Saturday, May 5, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje imejipanga kutekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kutimiza malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Kauli hiyo ilitolewa leo jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.)  wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Waziri Mahiga alieleza kuwa Wizara inatakiwa kuweka Sera na mikakati ya utekelezaji kwa kuzingatia miongozo na maelekezo ya Viongozi wa juu akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
“Sera ya Serikali ya awamu ya tano ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, hivyo Sera yetu ya Mambo ya Nje lazima ijikite katika diplomasia ya uchumi wa viwanda”. Dkt. Mahiga alieleza.
 Dkt. Mahiga alihitimisha hotuba yake kwa kuwataka watumishi kuhakikisha kuwa Wizara inatekeleza majukumu yake kwa kujiwekea ratiba ya kuyakamilisha kwa kuzingatia hotuba za Mhe. Rais Magufuli  alizozitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao cha Mabalozi na Mhe. Rais Magufuli na kikao cha watumishi wa Wizara na   Mhe. Rais Magufuli. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda amesema  kuwa Wizara yake imejipanga ipasavyo  kuhakikisha kwamba jukumu la kuchochea uchumi wa nchi kupitia Sera ya Mambo ya Nje inayojikita katika  diplomasia ya uchumi inatekelezwa kikamilifu.
Prof. Mkenda alisema Wizara kwa kushirikiana na ofisi zake za Ubalozi, licha ya changamoto mbalimbali inazokutana nazo, lakini imekuwa ikitafuta fursa za uwekezaji, mitaji, masoko, utalii na elimu na kuzileta nchini ili kufikia azma ya Serikali ya awamu ya tano  inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020.

Alizitaja Balozi chache zilizoleta wafanyabiashara wakubwa kwa ajili ya kutafuta fursa za uwekezaji nchini kuwa  ni pamoja na Balozi za Tanzania nchini China, Ufaransa, Korea Kusini, Kenya, Ujerumani na Israel. "Balozi wetu China, Mhe. Mbelwa Kairuki
ametafuta taasisi za kifedha kwa ajili ya kuzikopesha benki za Tanzania ili zikuze mitaji ya kutoa mikopo kwa wawekezaji. Aidha, Serikali ya Ujerumani imefungua ofisi maalum kwa ajili ya kuratibu na kusaidia shughuli za kibiashara na uwekezaji hapa nchini" Prof. Mkenda alisema.

Prof. Mkenda alisifu jitihada zilizofanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya hivi karibuni za kuandaa maonesho ya bidhaa za viwanda vya hapa nchini yaliyofanyika jijini Nairobi tarehe 25 - 28 Aprili 2018. Alisema maonesho hayo ya kipekee yalikuwa na mafanikio makubwa ambapo wafanyabiashara walioshiriki waliingia makubaliano na wafanyabiashara wa Kenya ya kupeleka bidhaa zao nchini Kenya.
"Tunatakiwa tuondoe vikwazo vya kufanya biashsra, kuondoa vikwazo hivyo haina maana Tanzania iwe gulio la kuuzia bidhaa kutoka nje, bali wafanyabiashara wetu wanatakiwa kuchangamkia masoko ya nje ili wauze bidhaa zao kwa wingi nje ya nchi", Katibu Mkuu alisisitiza.
Katibu Mkuu alisema ili watumishi waweze kutimiza malengo ya Wizara yakiwemo ya kuvutia wawekezaji kutoka nje, Wizara imejipanga kuwawezesha watumishi kupata elimu, ujuzi, teknolojia na uzoefu unaohitajika kutimiza majukumu hayo.
Kuhusu suala la kupeleka watumishi kwenye vituo vya Ubalozi, Katibu Mkuu alieleza kuwa Wizara itatekeleza jukumu hilo kwa haki kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa ambavyo ni weledi, ujuzi na mahitaji ya Balozi husika. “Wizara haitapeleka watumishi vituoni kutokana na shinikizo au kuangalia sura, kabila na dini ya mtu ili kuondoa malalamiko yaliyokuwepo kwa muda mrefu Wizarani.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
 05 Mei, 2018

