Monday, November 30, 2020
PROF. KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA, FINLAND NA SWEDEN
Saturday, November 28, 2020
UBALOZI WA TANZANIA AFRIKA KUSINI WAPEWA CHANGAMOTO YA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI, SIASA
Na Nelson Kessy, Pretoria
Ubalozi
wa Tanzania nchini Afrika Kusini wapewa changamoto ya kuhakikisha kuwa
unatekeleza Diplomasia ya Uchumi pamoja na Diplomasia ya Siasa iliyopo ndani ya
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM (2020-2025).
Changamoto
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge wakati alipotembelea
Ubalozi huo jijini Pretoria nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujionea utendaji
kazi wa Ubalozi na mali za Serikali nchini humo.
Balozi
Ibuge ameutaka Ubalozi huo kuhakikisha kuwa unatekeleza diplomasia ya uchumi
pamoja na diplomasia ya siasa kwa weledi ili kuleta manufaa ya Taifa.
"Nawapongeza
kwa utendaji kazi wenu na nawasihi muendelee kujituma katika kazi (proactive)
katika kuwapata wawekezaji na kutengeneza kuwa ni sehemu ya mfumo wa kuleta
mabadiliko ambayo Serikali imeyapanga kupitia Ilani ya CCM ya 2020-2025,"
Amesema Balozi Ibuge.
Balozi
Ibuge pia alipongeza utendaji wa Ubalozi huo ambao pamoja na Afrika Kusini
unaiwakilisha Tanzania katika Ufalme wa Lesotho, Jamhuri ya Botswana, Jamhuri
ya Namibia na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Kadhalika Balozi
Ibuge alipokea changamoto mbalimbali zinazoikumba Ubalozi huo na Kuahidi
kuzifanyia kazi ili kuongeza tija na ufanisi wa Ubalozi.
Kwa
upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence
Milanzi amemueleza Balozi Ibuge mafaniko mbalimbali ya Ubalozi katika
kutekeleza diplomasia ya uchumi na siasa nchini Afrika Kusini.
Moja
kati ya mafanikio hayo ni pamoja na kuenezwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo
Serikali ya Tanzania na ya Afrika Kusini zinatarajia kusaini mkataba wa
kutumika lugha ya Kiswahili kama katika shule za Afrika Kusini mwezi wa Machi
2021.
"Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Afrika Kusini
tutasaini mkataba wa kutumika kwa lugha ya Kiswahili katika shule za Afrika
Kusini mwezi wa Machi 2021," Amesema Balozi Milanzi.
Pamoja
na mambo mengine Balozi Milanzi ameahidi kusimamia sera ya Diplomasia ya uchumi
pamoja na Diplomasia ya siasa kwa kuhakikisha kuwa ubalozi utaendelea
kuwasiliana na wawekezaji mbalimbali wa kuwekeza nchini Tanzania katika sekta
za Biashara, Madini na Mawasiliano.
Balozi
wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akiwatambulisha baadhi ya wafanyakazi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ibuge wakati alipowasili Ubalozini
leo tarehe 27 Novemba 2020
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisaini kitabu cha wageni katika Ubalozi wa
Tanzania Nchini Afrika Kusini leo tarehe 27 Novemba 2020
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisisitiza jambo kwa watumishi (hawapo
pichani) wakati wa mkutano
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akiendesha kikao na wafanyakazi wa Ubalozi
wa Tanzania nchini Afrika Kusini
Balozi
wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akimuonesha
baadhi ya mali Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi wakati alipokuwa anakagua mali za Serikali Ubalozini
Friday, November 27, 2020
SADC-TROIKA, UN KUBORESHA MFUMO WA USALAMA NDANI YA DRC
Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) zimekubaliana kuboresha mfumo utakao weka ulinzi bora na usalama ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Akithibitisha
kuhusu mashirikiano ya mfumo wa kuimarisha ulinzi na usalama nchini DRC, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amemuwakilisha
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika
mkutano huo amesema kuwa kamati ya utatu inayoshughulika na usalama ndani ya
jumuiya ya SADC imekutana kwa dharura ili kuweza kuangalia namna ya kukabiliana
na matishio ya ugaidi yanayotishia sana hali ya amani na usalama katika nchi
zilizopo ukanda wa SADC ikiwemo Msumbiji, Congo DRC na Tanzania.
