Wednesday, January 11, 2023
Tuesday, January 10, 2023
DKT. TAX AKUTANA NA BALOZI WA INDIA, DPRK NA MWAKILISHI WA HUAWEI-TANZANIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.
Stergomena Tax amekutana kwa mazungumzo kwa nyakati tofauti na wageni
kadhaa waliomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
Wageni hao ni Balozi wa India nchini, Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, Mhe. Kim Young Su na Naibu Mkurugenzi
wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Tao Mian.
Akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Dkt. Tax amemshukuru Balozi
huyo kwa kutenga muda wa kumtembelea kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kwenye
wadhifa huo na kueleza kwamba ziara hiyo itamwezesha kuelewa kwa kina hatua
mbalimbali zilizofikiwa katika ushirikiano kati ya Tanzania na India na pia
kubadilishana mawazo ya namna ya kufanikisha
masuala mbalimbali yaliyokubalika katika ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Amesema Tanzania na India zinashirikiana katika Sekta mbalimbali zenye
umuhimu kwa wananchi ikiwemo Sekta ya
maji, elimu, teknolojia na afya na
kwamba ni wakati sasa kwa nchi hizi mbili kuendelea kutekeleza kwa kasi
makubaliano mbalimbali ambayo tayari yamefikiwa ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
“Ushirikiano wetu unaenda vizuri
na mambo tunayokubaliana kushirikiana na kufanyia kazi kwa pamoja yanaenda,
zaidi tuongeze kasi kuyatekeleza. Niwahakikishie kuwa tutaaendelea kushirikiana
ili kuendeleza uhusiano wetu ambao ni wa kidugu na kihistoria, ambao umekuwepo
kwa miaka mingi,” amesema Dkt. Tax.
Naye Balozi wa India Mhe. Binaya Pradhan
ameeleza kuridhishwa kwake na ushirikiano anaoupata nchini katika kutekeleza
majukumu yake na kueleza kwamba Serikali ya India kupitia Hospitali ya Apolo wamekubali
kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,
Hospitali ya Bugando ya jijini Mwanza na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam katika kutoa
huduma na kuwajengea uwezo watumishi katika hospitali hizo ili kusaidia
wananchi wa Tanzania.
Kuhusu sekta ya elimu, Balozi huyo amesema wamekuwa wakishirikiana na Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT) katika kukiboresha ili kukiwezesha kuwa Kituo bora cha utoaji wa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano nchini.
Akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea Mhe.
Dkt. Tax amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo katika sekta
mbalimbali ambazo tayari nchi hizi mbili zinashirikiana ikiwemo kilimo, elimu
afya na teknolojia ya habari na mawasiliano na utamaduni.
Kwa upande wake, Balozi Kim Young Su amempongeza Mhe. Dkt. Tax kwa
kuteuliwa kwenye wadhifa huo ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana naye na
kumwahidi ushirikiano. Pia amesema kuwa, Nchi yake itaendelea kushirkiana
na Tanzania katika sekta mbalimbali na
kwamba ushirikiano wa kihistoria uliopo ambao umejengwa katika misingi
iliyoachwa na waasisi wa mataifa mataifa haya utaendelezwa.
Akizungumza na Naibu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania Mhe. Tax ameipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji wao katika masuala ya Teknolojia hususan kupitia mradi wao wa kusambaza huduma za kidigitali vijijini.
“ Huawei ni Kampuni kubwa na tunathamini uwepo wenu hapa nchini. Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano ni mingoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya
Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Hivyo tutaendelea kushirikiana nanyi hususan kwenye kusambaza huduma
za kidigitali vijijini na vyuoni ili hatimaye tuweze kufikia ndoto yetu ya kuwa
kitovu cha kidigitali,” alisema Mhe. Dkt. Tax.
