Thursday, March 25, 2021

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AONGOZA WAKAZI WA GEITA NA MIKOA JIRANI KUMUAGA JPM

 Na Mwandishi Wetu, Geita

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amewaongoza wakazi wa Geita na mikoa jirani kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita.

 

Akizungumza katika shughuli hiyo ya kuuaga mwili wa hayati Magufuli Wilayani Chato, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya mazishi kitaifa amewasihi Watanzania kuendelea kushikamana katika kulijenga taifa, ambalo Magufuli ameliacha salama na lenye heshima.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, amesema ni wajibu wa viongozi na Watanzania kuungana kuenzi mazuri yote aliyofanya Hayati Magufuli na kuendeleza sera zake za kuchapa kazi, kupiga vita rushwa na ubadhirifu na kuweka mbele uzalendo na maslahi ya taifa.

Mazishi ya Hayati Dkt. Magufuli yatafanyika Ijumaa Machi 26, 2021 katika makaburi ya familia kijijini kwake Chato mkoani Geita.

Mawaziri mbalimbali pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali wakiwa katika uwanja wa Magufuli tayari kwa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi-Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika uwanja wa Magufuli wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika uwanja wa Magufuli wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita



Wednesday, March 24, 2021

WAZIRI MKUU WA INDIA NA JAPAN PAMOJA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA OMAN WAANDIKIA BARUA YA KISERIKALI KWA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KWA SALAMU ZA RAMBIRAMBI NA PONGEZI



 

MSAFARA WA HAYATI MAGUFULI KUELEKEA GEITA - CHATO

Picha mbalimbali za msafara wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea Chato mkoani Geita leo tarehe 24 Machi 2021














VIONGOZI WAKUU WA NCHI NA SERIKALI DUNIANI WASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA JPM

 

Rais wa Burundi Mhe. Èvariste Ndayishimiye akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Tanzania nchini Burundi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli 


Rais wa Ethiopia Mhe. Sahle-Work Zewde akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

Naibu Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Ulinzi wa Serikali ya Oman, Mtukufu Sayyid Shihab bin Tarik bin Taimur Al-Said, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli 

 


WAZIRI MKUU AONGOZA WAKAZI WA MWANZA KUMUAGA JPM

Na Mwandishi wetu, Mwanza

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Waombolezaji walianza kuingia uwanjani leo alfajiri na wengine wakiwa wamejipanga barabarani kuulaki msafara wa mwili wa Hayati Magufuli ukitokea Zanzibar.

Mhe. Majaliwa aliongozana na mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wa taasisi za umma na binafsi katika hafla ya kutoa heshima za mwisho kwa kwa hayati Dkt. Magufuli anayetarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Chato Machi 26, 2021.

Wengine waliohudhuria ni pamoja na wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa salamu za pole kwa wananchi wa Mwanza katika hafla kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati alipowasili katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza katika hafla kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akitoa heshima za mwisho katika uwanja wa CCM Kirumba wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli


Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba    

Wananchi wa Jiji la Mwanza wakiwa barabarani kushuhudia msafara uliobeba mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli 






 

Monday, March 22, 2021

HABARI PICHA MWILI WA HAYATI DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI UKIAGWA JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Lazarius Chakwera akipokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati alipowasili katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli 


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akisaini kitabu cha maombolezo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma baada ya kuwasili kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli


Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani akisaini kitabu cha maombolezo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma baada ya kuwasili kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli




Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa akisaini kitabu cha maombolezo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma baada ya kuwasili kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa wakati wa mazishi ya kitaifa ya Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa akitoa salamu za rambirambi wakati wa mazishi ya kitaifa ya Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mhe. Felix Tshisekedi akitoa salamu za rambirambi wakati wa mazishi ya kitaifa ya Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Mjane wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akitoa heshima za mwisho kwa mume wake hayati Dkt. Magufuli wakati wa mazishi ya kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu akitoa heshima za mwisho kwa Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. Magufuli wakati wa mazishi ya kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akitoa heshima za mwisho kwa Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. Magufuli wakati wa mazishi ya kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) Dkt. Stergomena Tax akitoa heshima za mwisho kwa Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. Magufuli wakati wa mazishi ya kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakitoa heshima za mwisho kwa Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. Magufuli wakati wa mazishi ya kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akitoa heshima za mwisho kwa Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. Magufuli wakati wa mazishi ya kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma 


Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati wa mazishi ya kitaifa ya Rais wa Tano wa Tanzania hayati Dkt. Magufuli  



Sunday, March 21, 2021

DODOMA WAENDELEA KUMLILIA MHE. DKT. MAGUFULI


Viongozi wa Serikali, Kitaifa na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya jijini Dodoma wameendelea kumlilia aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia tarehe 17 Machi, 2021 jijini Dar es Salaam. 

