu,Samiu Mussa akighani Qaswida mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye tamasha hilo,lililodhaminiwa na kampuni ya Dira  ya Mtanzania
Kikundhi cha Qaswida kiitwacho Iqhyau wakighani Qaswida ya maadili
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe (Mb) akipokelewa na wenyeji wake alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,kwa ajili ya kushiriki tamasha la kwanza la Qaswida
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulamaa Qaswida Promotions ambao ndio waandaji wa tamasha la kwanza la Qaswida,Ustaadh Jumanne Ligopora akimkaribisha mgeni rasmi  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe 
Sheikh Ismail Mohamed akizungumza jambo na Waziri Membe wakati wa tamasha la kwanza la Qaswida lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.
Waimbaji wa Qaswida kutoka kikundi cha Muumini cha Buguruni jijini Dar es Salaam wakiimba kwenye tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.

Media Release


 
                                                              


                                                   MEDIA RELEASE

The Joint Meeting of the COMESA-EAC-SADC Tripartite Sectoral Ministerial Committee took place on 29th -30th May 2015 in Dar es Salaam. The purpose of the meeting was to consider progress made in preparation for the Third COMESA-EAC-SADC Tripartite Summit to be held on 10th June 2015.

The Tripartite Summit launched the Free Trade Area in 2011 when SADC took over the chairpersonship and will be handing over the chairpersonship to COMESA at the third Summit scheduled to take place in June, 2015. Negotiations are at advanced stages and the COMESA-EAC-SADC Tripartite Free Trade Area is expected to be launched at Sharm El Sheikh on 10th June, 2015.

When concluded, the Tripartite FTA will encompass 26 Member States, that is, half of the African Continent with a GDP of over US$1.2 trillion that represents over 50% of the Continent’s GDP, and a population of 625 million. When operational, it will become a means for enhancing economic inter-linkages and enabling business environment to unlock regional potentials, scale up productive capacities and competitiveness, stimulating beneficiations and value chains, enhancing technological set-ups. More importantly, the TFTA will also address the issue of overlapping membership that has resulted in a number of challenges for the region’s business and trading community. It is foreseen that the TFTA will constitute an important foundation for the continental free trade area negotiations that will be launched by the African Union Summit in June 2015 towards the realisation of Agenda 2063 of the African Union.

Ministers reiterated the importance of making tariff offers and concluding related negotiations expeditiously. In this regard they decided that MemberStates that had not exchanged tariff offers do so within 6 -12 months and those that have exchanged and are negotiating tariff offers should endeavour to conclude within 12 months. They noted that rules of origin are a crucial element for the TFTA and therefore Member States needed to expedite work to finalise outstanding areas and agree on the Tripartite rules of origin that will be applied in the new TFTA.
The Meeting also endorsed the transitional arrangements on trade remedies that will apply to the TFTA pending the finalisation of a complete Annex in this area. It should be noted that the TFTA Agreement already includes detailed dispute settlement disciplines and a completed Annex on Tripartite Dispute Settlement Mechanism.

It is worth noting that the SADC region has adopted a Strategy and Roadmap on Industrialisation and therefore the incorporation of the pillars on Industry and Infrastructure are important and strategic components for the success of the Tripartite agenda. From a SADC perspective the Industrialisation work programme should result in the economic and technological transformation of the region, engender competitiveness as an active process to move from comparative advantage to competitive edges, reinforce regional integration and ultimately the development and economic prosperity of the Community. SADC would be implementing this strategy jointly with other regional priorities outlined in the Regional Infrastructure Development Medium Term Plan and the Regional Indicative Strategic Development Plan.

The SADC Industrialisation Strategy is anchored on three pillars, namely: Industrialisation as a champion of economic and technological transformation; competitiveness as an active process to move from comparative advantage to competitive edges, and Regional integration and geography as the context for industrial development and economic prosperity. The important features of the Industrialisation Strategy are focused programmes aimed at enhancing economic inter-linkages to unlock regional potentials, scaling up productive capacities and competitiveness, stimulating beneficiations and value chains, enhancing technological set-ups, and improving the business enabling environment. The implementation of the strategy will be underpinned on sound policies and appropriate enabling environment across the Member States.

In the area of ICT, commendable progress has been made in the SADC region with the roll out of Digital Terrestrial Migration equipment given the looming ITU switch-over deadline of 17 June, 2015.

SADC has developed and adopted the Regional Infrastructure Development Master Plan (RIDMP) which defines SADC’s infrastructure development strategy and constitute basis for prioritization of projects, as well as the modus operandi for implementation. The RIDMP constitutes the approved SADC Regional Infrastructure Development Programme and guides the process of selection and implementation of regional infrastructure projects at the level of feasibility assessments, preparation for bankability and investment.   It also constitutes the basis for SADC Member States commitment to a common infrastructure development programme.

NB: For any further information and clarification, SADC Executive Secretary, H.E. Dr. Stergomena Lawrence Tax is available for an interview.


For inquiries: Dr. Charles Mubita 0682994688