Friday, January 26, 2018

Mhe. Hamad Rashid akutana na Naibu Waziri wa Kilimo wa China

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Mhe. Dkt. QU DONGYU walipokutana katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijijni Dar es Salaam tarehe 26 Januari, 2018 kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikino katika sekta ya kilimo na uvuvi kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na China.  Mhe. Dkt. QU DONGYU yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mazungumzo kati ya Mhe. Hamad Rashid na Mhe. Dkt. QU DONGYU yakiendelea huku wajumbe wa China na Tanzania wakifuatilia.
Mhe. Hamad Rashid na Dkt. QU kwa pamoja wakipitia baadhi ya nyaraka za ushirikiano


Picha ya pamoja kati ya Mhe. Hamad Rashid na Dkt. QU DONGYU pamoja na wajumbe wengine walioshiriki kikao hicho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki
Mhe. Hamad Rashid akiagana na Dkt. QU DONGYU mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Thursday, January 25, 2018

Naibu Waziri wa Kilimo wa China atembelea Tanzania


Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt.Charles Tizeba ( Katikati mwenye kipaza sauti), akiongoza mazungumzo wakati wa Mkutano na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Mhe. DK QU DONGYU(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) tarehe 25 Januari,2018. 
Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania China Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki ( wa kwanza kulia), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt.Thomas Kashilila, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (wa pili kutoka mwisho kushoto). 

Katika majadiliano hayo pande zote mbili zimekubaliana kuundwa kikosi kazi ambacho kitakuwa na kazi ya kuhakikisha maeneo waliyokubaliana kushirikiana yanatekelezwa, kikosi kazi hicho kitahusisha wataalam kutoka Tanzania na China. Baadhi ya maeneo ambayo China na Tanzania watashirikiana ili kuinua kilimo cha Tanzania ni; kuboresha miundombinu ya Kilimo kama vile Scheme za Umwagiliaji, ushirikiano kati ya chuo cha Kilimo cha Sokoine na vyuo vya kilimo vya China, kushirikiana katika tafiti mbalimbali, China kuwekeza katika viwanda vya kuongeza thamani katika mazao, masoko n.k. Mhe. DONGYU  anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 28, Januari,2018. 


Naibu Waziri wa Kilimo wa China Mhe. DK QU DONGYU ( wa tatu kulia mwenye kipaza sauti) akielezea jambo katika mazungumzo hayo, kushoto kwake ni balozi wa China nchini Mhe. Balozi Wang Ke na wengine ni ujumbe wa watalaam waliongozana na Mhe. Waziri DONGYU

  Waziri wa Kilimo kutoka China Mhe. DK QU DONGYU pamoja na ujumbe aliongozana nao wakifuatilia mazungumzo
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mkutano.

Tuesday, January 23, 2018

Timu Maalum ya ADB yatembelea Tanzania



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda (kulia) akiwa katika mazungumzo na Bw. Alieu Jeng- Mjumbe wa Timu kutoka Bank ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank), walipomtembelea Wizarani tarehe 22 Januari,2018
Timu hiyo yenye jumla ya wajumbe watatu ambao watakuwa nchini kwa lengo la kujadiliana na Serikali kuhusu maeneo ya vipaombele ambayo wanaweza kusaidia kupitia bajeti yao ya 2018/2019. wakiwa nchini watakutana na Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. Kwa mujibu wa wajumbe hao, bajeti hii itazingatia zaidi kusaidia Serikali kupitia maeneo  ya vipaombele yaliyoanishwa  ili kuwezesha Sekta binafsi kuweza kuchochea uchumi wa nchi kupitia biashara na Uwekezaji katika maeneo mbalimbali.  wajumbe hao waliwasili tarehe 14 Januari, 2018 na wanatarajiwa kuondoka tarehe 27 Januari,2018.


