Wednesday, August 26, 2015

Katibu Mkuu na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki wasaini mkataba

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula kwa pamoja na  Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki, Bw. Ziya  Karaham (kushoto) wakisaini mkataba ili kumwezesha Bw. Karaham kuendelea kuiwakilisha Tanzania nchini Uturuki. Mkataba huo ulisainiwa Wizarani tarehe 25 Agosti, 2015.
Balozi Mulamula na Bw. Karaham wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kuusaini
Balozi Mulamula akiagana na Bw. Karaham.

Tuesday, August 25, 2015

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Algeria nchini.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Wizarani Balozi wa Algeria nchini, Mhe. Saad Belabeb alipofika kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria pamoja na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu.
Balozi Mulamula akizungumza na Balozi Belabeb 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala kwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje katika Idara hiyo wakifurahia jambio wakati wa mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Belabeb (hawapo pichani).
Balozi Mulamula akimsikiliza Balozi Belabeb
Mazungumzo yakiendelea

=================================

TANZANIA NA ALGERIA KUIMARISHA USHIRIKIANO


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa Tanzania na Algeria zitaendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali ya maendeleo ili kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Balozi Mulamula ameyasema hayo alipokutana na Balozi wa Algeria hapa nchini, Mhe. Saad Belabeb ambaye alimtembelea Wizarani leo kwa lengo la kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu.

Katika mazungumzo yao, Balozi Mulamula alisema kuwa Tanzania na Algeria zimekuwa na ushirikiano wa karibu na wa kihistoria tangu kipindi cha waasisi wa mataifa haya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Rais Ahmed Ben Bella na kwamba kuuimarisha ushirikiano huo ni kuendelea kuwaenzi.

Aliongeza kusema kuwa, katika kipindi chote Tanzania na Algeria zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya na katika masuala yanayohusu Bara la Afrika  chini ya Umoja wa Afrika.

“Tanzania itasimama na Algeria  pamoja na marafiki zetu wengine ili kuhakikisha ushirikiano uliopo unaimarika na unaendelea mbele zaidi,” alisisitiza Balozi Mulamula.

Kwa upande wake, Balozi Belabeb alimpongeza Balozi Mulamula kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo alimhakikishia ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwake.

Balozi Belabeb alisema kuwa Tanzania ni rafiki muhimu kwa Algeria na hilo linathibitishwa na ziara mbalimbali za viongozi wakuu wa nchi hizi ikiwemo ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete mapema mwaka huu nchini Algeria.

-Mwisho-


Balozi mteule wa Switzerland awasilisha nakala za Hati za Utambulisho

 Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Switzerland hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, leo Tarehe 25-08-2015 ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri Bernard Membe akizungumza na Balozi Mteule wa Switzerland hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Balozi Mteule wa Switzerland hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), wakati alipokua akiwasilisha nakala ya hati zake za utambulisho leo Tarehe 25-08-2015

Mazungumzo yakiendelea huku Msaidizi wa Waziri Bw. Thobias Makoba (kulia) akisikiliza na kufuatilia mazungumzo hayo na Afisa wa Mambo ya Nje Bi. Olivia Maboko (kushoto) naye akifuatilia mazungumzo hayo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), akiagana na  Balozi Mteule wa Switzerland hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, leo Tarehe 25-08-2015 ofisini kwake jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.
===========
PICHA NA REUBEN MCHOME.

Monday, August 24, 2015

Katibu Mkuu akutana na Mwakilishi Maalum wa Marekani Eneo la Maziwa Makuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula akizungumza na Mwakilishi Maalum wa Marekani katika eneo la Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), Mhe. Thomas Perriello alipofika Wizarani kwa ajili ya  mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali katika eneo hilo.  
Ujumbe ulioambatana na Mhe. Perriello wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Mhe. Pirriello (hawapo pichani) akiwemo Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Mark Childress (kulia). 
Mhe. Perriello akizungumza huku Balozi Mulamula akimsikiliza
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (wa pili kulia) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo (kushoto)  wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Mhe. Perriello (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Bi. Grace Martin (wa pili kushoto), Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Bi. Shamim Khalfan (kulia), Afisa Mambo ya Nje. 
Mazungumzo yakiendelea
Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Mhe. Perriello na Balozi Mulamula (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Bi. Redemptor Tibaigana, Bw. Suleiman Saleh na Afisa aliyeambatana na Mhe. Perrielo
Balozi wa Marekani nchinui, Mhe. Childress (wa kwanza kushoto) akimtambulisha Mhe. Perriello (Katikati) kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Liberata Mulamula (kulia)
 Balozi Mulamula akiwa  akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Perriello mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao.


Picha na Reginald Philip.

Friday, August 21, 2015

Rais Kikwete amuapisha Balozi mpya wa Tanzania Nchini Zimbabwe.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akimuapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala katika hafla iliyofanyika tarehe 21-08-2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kabla ya Uteuzi huo, Luteni Jenerali Makakala, alikua Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Mabalozi na Maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na familia ya Balozi Mteule Makakala wakishuhudia kiapo.
 Rais Kikwete akimkabizi Balozi Makakala nyaraka na vitendea kazi mbalimbali kama muongozo wa kazi yake mpya ya Ubalozi.
 Familia ya Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala  wakishuhudia uapisho huo.