Ziara ya Waziri Heiko Maas Jijini Arusha


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Heiko Maas akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tayari kwa kuendelea na ziara yake katika mkoa wa Arusha, ambapo amekutana na viongozi wa Mahakama ya Kesi ya Masalaia za Mauaji ya Kimbari (United Nations Mechanism for International Criminal Tribiunals-MICT) na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (African Court on Human and Peoples' Rights). Pia ametembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Mhe. Maas akiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Bw. Jestas Nyamanga (mwenye tai ya Njano) mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro.
Mhe. Maas (kulia) akisalimiana na Afisa mahusiano wa Mahakama ya Kesi ya Masalaia za Mauaji ya Kimbari Bw. Ousman Njikam, mara baada ya kuwasili katika mahakama hiyo.
Bw. Njikam akimtambulisha Msajili Mkuu wa Mahakama ya Kesi ya Masalaia za Mauaji ya Kimbari (United Nations Mechanism for International Criminal Tribiunals-MICT) Bi. Sera Attika kwa Waziri Haeko Maas
Waziri Maas. akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kilichoandaliwa kwenye mahakama hiyo.
Bw. Njikam akielezea namna mahakama hiyo inavyofanya kazi kwa Waziri Maas, wa kwanza kulia ni Bi. Attika na wapili kutoka kushoto ni Afisa mwandamizi wa mahakama hiyo Bi. Thembile Segoete wakisikiliza kwa makini.
Bi. Attika akimwelezea jambo Mhe. Maas
Waziri Haeko Maas, pamoja na Bw. Nyamanga wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mahakama ya Kesi ya Masalaia za Mauaji ya Kimbari.
Rais wa Mahakama ya Haki za Binadamu na watu Mhe. Jaji Sylvain Ore (wa kwanza kulia) akiongozana na Waziri wa Ujerumani Mhe. Haeko Maasi mara baada ya kuwasili kwenye Mahakama hiyo tayari kwakufanya mazungumzo, mazungumzo hayo yameudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Jestas Nyamanga. Makao Makuu ya Mahakama hiyo yapo jijini Arusha.
Waziri Haeko Maasi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Libérat Mfumukeko walipokutana na kufanya mazungumzo. 
Mhe. Haeko Maas akizungumza na Majaji wa mahakama hiyo (hawapo pichani)
Sehemu ya Majaji wa Mahakama hiyo wakimsikiliza kwa makini Mhe. Maas (hayupo pichani)
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Bw. Jestas Nyamanga akifuatilia kwa mikini mazungumzo hayo kati ya Jaji Sylvain Ore (hawapo pichani)
Jaji Ore akimkabidhi Mhe. Maas zawadi ya Nembo ya Mahakama hiyo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Waziri Haeko Maasi pamoja na Jaji Sylvain Ore wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama pia na ujumbe ulioambatana na Mhe. Maas.
Waziri Haeko Maasi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Libérat Mfumukeko walipokutana na kufanya mazungumzo. 

Mhe. Maas pamoja na Dkt. Mfumukeko wakiwa kwenye mazungumzo

Mazungumzo yakiendelea.
Dkt Libérat Mfumukeko (wa nne kutoka kulia), Waziri Haeko Maas (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja

























Balozi Dkt. Dau ashiriki kujadili zao la nazi nchini indonesia.

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Thailand, Philippines, Cambodia, Brunei, Laos pamoja na Indonesia Dkt. Ramadhani Kitwana Dau, leo akichangia mada  kwenye Kongamano la Kitaifa kujadili zao la nazi kwenye mji wa Gorontalo Indonesia 
Kongamano likiendelea
Mhe Dau amefanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Indonesi Dkt. Amran Sulaiman, katika mazungumzo yao yaliyojikita katika kushirikiana na kukuza sekta ya kilimo baina ya Tanzania na Indonesia.

********************* 

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Thailand, Philippines, Cambodia, Brunei, Laos pamoja na Indonesia Mhe Dkt Ramadhani Kitwana Dau, leo ameshiriki  katika Kongamano la Kitaifa kujadili zao la nazi kwenye mji wa Gorontalo Indonesia .
Balozi Dau alishiriki kwenye mjadala huo (panellist) kwa kutoa historia ya zao la nazi Tanzania ikiwemo uzalishaji na changamoto zake. Mkutano huo wa siku 2 umeanza leo na unashirikisha Wadau wote wa zao la nazi nchini Indonesia. Indonesia inaongoza katika uzalishaji wa nazi Duniani kwa kulima hekta 3.6 milioni na kuzalisha nazi zaidi ya tani 17 milioni. Kwa upande wake, Tanzania inaongoza kwa zao hilo Barani Afrika lakini inalima hekta 350,000. 
Zao la nazi kwa sasa linaongoza kwa bei kwenye soko la Dunia na kulipita zao la chikichi na hata mafuta ya Petroli . Nchini Indonesia mnazi mmoja unatoa kati ya nazi 100 hadi 150 ingawa wastani wa kitaifa Ni nazi 70 kwa mnazi mmoja. 