Kwa upande wake, Bw. Tao Mian alieleza kwamba hapa nchini Kampuni hiyo
imetengeneza ajira zaidi ya 1000 ambapo zaidi ya asilimia 70 ya ajira ni za
watanzania.Kadhalika Kampuni hiyo inashirikiana na zaidi ya kampuni 70 za ndani, Wahandisi wa
TEHAMA zaidi ya 2000 nchi nzima pamoja na vyuo zaidi ya 19 nchini. Aidha,
Kampuni hiyo inaendesha mafunzo ya TEHAMA kwa zaidi ya wanafunzi 2000,
kuhudumia zaidi ya asilimia 75 ya watanzania na kwamba imekuwa mchangiaji
mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA nchini.
“Tunaridhishwa na uungwaji mkono wa Kampuni yetu hapa Tanzania na tunaahidi
kuendelea kuchapa kazi ili kuhakikisha huduma za kidigitali zinawafikia
wananchi wengi kwa wakati mmoja hususan wale wa vijijini” alisema Bw. Mian.
Pia alimueleza Mhe.
Dkt Tax juu ya Mpango kabambe wa kuboresha mawasiliano ya TEHAMA vijijini ambao
ni sehemu ya Mkataba wa ushirikiano uliosainiwa baina ya Tanzania na China ambao
unatarajiwa kutekelezwa na Kampuni hiyo. Katika mradi huo kutakuwa na jumla ya
miradi 19 ya kipaumbele, uboreshaji wa mawasiliano vijijini, usambazaji wa umeme
Kaskazini Mashariki mwa Tanzania pamoja na miradi 9 ya msaada ambayo
itatekelezwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) na
Hospitali ya Zanzibar.
Kampuni ya Huawei Tanzania ambayo imewekeza kwa zaidi miaka 15 nchini, inashirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) kusambaza Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwezesha huduma za kidigitali kupatikana kwa urahisi nchi nzima ambapo hadi sasa mkongo huo umesambaa kwa zaidi ya kilomita 15,000 nchi nzima.
Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa India nchini (kulia) akiwa na Naibu Balozi wa Ubalozi huo wakati wa mazungumzo kati yake na Mhe. Dkt. Tax |
Mhe Binaya Pradhan, Balozi wa India nchini akimkabidhi Mhe. Dkt. Tax zawadi ya kasha la kuhifadhia vitu. |
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Balozi Mhe Binaya Pradhan mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao |
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Balozi Mhe Binaya Pradhan wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki mazungumzo yao |
Mhe. Dkt. Tax akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Kim Young Su |
Mazungumzo yakiendelea |
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Mhe. Kim Young Su mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao |
Picha ya pamoja Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Tao Mian alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 10 Januari 2023
|
Picha ya pamoja |
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Bw. Tao Mian mar abaada ya kukamilisha mazungumzo yao |
Monday, January 9, 2023
DKT. TAX AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NA WAWAKILISHI WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA YALIYOPO NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Dkt. Stergomena Tax leo tarehe 09
Januari 2023 amekutana kwa mazungumzo kwa nyakati tofauti na wageni mbalimbali
waliomtembelea ofisini kwake Mtumba
jijini Dodoma
Wageni hao ni Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui; Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Mahoua
Parums; Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Bianadamu na Watu, Mhe. Jaji Iman
Aboud na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna.
Akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Dkt. Tax
amempongeza Mhe. Balozi Nabil Hajlaoui kwa hatua ya Ubalozi huo kufungua ofisi
jijini Dodoma ikiwa ni ishara ya Ufaransa katika kuuunga mkono harakati za Serikali
ya Tanzania za kuimarisha makao makuu ya nchi Dodoma.
“Mhe. Balozi nchi zetu zimekuwa na uhusiano wa kirafiki
uliodumu tangu Tanzania ilipopata uhuru wake, na tumeendelea kuungana mkono
katika ngazi ya nchi na hata kimataifa, na kwa hili mnalolifanya hapa Dodoma
linadhihirisha kuimarika kwa ushirikiano wetu,” alisema Dkt. Tax
Akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Ufaransa alisema
nchi yake imeamua kufungua ofisi ya ubalozi jijini Dodoma kama njia mojawapo ya
kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Ufaransa pamoja kuunga mkono hatua ya
Serikali ya kuhamishia makao makuu yake jijini humo.