Wananchi hao wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nyerere Square jijini humo kusaini kitabu cha maombolezo. Wananchi hao pia wameelezea hisia zao jinsi walivyokea msiba huo na walivyomfahamu Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 

Akiandika katika kitabu cha Maombolezo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge ameelezea jinsi alivyoguswa na msiba huo na kusema kuwa atamkumbuka daima Hayati Magufuli kwa jinsi alivyojitoa kuwatumikia wananchi wa Tanzania. " Kwa uchungu na masikitiko makubwa sana sababu Watanzania tumempoteza kiongozi na mpenda maendeleo aliyejipanga kuwaletea maendeleo ya kweli Watanzania," ameandika .

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ameelezea hisia zake kwa kuandika "Tunakushukuru na kumshukuru kwa zawadi ya uhai wako uliyoitoa kwa Watanzania kizalendo kuwapigania, Mungu kazi sake haina makosa. Taifa limetikisika tutakuenzi kwa mema mengi, uongozi bora, uzalendo, maendeleo, upendo, amani na taifa".

 
Kwa upande wake Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia alijitokeza katika viwanja vya Nyerere Square kusaini kitabu cha maombolezo ameelezea hisia zake akisema “Hayati Dkt. Magufuli ametutoka katika kipindi ambacho tulikuhitaji sana. Watanzania tunakupenda na tutaendelea kukuoenda kwa matendo na mambo mema uliyotufanyia na kutuachia kama Taifa”. Aliendelea kueleza kuwa Afrika imepoteza shujaa na mtetezi wa Bara.

Wakati huo huo Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mhe. Dormohamed Issa Rahmat amesema “Kwa majonzi, masikitiko na maumivu makubwa tuliyonayo Watanzania kwa kuondokewa na mzalendo namba moja, Jemedari wa Maendeleo na shujaa wa kupambania maskini na wanyonge. Sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu na kumuomba ialaze Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw. Mohamed Ramadhani ameeleza “Mheshimiwa Rais ulikuwa kiigizo chema kwetu, umeweza kutufumbua Watanzania kuwa hakuna kinachoshindikana panapo dhamira ya dhati tukiamua kufanya masuala ya msingi katika kutatua changamoto zinazoikabili nchi yetu, tutakuenzi kwa kuendeleza yale uliyoyanzisha huku tukitambua na kuzingatia kauli yako ya vita ya kiuchumi hakuna Mataifa yasiyo na nia njema yatakayo tupenda. Pumzika kwa amani Jemadari Wetu Mungu akujalie Pepo”. 

Mwili Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli umewasili jijini Dodoma majira ya saa 10 jioni kutokea Dar es Salaam na kupokelewa na Wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Dkt, Benelith Mahenge na Viongozi weinigen wa Serikali.

Mwili wa Hayati Dkt. Magufuli umepitishwa katika Mitaa mbalimbali ya Jiji la Dodoma na kuelekea Ikulu Chamwino. Tarehe 22 Machi, 2021 ataagwa rasmi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye kueleekea katika uwanja wa Jamhuri. Miongoni mwa shughuli zitakazofanyika Uwanjani hapo ni pamoja na gwaride la mazishi kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania, dua na sala, salamu za maombolezo na kutoa heshima za mwisho.

Jumanne Machi 23, 2021 saa 12 asubuhi mwili wa Hayati Dkt. Magufuli utatolewa katika hospitali ya Banjamin Mkapa na kusafirishwa kuelekea Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea jijini Dar es Salaam tarehe 17, Machi 2021.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Patrobas Katambi akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea jijini Dar es Salaam tarehe 17, Machi 2021.

Mke wa Rais wa Awamu ya Nne na Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi Mhe. Salma Kikwete akitia saini katika kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea jijini Dar es Salaam tarehe 17, Machi 2021.

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea jijini Dar es Salaam tarehe 17, Machi 2021.

Wakazi wa jijini Dodoma wakiwa katika Viwanja vya Nyerere Square jijini humo kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea jijini Dar es Salaam tarehe 17, Machi 2021.

Mtoto huyu alikuwa miongoni mwa wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea jijini Dar es Salaam tarehe 17, Machi 2021.

Mwanahabari kutoka Television ya Serbia akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea jijini Dar es Salaam tarehe 17, Machi 2021.