 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda (kulia), akiendelea na mazungumzo na wajumbe wa Timu kutoka ADB ambao ni Bw.Alieu Jeng(Kushoto), Bw. Frsncois Nkulikiyimfura anayefuata na mwisho kushoto ni Bi.Eline Okuozeto

Katibu Mkuu, timu ya ADB na Wataalam kutoka Wizarani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo




Monday, January 22, 2018

Israel kusaidia sekta ya afya nchini Tanzania


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Dkt. Otilia Flavian Gowelle akiwa katika mazungumzo na Naibu Balozi wa Israel nchini, Mhe. Michael Baruch Baror kabla ya wawili hao hawajasaini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya Afya kati ya Tanzania na Israel.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Dkt. Otilia Flavian Gowelle pamoja na Naibu Balozi wa Israel nchini, Mhe. Michael Baruch Baror wakiweka saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya Afya kati ya Tanzania na Israel. Makubaliano hayo yataanza kwa kuijengea uwezo hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma ambapo Israel itasaidia ujenzi wa Kitengo cha dharua na mifupa pamoja na ujenzi wa Kitengo cha kisasa cha wagonjwa mahututi (ICU).
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Dkt. Otilia Flavian Gowelle pamoja na Naibu Balozi wa Israel nchini, Mhe. Michael Baruch Baror wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha zoezi la uwekaji saini. Watatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda.

Balozi wa Zimbawe atembelea Wizara ya Mambo ya Nje


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba akisalimiana na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania anayemakiza muda wake, Mhe. Idzai Chimonyo ambaye alifika ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri kwa ajili ya kuaga.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania anayemakiza muda wake, Mhe. Idzai Chimonyo.
Mazungumzo yanaendelea

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania anayemaliza muda wake, Mhe. Idzai Chimonyo. Wengine katika picha ni Afisa Dawati wa Zimbabwe, Bibi Halima Abdallah na Afisa Ubalozi wa Zimbabwe, Bw. Martin Tavenyika.

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA COMORO


Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe, Sylvester Mabumba (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji wa Comoro, Bw. Said Mohamed Omar (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group pamoja na wajumbe waliofuatana nao katika ziara maalum ya kufungua na kuzitangaza fursa zilizopo Tanzania na Comoro.

================================================
WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA COMORO

Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba alipokea ujumbe wa Clouds Media Group uliowasili visiwani humo  tarehe tarehe 20 Januari 2017 kwa ziara maalumu ya siku tatu ikiwa na lengo la kushirikiana na Ubalozi kuzitangaza fursa mbalimbali zinazopatikana Visiwani humo kwa Watanzania.   

Ujumbe huo wa Clouds Media Group ukiongozwa na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Bw. Ruge Mutahaba uliwasili Comoro kufuatia mualiko wa Ubalozi wa Tanzania hapa Comoro ambapo lengo lake lilikuwa ni kuja kufanya tathamini ya kuzindua Jukwa la Fursa (FURSA EXPO) Visiwani Comoro kama sehemu ya kuendeleza kampeni za kuwapatia vijana wa Kitanzania taarifa muhimu kuhusiana na fursa za uwekezaji na biashara.

Ubalozi wa Tanzania Visiwani Comoro kwa kushirikiana na Ujumbe wa Clouds Media Group umelenga ifikapo mwezi Aprili 2018 kupanua mianya ya uwekezaji nchini Comoro pamoja na kuhakikisha kwamba masoko ya uhakika yanapatikana kwa ajili ya bidhaa za Tanzania hasa katika kipindi hiki ambapo Uchumi wa Tanzania unaelekea kuwa ni uchumi wa Viwanda.