Mkutano
huo wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa,
Ulinzi na Usalama ya SADC, nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya
Umoja wa Mataifa kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji
umefanyika leo Tarehe 27, Novemba 2020 mjini Gaborone, Botswana ambapo
pamoja na mambo mengine umeangalia masuala mbalimbali yanayohusu amani, ulinzi
na Usalama ndani ya SADC.
"Tumeangalia
kwa undani mapendekezo mapya ya mfumo wa ulinzi katika enao la DRC ambapo nchi
tatu zinazoshiriki katika kuimarisha Ulinzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo ambapo nchi tatu zinashiriki kuimarisha ulinzi na usalama nchini DRC
(Tanzania, Malawi na Afrika Kusini) kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa
zitaendelea kuimarisha masuala ya amani, Ulinzi na usalama Nchini DRC kwa
kutumia mfumo mpya utakao weka ulinzi bora na amani nchini DRC," Amesema
Mama Samia Suluhu Hassan.
Ameongeza
kuwa, kupitia mkutano huo pia limejadiliwa suala la hali halisi ya usalama
ndani ya nchi wanachama ndani ya SADC na kuona jinsi ya kutumia usalama wetu
kwa ajili ya kujenga uchumi wa ukanda wetu wa kusini mwa Afrika
Kwa
upande wake Rais wa Botswana, Dkt. Mokgweetsi Masisi ambae pia alikuwa
Mwenyekiti wa Mkutano huo amezipongeza nchi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania pamoja na Visiwa vya Shelisheli kwa kufanya chaguzi ambazo zilikuwa
huru, haki na amani na kuzitaka nchi nyingine kuiga mfano huo wa kuwa na
demokrisia ya uhuru, amani na haki.
"Matokeo
ya chaguzi hizo ni mfano mzuri kwetu sisi kama nchi wanachama wa SADC kujifunza
mfano kutoka kwa wenzetu," Amesema Dkt. Masisi.
Dkt.
Masisi ameongeza kuwa pamoja kufanya chaguzi huru haki na za amani, kuna mambo
ambayo yamekuwa yakijitokeza katika ukanda wa SADC kama vile, Ugaidi, uhalifu
wa kimtandao na vikundi vya waasi jambo ambalo limepelekea wakuu wan chi na
serikali kukutana hapa (Botswana) na kujadili namna ya kukabiliana na
changamoto hizo kwa kuwa changamoto hizi siyo za nchi moja moja bali na
kuzitaka nchi zote kuungana na kukabiliana na vikundi hivyo vya kigaidi.
"Mtakumbuka
kuwa katika mkutano wetu wa SADC uliofanyika mwezi wa nane mwaka huu tulitoa
ripoti iliyoonesha kuwa na baadhi ya ugaidi kwa baadhi ya nchi zetu za SADC,
pamoja na ripoti kuonyesha kuwa kuna hali ambayo siyo shwari kwa baadhi ya nchi
wananchama, kuna haja ya kuungana pamoja na kuhakikisha kuwa vikundi hivi vya
kigaidi vinatokomezwa katika ukanda wetu wa SADC," Amesema Dkt. Masisi.
"Ni
jukumu letu sote kuipa ushirikiano Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo hasa upande
wa Mashariki mwa DRC na kuhakikisha kuwa amani ya nchi hiyo inalindwa kwa
kutokomezwa kwa vikundi vya kigaidi vinavyochangia kutoweka kwa amani nchini
humo, na ndiyo maana leo tumekutana hapa ili tuweze kuona na jinsi gani ya
kumsaidia mwenzetu DRC," Ameongeza Dkt. Masisi
Pamoja
na mambo mengine, Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama inawajibika kukuza amani na usalama katika
eneo la SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo
kuhusu mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama.
