Wednesday, July 22, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Sweden aliyemaliza muda wa kazi nchini

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Sweden hapa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kazi, Mhe. Lennarth Hjelmaker. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Sweden anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Lennarth Hjelmaker akimsikiliza Balozi Kasyanju (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya kumuaga Balozi huyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
Balozi Sokoine akizungumza kuwakaribisha Wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Sweden aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Balozi Kasyanju (katikati) na Balozi Hjelmaker (kushoto) kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini, Mhe. Juma Halfan Mpango (kulia) wakimsikiliza Balozi Sokoine ambaye hayupo pichani.
Balozi Hjelmaker nae akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa kumpatia ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha miaka mitano aliyokuwepo hapa nchini kama Balozi wa Sweden. 
Balozi Hjelmaker akizungumza huku wageni waalikwa wakimsikiliza
Balozi Kasyanju akimkabidhi Balozi Hjelmaker zawadi ya picha ya kuchora ya  Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania
Balozi Kasyanju akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Hjelmaker na Balozi Mpango
Maafisa Mambo ya Nje walioshiriki hafla hiyo
Picha ya pamoja
Balozi Kasyanju akiagana na Balozi Hjelmaker mara baada ya hafla ya kumuaga kukamilika.

Picha  na Reginald Philip

Tuesday, July 21, 2015

Kongamano la Pili la Diaspora kufanyika hapa nchini mwezi Agosti


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Rosemary Jairo akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa Habari juu ya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora and SMEs partnership 2015) litakalofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015, likiwa na kaulimbiu isemayo 'Creating Linkages between Diaspora and local SMEs in Tanzania' 
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea
Picha na Reginald Philip

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA



Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              


 



  
 


20 KIVUKONI FRONT P.O. BOX 9000,
11466 DAR    ES SALAAM,                             Tanzania.








TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade Centre UN-Agency) inafanya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora & SMEs Partnership Conference 2015). Kongamano husika litafanyika hapa Dar es Salaam, kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015 katika Hoteli ya Serena. Kongamano hilo litakuwa la pili kufanyika hapa nchini na litahusisha Diaspora na Wadau wa hapa Tanzania.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ndio Wadau Wakuu katika Maandalizi ya Kongamano hili.
Kongamano la mwaka huu lina Kauli Mbiu, ‘Creating Linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania’ na Dhumuni lake ni kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara Ndogo na za Kati hapa nchini. Kongamano la mwaka huu pia litahusisha Mikoa ya Tanzania ambapo Mikoa itapata fursa ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mikoani.
Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Aidha, katika kuhitimisha kilele cha Kongamano hilo, Diaspora wanatarajiwa kufanya ziara Zanzibar tarehe 15 Agosti 2015, ikiwa ni sehemu ya mwaliko maalum kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pamoja na Shughuli za Ufunguzi na Kilele, Matukio muhimu yatakuwa ni Maonesho ya Kibiashara, Majadiliano ya Mada kuhusu Ushirikishwaji wa Diaspora kwa Maendeleo ya Nchi hususan SMEs, uwekezaji Mikoani n.k.

Kongamano hilo litahudhuriwa na Watanzania Wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) na wale waliorejea hapa nchini na Wadau wa Maendeleo kutoka hapa nchini.

Wizara ya Mambo ya Nje Usually integration involves one or more written agreements that describe the areas of cooperation in detail, as well as some coordinating bodies representing the countries involved.inawakaribisha kushiriki nasi katika Kongamano hilo. Tafadhali tembeleeni tovuti ya (www.tzdiaspora.com) kupata taarifa muhimu hususan kuhusu Ada za Ushiriki, fursa za Kufadhili na namna ya kujisajili.

Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
21 Julai, 2015


Monday, July 20, 2015

Ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka Nigeria watembelea Wizara ya Mambo

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akiukaribisha Ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi ya Taifa ya Mafunzo ya Sera na Stratejia ya Nigeria walipotembelea Wizarani  tarehe 20 Julai, 2015. Ujumbe huo upo nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku 12 ambapo watatembelea Wizara na Taasisi mbalimbali za hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu kuzungumza na ujumbe huo kutoka Nigeria.
 JUU NA CHINI:
Baadhi ya wajumbe wa msafara huo wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

 Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Simba akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa msafara huo Bw.Hamakim Jonny Godwin. 
Picha ya pamoja.

Sunday, July 19, 2015

Wizara yawapokea Madaktari kutoka Marekani


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akiwakaribisha nchini Timu ya Madaktari kutoka Marekani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni. Madaktari hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa mbalimbali katika Hospitali za Mwananyamala ya Jijini Dar es Salaam na Mnazi Mmoja, Zanzibar. Ziara ya Madaktari hao ambao wametoka Majimbo ya Washington DC, Maryland na Virginia imeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani (Diaspora).
Rais wa Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani, Bw. Iddi Sandaly ambaye amefuatana na Madaktari hao kutoka Marekani akielezea jambo mara baada ya kuwasili nchini.
Bibi Jairo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu dhumuni la ziara ya madaktari hao hapa nchini.
Mmoja wa Madaktari kutoka Marekani akizungumza na Waandishi kuhusu  ziara yao hapa nchini
Bw. Sandaly akifafanua jambo kwa waandishi kuhusu ziara ya madaktari hao kutoka Marekani.

Thursday, July 16, 2015

Waziri Membe afuturisha Mashehe na watumishi wa Wizara

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mhe. Bernard K. Membe akiwakaribisha  Mashehe pamoja na  Watumishi wa Wizara (hawapo pichani)   kabla  ya kushiriki  Futari aliyoiandaa kwa ajili yao nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam  hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kulia), akiwa pamoja na Mashehe walioudhuria Futari hiyo
Waziri Membe akiendelea kuzungumza na kuwakarisha wageni wote nyumbani kwake
Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nigel Msangi akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Waziri Membe na Familia yake  kwa niaba ya Watumishi wa Wizara na Wageni wengine walioalikwa  kufuturu pamoja na Mhe. Membe nyumbani kwake
Mhe. Membe akiwa na Kadhi Mkuu walioshiriki futari hiyo
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki futari nyumbani kwa Mhe. Membe
Wageni waalikwa
Mke wa Waziri Membe, Mama Dorcas Membe (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju wakati wa futari iliyoandaliwa na Familia ya Waziri Membe kwa Watumishi wa Wizara.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba wakati wa futari nyumbani kwa Mhe. Membe. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa APRM, Bibi Rehema Twalib, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga na Bi. Aisha Mandia.
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa futari hiyo
Watumishi wa Wizara wakiwa wametulia kabla ya kuanza kufuturu
Waziri Membe akimpongeza Kadhi Mkuu baada ya kuhutubia
Shehe  akitoa dua kabla ya kuanza kufuturu
Dua ikiendelea
Mhe. Membe akiwaongoza wageni wake kuchukua futari

Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mashehe na Wageni wengine aliwaalika kufuturu pamoja nae.

Picha na Reginald Philip