Aidha, Mhe. Balozi akiwa ameambatana na ujumbe wa Clouds Media Group alipata fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo na wadau kutoka sekta mbalimbali za Serikali ya Comoro, Mashirika ya Umma na Sekta Binafsi. “Serikali ya Tanzania itaendelea kufungua maeneo mapya ya ushirikiano sambamba na kuhakikisha vijana wananufaika na ushirikiano baina ya nchi na nchi ulioanzishwa na mataifa yao” alisema Mhe. Balozi

Aidha, Mhe. Balozi alielezea anataraji ziara hiyo italeta matokeo chanya na kwamba kuzinduliwa kwa jukwaa la FURSA EXPO ni sehemu mojawapo ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ambayo inalenga kwenye Diplomasia ya Uchumi na kwamba kupitia jukwaa hilo bidhaa za Tanzania zinauhakika wa kuingia kwenye Soko la Comoro kwani nchi ya Comoro inaitegemea Tanzania kwa kiasi kikubwa katika mahitaji yake mbalimbali.

Pia ujumbe wa Clouds Media Group ulitumia nafasi hiyo kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Visiwani Comoro, Ndg. Said Mohamed Omar, Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Kitaifa ya Utalii, Ndg. Mouzamildine Youssouf pamoja na Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Vijana. Katika mazungumzo hayo, wajumbe walionesha nia ya kutaka kushirikiana kwa pamoja katika kuendesha kampeni itakayoibua maeneo muhimu ya kimkakati ambayo Vijana wa Kitanzania na wale wa KiComoro wanaweza kushirikiana.

Naye Bw. Ruge Mutahaba kwa upande wake alieleza kufurahishwa na fursa mbalimbali zinazopatikana Comoro na kuahidi kuendelea kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Visiwani hapa kuhakikisha kwamba FURSA EXPO Comoro inafanikiwa na kuleta matokeo chanya kwa lengo la kuinua uchumi wa vijana wa Kitanzania na wa KiComoro.



Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya comoro pamoja na Wajumbe kutoka clouds Media Group wakiwa katika mazungumzo ya pamoja  na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Comoro, Bw. Mouzamildine Youssouf.


Sunday, January 21, 2018

Mabalozi watano wawasilisha Nakala za Hati za Utambulisho


Balozi Mteule wa Ugiriki
Balozi Mteule wa Ugiriki nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Konstantinos Moatsos (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kabla ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho leo jijin Dar es Salaam.
Balozi Mteule wa Ugiriki nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Konstantinos Moatsos akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Ugiriki nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Konstantinos Moatsos. Mazungumzo yao yalijikita katika kuboresha ushirikiano kati ya Tanzania na Ugiriki hususan kwenye eneo la uwekezaji na biashara.



Balozi Mteule wa Mali

Balozi Mteule wa Mali nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Fafre Camara akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Mali nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Fafre Camara. Wawili hao walijadili namna nchi zao zitakavyoweza kushirikiana katika kutatua changamoto za pamoja kama vile ugaidi na imani kali.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Mali nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Fafre Camara. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Bw. Suleiman Salehe (kulia) na Afisa wa Ubalozi wa Mali.
Balozi Mteule wa Colombia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Colombia nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Elizabeth Taylor kabla ya zoezi la kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho
.
Balozi Mteule wa Colombia nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Elizabeth Taylor akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Colombia nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Elizabeth Taylor. Wawili hao walijadili namna nchi zao zitakavyoweza kushirikiana katika masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Colombia nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Elizabeth Taylor. Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) na Afisa wa Ubalozi wa Colombia.

 Balozi Mteule wa Argentina

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Argentina nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Martin Gomez Bustillo kabla ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.
Balozi Mteule wa Argentina nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya,  Mhe. Martin Gomez Bustillo akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Argentina nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Martin Gomez Bustillo. Wawili hao walijadili namna nchi zao zitakavyoweza kushirikiana katika masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Argentina nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Martin Gomez Bustillo. Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia).
 Balozi Mteule wa Ufilipino

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Ufilipino nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Uriel Norman Garibay kabla ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.

