Saturday, June 13, 2015

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wa kazi nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango wakimsikiliza kwa furaha Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe.Francisco Suarez Luz (kushoto) kabla ya kuanza kwa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga Balozi Luz. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Juni, 2015.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula kwa pamoja na Balozi Mpango wakiendelea kumsikiliza Balozi Luz mara baada ya kuketi tayari kwa kushiriki chakula cha mchana kwa heshima ya kumuaga Balozi Luz.
Meza Kuu wakiwemo Mabalozi kutoka nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Francisco Suarez Luz. Katika hotuba yake alimshukuru Balozi huyo kwa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika kipindi chote alichokuwepo nchini na kumuomba aendelee kuwa Balozi mzuri kwa kuitangaza Tanzania.
Balozi Luz pamoja na Mablozi wengine wakimsikiliza Balozi Mulamula ambaye haonekani pichani
Balozi Luz nae akitoa hotuba yake ambapo aliisifu Tanzania kuwa ni nchi ya amani na kwamba nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula pamoja na Mabalozi wengine wakimsikiliza Balozi Luz (hayupo pichani)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula na Balozi Luz wakigonga glasi kama ishara ya kuutakia heri ushirikiano kati ya Tanzania na Brazil 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula akimkabidhi Balozi Luz zawadi ya picha ya mchoro unaoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania. Anayeshuhudia ni Bi. Felister Rugambwa, Afisa Mambo ya Nje.
Sehemu ya Mabalozi wakishuhudia Balozi Luz akipewa zawadi (hayupo pichani)
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa  Balozi wa Brazil hapa nchini. Kushoto ni Bw. Leonce Bilauri na Bi. Felister Rugambwa
Balozi wa Namibia hapa nchini akiwa pamoja na Balozi wa Cuba nchini.
Balozi wa Urusi hapa nchini Mhe. Yuri Fedorovich Popov (kushoto) akimweleza jambo mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Brazil
Sehemu nyingine ya Wageni waalikwa


Waziri Membe awaaga Mawaziri wa nchin wanachama wa Umoja wa Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimtaifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisoma Hotuba ya kuwaaga Mawaziri wenzake katika mkutano wa Mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Naimi Azizi (wa Nne kulia), Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Balozi Dkt. Mohamed Maundi, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika Bi. Zuhura Bundala pamoja na ujumbe alioambatana nao



Friday, June 12, 2015

Watanzania wengine 13 warejea kutoka nchini Yemen

Kiongozi wa msafara wa Watanzania kumi na tatu waliorejea leo nchini wakitokea nchini Yemeni, Bw.Faiz Abdulsheikh Said akizungumza na Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Asha Mkuja wakati wa mapokezi ya Watanzania hao walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Shirika la Ndege la Qatar. Serikali imefanikiwa kuwarejesha nchini zaidi ya Watanzania 100  kutoka Yemen baada ya nchi hiyo kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Zoezi la kuwarejesha Watanzania hao linaratibiwa na kusimamiwa na Wizara kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman. Watanzania wengine 15 wanatarajiwa kuwasili nchini kesho tarehe 13 Juni, 2015.
Bi. Asha Mkuja akiendelea kupata maelezo kutoka kwa mmoja wa Watanzania hao Mzee Bader Saleh Omar kuhusu hali ilivyo nchini Yemen.
 Mazungumzo yakiendelea
 Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha akimsikiliza kwa makini mzee Bader, akimpa maelezo ya hali ilivyo huko Nchini Yemen.
 Watanzania hao wakijiandaa kuondoka ndani ya Uwanja wa Ndege baada ya kukamilisha taratibu zote.

Picha na Reuben Mchome

Wednesday, June 10, 2015

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje aongoza maadhimisho ya siku ya Taifa la Sweden

Mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
 Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filberto Cerian Sebregondi akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula huku Afisa wa Wizara hiyo Bi.Asha Mkuja (kushoto mwenye kilemba).
 Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe.Balozi Juma Halifan Mpango akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Katibu Mkuu Mulamula akiendelea na hotuba yake,kushoto ni Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe.Lennarth 
 Balozi Lennarth  na Katibu Mkuu Balozi Mulamula pamoja na wageni waalikwa wakinyanyua glasi kutakiana kheri katika ushirikiano wa nchi hizi mbili.
 Balozi wa Sweden Mhe.Lennarth  akicheza kwa furaha pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi huo hapa nchini kama ishara ya kufurahia maadhimisho ya siku ya Taifa lao la Sweden sherehe zilizofanyika katika makazi ya balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha watoto wa Maafisa wa Ubalozi wa Sweden hapa nchini walioshiriki hafla hiyo kwa wakiimba kwa ufasaha nyimbo za Mataifa ya Sweden na Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa   Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na     Waandishi wa abari katika hafla hiyo.

                            ===================
                          Picha na Reuben Mchome.

Tuesday, June 9, 2015

Balozi Mulamula akutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa EU hapa nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Kiongozi wa Ujumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Balozi Filberto Cerian Sebregondi alipofika Wizarani kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Jumuiya  hiyo na Tanzania na pia kujitambulisha kwa Balozi Mulamula ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje. 
Maafisa Mambo ya Nje Waandamizi wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi (hawapo pichani).
Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Diana Melrose kwa pamoja na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Mhe Adam Koeler na Maaafisa wengine  kutoka nchi za EU  wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi.
Balozi Mulamula na Balozi  Sebregondi wakimsikiliza Balozi Melrose akifafanua jambo
Kikao kikiendelea

Picha na Reginald Philip

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje azungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Balozi Linda Thomas - Greenfield alipotembelea Wizarani na kufanya mazungumzo yaliyojikita katika kukuza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani katika Sekta mbalimbali.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress pamoja na ujumbe ulioambatana na Mhe. Thomas - Greenfield nao wakifuatilia mazungumzo.
Balozi Linda akitoa ufafanuzi wa jambo huku Balozi Mulamula akimsikiliza kwa makini. 
Balozi Mulamula (katikati) akimsikiliza Mhe. Linda alipokuwa akizungumza naye kulia ni Afisa Mambo ya Nje Bwa. Lucas Mayenga. 
Mazungumzo yakiendelea
 Balozi Liberatta Mulamula akimlaki kwa furaha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Balozi Linda Thomas - Greenfield wakati alipowasili na kufanya mazungumzo yaliyojikita katika kukuza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani katika Sekta mbalimbali.


