Thursday, October 18, 2018

Waziri Mahiga ziarani nchini India.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.),  akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Mhe. Sushma Swaraj walipokutana katika Mkutano wa 9 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India Ngazi ya Mawaziri Uliofanyika mjini New Delhi, katika Mkutano huo uliotanguliwa na Mkutano wa Ngazi ya wataalamu wakiongozwa na Makatibu Wakuu Tarehe 15 na Tarehe 16 Octoba Ngazi ya Mawaziri. 

Pia katika Mkutano huo Serikali ya Tanzania na India ziliwekeana saini kwenye mikataba miwili, ukiwepo Mkataba wa Makubaliano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na India kwaajili ya kubadilishana uzoefu na kuwaandaa wanadiplomasia bora watakao weza kutekeleza diplomasia ya Uchumi na Mkataba wa makubaliano kati ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda (TIRDO) na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya India (NRDC).

Aidha, Ujumbe wa Tanzania Uliongozwa na Mhe. Dkt. Mahiga, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa, Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bi. Justa Nyange, na viongozi kutoka kwenye Taasisi.

Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Mhe. Sushma Swaraj mara baada ya kumalizika kwa Mkutano 
Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri Ukiendelea mjini New Delhi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) pamoja na Mhe. Swaraj wakiwekeana saini makubaliano ya mkutano wa 9 wa tume ya pamoja ya kudumu kati ya India na Tanzania mara baada ya kumalizika kwa majidiliano ya mkutano huo kwa Ngazi ya Mawaziri
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi Muombwa kwa niaba ya Chuo cha Diplomasia Tanzania wakiwekeana Saini na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia India Bw. Shri J.S. Mukul, kwenye Mkataba wa Makubaliano ya pamoja Kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Chuo cha Diplomasia India. Lengo la Mkatabao huo ni kubadilishana uzoefu na kuwaandaa wanadiplomasia bora watakao weza kutekeleza diplomasia ya Uchumi kati ya taasisi hizi mbili. 




Dkt. Mahiga akutana na Mkurugenzi wa Chuo cha Ulinzi na Usalama New Delhi, India.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Ulinzi na Usalama nchini India Kapt. Guroreet S. Khurana (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Ulinzi na Usalama,  jijini New Delhi, India. Dkt. Mahiga alifanya mazungumzo na Kapt Khurana, katika mazungumzo yao yaliyojikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India, mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda (Hayupo pichani).
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Ulinzi na Usalama India, Kapt. Sarabjeet S Parmar
Mazungumzo yakiendelea.



Dkt. Ndumbaro Akutana na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Naibu Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akisalimiana na Mkuu Kitengo cha Fedha na Uhasibu cha Wizara hiyo Bw. Paul Kabale  leo kabla ya kukutana na baadhi wa viongozi wa Wizara hiyo katika Ofisi zake zilizopo Mtaa wa Makole Jengo la LAPF jijini Dodoma na aliyesimama pembeni ni Bw. Mapesi Manyama  Mkurugenzi Kitengo cha Ununuzi na Ugavi.

Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro (Mb) akisalimiana na Bw. Japhary Kachenje Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mhe. Dkt. Ndumbaro (Mb.) akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Diaspora cha Wizara hiyo Balozi Anisa Mbega akichukua maelezo yaliyotolewa na Naibu Waziri.

Aidha baadhi ya Wakuu wa Idara na Kitengo wakimsikila Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro (Mb), wa kwanza kulia  Bw. Japhary Kachenje  Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, wa pili Bi. Savera Kazauru Mkurugenzi Msaidizi  Utawala na Rasilimali Watu na wa tatu  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Marekani na Ulaya Bw. Jestus Nyamanga.

Baadhi ya Wakuu wa  Vitengo vya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro, wa kwanza kushoto Bw.  Mapesi Mnyama Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa pili Bw.  Paul Kabale Mkuu wa Kitengo Fedha na Uhasibu na wa tatu Balozi Anisa Mbega Mkuu wa Kitengo cha Diaspora.


Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa pamoja na Mhe. Dkt. Ndumbaro (Mb) Naibu Waziri wa Wizara hiyo baada ya kumaliza mazungumzo yao.