Ni
mara ya kwanza kwa Wakuu wan chi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC - TROIKA) kukutana ana kwa ana tangu ulipotokea ugonjwa wa Homa
Kali ya Mapafu (Covid-19).
Mkutano
huo ulihudhuriwa na, Rais wa Botswana Mhe. Dkt. Mokgweetsi Masisi, Rais wa
Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril
Ramaphosa, Rais wa Malawi Mhe. Lazarus Chikwera, Rais wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Felix Tshisekedi, Makamu wa Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya
Msumbiji Bw. Jaime Neto aliyemuwakilisha Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano
wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na
amani vya Umoja wa Mataifa kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji uliofanyika leo Tarehe 27, Novemba 2020,
mjini Gaborone Botswana
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano
wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na
amani vya Umoja wa Mataifa kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji uliofanyika leo Tarehe 27, Novemba 2020,
mjini Gaborone Botswana
Thursday, November 26, 2020
MAWAZIRI SADC - TROIKA WAKUTANA KWA DHARURA BOTSWANA
Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama wakutana katika mkutano wa dharura na kujadili masuala ya siasa, ulinzi na usalama.
Mkutano huo umefanyika leo mjini Gaborone,
Botswana ambapo ulitanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya
Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ulioanza asubuhi na kumalizika mchana.
Kupitia mkutano huo, mawaziri wameweza
kujadili masuala ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC na kupendekeza
njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwenye siasa,
ulinzi na usalama ndani ya ukanda wa SADC.
Pamoja na mambo mengine, Asasi ya SADC ya Ushirikiano
wa Siasa, Ulinzi na Usalama inawajibika kukuza
amani na usalama katika eneo la SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia
nchi Wanachama mwongozo kuhusu mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na
usalama.
Ujumbe
wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
ukiwa ukiimba wimbo wa SADC kabla ya kuanza kwa mkutano wa dharura wa baraza la
Mawaziri
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana Dkt. Lemogang Kwape akifungua
mkutano wa Dharura wa baraza la mawaziri, kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa SADC,
Dkt. Stegomena Taxi Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama
wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stegomena Taxi mara
baada ya kumaliza mkutano wao
MAKATIBU WAKUU SADC - TROIKA WAKUTANA KUJADILI SIASA NA USALAMA
Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA wamekutana na kujadiliana Mambo mbalimbali
yakiwemo masuala ya hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani ya SADC mjini
Gaborone, Botswana.
Awali, Mkutano wa Makatibu Wakuu ulifunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Bw. Gaeimelwe Goitsemang ambae pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) kukutana ana kwa ana tangu ulipotokea ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (Covid-19).
Kwa upande wa Makatibu wakuu waliohudhuria katika Mkutano huo kutoka Tanzania ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.
Mkutano wa Makatibu Wakuu utafuatiwa na Mkutano wa Dharua wa Baraza la
Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama baadae
mjini Gaborone.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ukifuatilia Mkutano wa
Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA uliofanyika mjini Gaborone, Botswana
Mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA ukiendelea Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ngazi ya Makatibu Wakuu ukifuatilia mkutano
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiwasilisha mada katika Mkutano wa Makatibu
Wakuu wa Asasi ya SADC ya ushirikiano katika siasa, ulinzi na Usalama unaondelea
Mjini Gaborone, Botswana
VACANCY ANNOUNCEMENT
Wednesday, November 25, 2020
Mama Samia kumwakilisha JPM Mkutano wa SADC Organ Troika
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi
Na Nelson Kessy, Gaborone-Botswana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa dharura wa pamoja baina ya SADC Organ Troika (Botswana, Malawi
na Zimbabwe), na nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa
Mataifa, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenye Kikosi cha
Umoja wa Mataifa nchini DRC utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2020, mjini
Gaborone, Botswana.