Picha na Reginald Philip.


Monday, June 8, 2015

Balozi wa China amtembelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youquig alipomtembelea Wizarani kwa mazungumzo ya kudumisha ushirikiano wa nchi hizi mbili.
 Mkalimani wa Balozi wa China Bi.Wang Fang akisalimiana na Katibu Mkuu 

Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youqing akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa China huku Maafisa wa pande zote mbili wakinukuu kile kinachozungumzwa.
 Balozi wa China, Mhe.Lu akifurahia jambo na Balozi Mulamula
Balozi Lu Youqing akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Maafisa kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Mr.Dong (kulia), Mr.Lin Liang (katikati) na Bi.Wang Fang wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw.Nathaniel Kaaya (wa kwanza kushoto) kwa pamoja na  Maafisa  Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza (wa kwanza kulia) pamoja na Bi.Ramla Hamis wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu (hawapo pichani).

 Picha na Reuben Mchome

Friday, June 5, 2015

Tanzania yachaguliwa Mjumbe Baraza la Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (mwenye suti nyeusi) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa 17 wa Shririka la Hali ya Hewa Duniani unaofanyika Mjini Geneva, Uswisi. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Celestine Mushy (Kulia)
===================================
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TANZANIA YACHAGULIWA KUWA MJUMBE KATIKA BARAZA LA UTENDAJI (EXECUTIVE COUNCIL) LA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI–WORLD METEOROLOGICAL ORGANIZATION (WMO).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi, amechaguliwa kuwa Mjumbe katika Baraza la Utendaji (Executive Council) la Shirika la Hali ya Hewa Duniani–World Meteorological Organization (WMO) kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2015 hadi 2019. Dr. Kijazi amechaguliwa tarehe 4 June 2015 wakati wa Mkutano Mkuu wa Kumi na Saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Congress wa 17) ulioanza tarehe 25 Mei 2015 na unatarajiwa kumalizika tarehe 12 Juni, 2015 Jijini Geneva, Uswisi.

Kuchaguliwa kwa Dr. Agnes Kijazi kumetokana na jitihada zilizofanywa na Ubalozi wetu wa Kudumu Umoja wa Mataifa wa Geneva na Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambazo kwa pamoja zilisimamia zoezi la kuomba kura kutoka kwa wanachama na kampeni wakati wa uchaguzi. 

Dr. Kijazi ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika ushiriki Mkutano huo ambao una washiriki kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Maji na Ubalozi wa Tanzania Nchini Uswisi.

WMO ni Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya hali ya hewa duniani na mabadiliko ya tabianchi. WMO inatekeleza majukumu na maamuzi kuhusu maendeleo ya sayansi ya hali ya hewa na uboreshaji wake ikiwa ni pamoja na kusimamia viwango katika upimaji na utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa nchi wanachama.

Hadi wakati wa Mkutano huu huko nchini Uswisi, WMO ilikuwa na nchi wanachama 191. Katika Mkutano huu nchi za Sudan Kusini na Tuvalu zilikaribishwa rasmi kama wanachama wapya wa WMO. Kati ya nchi hizi 191 ni nchi 37 tu ambazo zina wajumbe katika Baraza hilo kuu. Hivyo hii ni nafasi adhimu na heshima kwa Tanzania, TMA na Dr Kijazi ambaye ni msomi mwenye utaalamu wa kutosha akiwa na Shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika Sayansi ya Hali ya hewa.

Kazi kuu ya Baraza la Utendaji la WMO, ambalo Tanzania imefanikiwa kuwa mjumbe ni kuchukua hatua zinazostahili, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Shirika hilo kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mkutano Mkuu (WMO-Congress) ambao hukutana mara moja kila baada ya miaka minne.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alielezea sababu ya Tanzania kugombea nafasi hiyo muhimu kuwa ni pamoja na  kuwa ndani ya chombo cha maamuzi na hivyo kushawishi maamuzi yatakayoinufaisha jamii nzima ya kimataifa ikiwemo Tanzania katika masuala ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kutoa mwelekeo wa kisayansi katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea katika maeneo mengi Duniani.

Kwa upande wake, Dkt. Kijazi alieleza kuridhishwa kwake na jinsi ambavyo nchi wanachama 190 walivyoridhishwa na utendaji wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu (2012-2015) ambacho alikuwa mjumbe wa Baraza hili na hivyo kumchagua tena katika kipindi kingine cha miaka minne. “Hii ni heshima kubwa kwa nchi yangu ya Tanzania na ninaahidi kutumia uwezo wangu wote kutekeleza majukumu ya nafasi hii” alisema Dkt. Kijazi.

Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam

05 Juni, 2015


Balozi Hamza awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme wa Jordan

Balozi wa Tanzania nchini Jordani mwenye makazi yake Kairo Misri Mhe. Mohammed Hamza Mohammed akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme Abdallah II wa Jordan
Balozi Hamza akimsikiliza Mfalme Abdallah II mara baada ya kumaliza kuwasilisha Hati za Utambulisho.