 Mheshimiwa Balozi Makakala akisaini kiapo hicho mbele ya Mheshimiwa Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala, muda mfupi baada ya kula kiapo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Mabalozi na Maofisa kutoka Wizara hiyo, pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe.  Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala, baada ya kiapo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Tarehe 21-08-2015.

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala.
Rais Kikwete akibadilishana mawazo na Balozi Mteule Makakala (kushoto kwa Rais) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
 Rais Kikwete akibadilishana mawazo na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala, muda mfupi baada ya kumuapisha kuwa Balozi.
 Rais Kikwete akibadilishana mawazo na Viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mabalozi na Maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, nao wakibadilishana mawazo mara baada ya hafla hiyo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (Kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na msemaji wa Wizara Bi Mindi Kasiga wakimpongeza Balozi Mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala, mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
=========================
PICHA NA REUBEN MCHOME.

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Mabalozi wa India na Denmark

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Denmark nchini Mhe. Einar Hebogard Jensen, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Tarehe 21-08-2015.

Balozi mpya wa Denmark hapa nchini Mhe. Einar Hebogard Jensen, akiwasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mnikulu Bw. George Bwando, anayeshuhudia (kushoto) ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Juma Maharage.

Mhe. Einar Hebogard akipokea heshima kutoka kwa Bendi ya Jeshi la Polisi (hawapo pichani), kwa kuimbiwa nyimbo za Taifa za Denmark na Tanzania.

Mhe. Balozi Hebogard akiweka saini kitabu cha wageni Ikulu Jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete.
Rais Kikwete akimpokea Balozi Hebogard baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), akisalimiana na Balozi mpya wa Denmark hapa Nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine, akisalimiana na Balozi Hebogard.

Rais Kikwete akizungumza na Balozi Hebogard mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho.

Picha ya Pamoja.
========
Balozi wa India

Msafara wa Balozi mpya wa India ukiingia katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, tayari kwa kuwasilisha hati za utambulisho kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Balozi mpya wa India Nchini, Mhe. Sandeep Arya, akipokea heshima kutoka kwa Bendi ya Jeshi la Polisi, kwa kuimbiwa Nyimbo za Taifa za India na Tanzania.
 Mhe. Sandeep Arya, akiweka saini kitabu cha wageni Ikulu Jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete.
 Rais Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Mheshimiwa Balozi Sandeep Arya.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), akisalimiana na Balozi mpya wa India hapa Nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki, akisalimiana na Balozi mpya wa India hapa Nchini Mhe. Sandeep Arya.
Mhe. Sandeep Arya, akiagana na Mnikulu tayari kwa kuondoka viwanja vya Ikulu, mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete.

Thursday, August 20, 2015

Matukio mbalimbali yaendelea kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwa pamoja na  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakichanganya saruji, kokoto na mchanga ili kupata zege kwa ajili ya kuweka Jiwe la  Msingi ikiwa ni uzinduzi wa kuanza kwa ujenzi wa vyoo 22 kwenye Shule ya Msingi Kiboriloni, Mkoani Kilimanjaro. Uzinduzi huo ni tukio mojawapo kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa  Ujenzi huo umedhaminiwa na UNDP. 
Bw. Alvaro akiweka jiwe la msingi  kuzindua kuanza kwa ujenzi wa  Vyoo hivyo
Balozi Mushy naye akiweka tofali katika msingi huo 
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Nathalia Kanem naye akimpatia fundi tofali la ujenzi wa vyoo hive
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza mbele) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,kwa pamoja wakimimina zege kwenye msingi wa Vyoo vinavyojengwa katika Shule ya Msingi ya Kiboriloni
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza katika uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 vinavyojengwa katika shule ya msingi ya Kiboriloni
Juu na Chini ni Balozi Mushy akizungumza na wanafunzi wakati wa Uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 katika Shule hiyo
Wanafunzi wa Shule hiyo wakionekana kuwa na furaha na matumaini baada ya uzinduzi wa Vyoo hivyo vya Shule yao.
Sehemu ya Uongozi wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni
Wananchini na waalimu wa shule hiyo wakisikiliza kwa makini 
Dkt. Kanem akizungumza kwenye uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 vya shule ya Msingi Kiboriloni
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Nathalia Kanem (kulia) akifurahia jambo na Balozi Mushy (katikati), pamoja na Bw. Alvarp
Balozi Mushy akimtambulisha Bwa. Alvaro kwa waalimu wa shule ya msingi ya kiboriloni waliojipang kumpokea  
Balozi Celestine Mushy akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Alvaro
Bwa. Alvaro (wa nne kutoka kulia) na Balozi Celestine Mushy wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi na waalimu wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni

Picha na Reginald Philip