Balozi Mteule wa Ufilipino nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya,  Mhe. Uriel Norman Garibay akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ofisini kwake jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Ufilipino nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya,  Mhe. Uriel Norman Garibay. Wawili hao walijadili namna nchi zao zitakavyoweza kushirikiana katika masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Ufilipino nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya,  Mhe. Uriel Norman Garibay. Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bibi Justa Nyange (kulia) na Afisa wa Ubalozi wa Ufilipino.

Saturday, January 20, 2018

Wizara yawanoa Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Nne la Afrika Mashariki

   Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifungua Semina Elekezi kwa Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Nne la Afrika Mashariki iliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere tarehe 19-20 Januari, 2018.

Wajumbe wa Semina hiyo wakimsikiliza Mheshimiwa Dkt. Mahiga wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku mbili ya kuwaongezea uwezo Wabunge wa Tanzania watakaowakilisha nchi kwenye Bunge la Nne la Afrika Mashariki.

Dkt. Suzan Kolimba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwatambulisha baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo kwa Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Afrika Mashariki wakati wa Semina elekezi iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya Wabunge hao. 

   Waheshimiwa Dkt. Mahiga na Dkt. Kolimba kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Nne la Afrika Mashariki. Kulia kwa Waziri Mahiga ni Mwenyekiti wa Wabunge hao Mhe. Dkt. Abdullah Makame. Wengine waliosimama kutoka kushoto ni Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, Mhe. Happiness Lugiko, Mhe. Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa, Mhe. Pamela Maasay na Mhe. Adam Kimbisa.

Waheshimiwa Dkt. Mahiga na Dkt. Kolimba kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Nne la Afrika Mashariki kwenye Semina elekezi iliyoandaliwa na Wizara kwa lengo la kuwaongezea uzoefu Wabunge hao. 

Mheshimiwa Adam Kimbisa akisalimiana na Mheshimiwa Dkt. Mahiga wakati wa Semina hiyo ya siku mbili iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere tarehe 19-20 Januari, 2018. 

Mheshimiwa Pamela Maasay akijitambulisha wakati wa Semina elekezi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki. 


Mheshimiwa Dkt. Ngwaru Maghembe akijitambulisha wakati wa Semina elekezi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akijitambulisha wakati wa Semina elekezi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Wengine kwenye picha waliokaa kuanzia kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara Kuu ya Usalama wa Taifa  Dkt. Modestus Kapilimba, Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa Wizara na Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara.


Mheshimiwa Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa akijitambulisha wakati wa Semina elekezi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki



Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlowola akitoa mada kuhusu mapambano ya rushwa wakati wa Semina elekezi kwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Kabla ya mada hiyo Mkurugenzi Dkt. Kapilimba wa Idara Kuu ya Usalama wwa Mataifa alitoa mada kuhusu uzalendo na usalama wa nchi.

Mheshimiwa Adam Kimbisa akichangia hoja kuhusu mapambano ya rushwa nchini iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola wakati  wa Semina elekezi kwa Wabunge wa Afrika Mashariki iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Dkt. Benard Achiula, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia akiwasilisha mada kuhusu itifaki na diplomasia wakati wa Semina hiyo. Pichani Dkt. Achiula akiwa na sahani na vyombo vya kulia chakula akionesha mfano wa kula kwenye dhifa za kitaifa. Mada hiyo iliambatana pia na andiko kuhusu Diplomasia ya Uchumi ambao ndio mwelekeo wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania. 

Jaji (Mstaafu) Harold Nsekela, Kamishna wa Maadili, Ofisi ya Rais - Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  akitoa mada kuhusu maadili ya Mbunge wa Afrika Mashariki na Taswira ya Nchi katika uwakilishi wa Taifa.

Dkt. Maduka Kessy, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango akitoa mada kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mipango mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo ya kimkakati katika Mtangamano wa Afrika Mashariki.

Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Wizara akichangia mada wakati wa Semina Elekezi ya Wabunge wa Bunge la nne  la Afrika Mashariki.