Akithibitisha kuhusu
ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa ujumbe wa
Tanzania kwenye mkutano huo utaongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa anamwakilisha Mhe. Rais.
Kwa mujibu wa Prof. Kabudi, mkutano huu utatanguliwa
na mkutano wa Maafisa Waandamizi/Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano
wa Siasa, Ulinzi na Usalama na kufuatiwa na mkutano wa Dharura wa Kamati ya
Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 26 Novemba 2020.
"Pamoja na Mambo
mengine, mkutano huo utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya
SADC na kuweza kuona changamoto mbalimbali zilizojitokeza na kupata majibu ya
kutatua changamoto hizo," Amesema Prof.
Kabudi
Makamu
wa Rais ataambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu
Wizara ya Ulinzi Dkt. Faraji Mnyepe pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya
Ushirikiano wa Kikanda na Mratibu Kitaifa wa Masuala ya SADC, Bibi Agnes
Kayola.
ASASI
ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) inawajibika kukuza amani na usalama katika eneo la
SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo kuhusu
mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama.
Tuesday, November 24, 2020
TANZANIA YAITHIBITISHIA JUMUIYA YA KIMTAIFA KUENDELEA KULINDA AMANI AFRIKA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeihibitishia jumuiya ya kimataifa kuwa itaendelea kutoa vikosi vya kulinda amani na ulinzi katika nchi za bara la Afrika.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati alipokuwa katika mkutano wa kunzindua
kikosi kazi cha kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa juu ya wanawake, amani na
usalama jijini Dar es Salaam.
Prof.
Kabudi amesema kuwa serikali ya Tanzania ipo tayari kufanya kazi kwa
kushirikiana na Shirika la Mwalimu Nyerere na Shirika la Umoja wa Mataifa
pamoja na mashirika mengine duniani katika kuhakikisha kuwa amani ulinzi na
usalama vinapatikana.
"Tanzania
imekuwa ni nchi mojawapo inayotoa askari wanaokwenda kulinda amani katika
mataifa mbalimbali katika bara la Afrika ambapo baadhi yake ni Sudani, Congo
DRC, Lebanon na Afrika ya Kati……… kwa hiyo lengo la mpango kazi huu ni
kuwezasha Serikali ya Tanzania kuboresha ushiriki wa askari wa kike katika
masuala ya ulinzi na amani," Amesema Prof. kabudi
Aidha,
Prof. Kabudi ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kutoa askari wa kulinda amani
katika mataifa mbalimbali barani afrika kwani suala la amani katika jamii ni
jambo muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa lolote lile Duniani.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku,
amesema kuwa Taasisi anayoiongoza iko tayari kufanya kazi kwa karibu na jumuiya
ya kimataifa na washirika wote wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa amani na
utu wa mwanamke unalindwa na kuheshimiwa katika jamii.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo pia ulihudhuriwa na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, akiwemo Balozi wa Norway, Mhe. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu, mhe. Khalifa Abdulrahman Mohammed Ali-Marzouki, Balozi wa Canada Mhe. Pamela O'Donnell pamoja Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Zlatan Milišić.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
Sunday, November 22, 2020
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA SADC WA TROIKA MBILI NA WASHIRIKA WA MAENDELEO
Saturday, November 21, 2020
PROF. KABUDI: TUTASHIRIKIANA NA TAIFA LOLOTE LINALOIHESHIMU TANZANIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)akimkabidhi nyaraka Mkurugenzi wa
Kitengo cha Diaspora Balozi, Anisa Mbega |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)akimkabidhi nyaraka Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Bibi. Caroline Chipeta |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)akiongea na Watumishi wa
wizara katika mkutano uliofanyika jijini
Dodoma |