Aidha katika mkutano huo Balozi Dau alipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Kilimo wa Indonesia Mhe Dr Amran Sulaiman ambapo walikubaliana kukuza zaidi ushirikiano kwenye kilimo baina ya nchi hizi mbili. 

Pamoja na zao la nazi, Indonesia inaongoza Duniani kwenye mazao  kadhaa yakiwemo muhogo, Mahindi ya njano. 
Balozi Dau anatarajia kukutana na wawekezaji wa sukari michikichi na mihogo kwa madhumuni ya kuwashawishi kuja kuwekeza Tanzania .


Friday, May 4, 2018

Waziri Mahiga afungua Baraza la Wafanyakazi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Mei, 2018
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakimsikiliza Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Baraza nao wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Mahiga ambaye hayupo pichani
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Susan Kolimba nae akitoa mchango wake kwa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Wajumbe wa Baraza wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri (hayupo pichani)
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza wakiwa kwenye mkutano
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda nae akisisitiza jambo kwa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani)
Wajumbe wakimsikiliza Prof. Mkenda (hayupo pichani)
Wajumbe wengine nao wakiwa makini kufuatilia hatuba ya Prof. Mkenda (hayupo pichani)
Mhe. Waziri Mahiga akimzawadia Mfanyakazi Hodari wa Wizara, Bw. Juma Kigwa wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Bw. Kigwa aliibuka mshindi wa jumla wa Wizara kati ya wafanyakazi bora waliochaguliwa kutoka katika kila Idara na Vitengo.
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi cheti Bibi Lilian Mushi ambaye ni mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Masjala
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi cheti Bw. Erick Ngilangwa ambaye ni mfanyakazi bora kutoka Idara ya Afrika

Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi cheti Bw. Suleiman Magoma ambaye ni mfanyakazi bora kutoka Idara ya Diaspora
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi cheti Bw. Hangi Mgaka ambaye ni mfanyakazi bora kutoka Idara ya Mashariki ya Kati
Meza kuu
 Mhe. Waziri, Mhe. Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi.
 Mhe. Waziri, Mhe. Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Mfanyakazi Hodari wa Wizara Bw. Juma Kigwa(wa tatu kutoka kulia)
 Mhe. Waziri, Mhe. Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.
Mhe. Waziri, Mhe. Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi bora wa Wizara

Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki wafikia tamati jijini Arusha

Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la masuala ya Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki umehitimishwa  leo tarehe 04 Aprili, 2018 jijini Arusha.

Mkutano huu uliofanyika kuanzia Aprili 28 hadi Mei 5, 2018, kabla ya kuhitimishwa ulitanguliwa na mikutano ngazi ya Wataalamu, ngazi ya Makatibu Wakuu, na hatimaye Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta.

Pamoja na mambo mengine lengo la Mkutano huu lilikuwa ni kufanya mambo yafuatayo:-
kupokea na kujadili taarifa ya hali ya utekelezaji wa maamuzi yaliyofanywa na Mkutano uliopita wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi;
Kupokea na kupitia taarifa ya Kamati ya Takwimu;
Kupokea na kujadili taarifa ya Kikosi kazi cha kuandaa muswada wa kuanzishwa kwa taasisi za Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Masuala ya Fedha; na
Kujadili taarifa ya mapendekezo ya utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, Mkutano huu umefanikiwa kupata ufumbuzi wa masuala kadhaa ya kichumi na fedha ambayo yanalenga kuboresha na kurahisisha mazingira ya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Dkt. Philip Mpango Waziri wa Fedha na Mipango akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hotel ya Four Points jijini Arusha.

Mkutano ukiwa unaendelea

Mhe.Dkt. Mpango akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hotel ya Four Points jijini Arusha
Bibi Judica Omari (kushoto) Kamishna Msaidizi wa Ushirikiano wa Kikanda, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Tanzania akizumgumza wakati Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi ngazi ya Wataalamu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji Bw. Bernard Haule kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Sehemu ya wajumbe wakifuatilia Mkutano