Ameongeza kusema mwezi Juni 2023 Ufaransa inatarajia
kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Paris hadi Dar es Salaam
kupitia Zanzibar. Itakumbukwa kuwa mwaka 2021 Shirika hilo lilianzisha safari
zake Zanzibar kupitia Nairobi, Kenya.
Amesema kuanzishwa kwa safari hizo za moja kwa moja
zitawawezesha watalii kutoka Ufaransa kuja moja kwa moja nchini na hivyo
kupunguza urefu wa safari na hivyo kufanya watalii na wafanybiashara wengi kuja
kuangalia fursa na kutembelea vivutio vya utalii nchini kwa urahisi.
Mhe. Balozi pia amesema Ubalozi pia utaendeloea kutoa
mafunzo ya lugha ya kifaransa kwa watumishi wa umma ambapo ikwa kuanzia
wanaendelea na mafunzo hayo kwa watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Ulinzi na katika Chuo cha Idara ya
Uhamiaji mjini Moshi.
Mhe. Balozi pia ameongelea nia ya nchi yake kuunganisha
nguvu na Tanzania katika sekta ya nishati mbadala ili kuiwezesha Tanzania
kujitosheleza na nishati hiyo nchini na hivyo kukuza uchumi wake.
Katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Mahoua Parums, Mhe. Dkt.
Tax amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Shirika hilo katika zoezi
linaloendelea la kuwarejesha kwa hiari wakimbizi kwenye nchi zao za asili.
Kwa upande wake, Bi. Parums ameipongeza Serikali ya
Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi licha ya changamoto mbalimbali
zilizopo. Amesema Shirika lake linathamini mchango huo wa kibinadamu wa
Tanzania kwa wakimbizi hao na kwamba litaendelea kushirikiana na Serikali
katika kuwarejesha kwa hiari wakimbizi wa Burundi.
Akizungumza na Mhe. Jaji Iman wa Mahakama ya Afrika ya
Haki za Bianadamu na Watu, Mhe. Dkt. Tax amesema Serikali ya Tanzania kama
mwenyeji wa Mahakama hiyo iliyopo Arusha itaendelea kutekeleza makubaliano ya
mkataba wa uenyeji kama ulivyoainisha.
Naye Jaji Iman amemhakikishia ushirikiano Dkt. Tax na
kwamba wanaipongeza Serikali kwa kuendelea kutekeleza makubaliano ya mkataba wa
uenyeji ambapo hadi sasa Mahakama hiyo
imepatiwa eneo la ukubwa wa ekari 25 kwa ajili ya kujenga ofisi zake za kudumu
jijini Arusha.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa UNICEF nchini ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kusimamia na kutekeleza kikamilifu mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayohusu masuala ya haki za watoto ikiwemo afya, elimu na kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023 |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui pamoja na wajumbe walioambatana nao kwenye mazungumzo kati yao yaliyofanyika ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023 |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Bi. Mahoua Parums alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023 |
Mhe. Dkt. Tax akipokea zawadi ya machapisho mbalimbali kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Bi. Mahoua Parums alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023 |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Bianadamu na Watu, Mhe. Jaji Iman Aboud alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023 |
Mhe. Dkt. Tax akiwa katika mazungumzo na Mhe. Jaji Iman |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna alipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 09 Januari 2023 |
Sehemu ya ujumbe wa Mhe. Dkt. Tax ukifuatilia mazungumzo kati yake na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna |
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna akimpatia Mhe. Dkt. Tax maelezo ya zawadi ya picha kabla ya kumkabidhi |
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna akimkabidhi Mhe. Dkt. Tax zawadi ya picha ya watoto kama ishara ya kuonesha mchango wa shirika hilo katika kuwahudumia watoto hapa nchini |
Saturday, January 7, 2023
DKT. TAX AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA WIZARA MTUMBA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), ametembelea na kujionea namna ujenzi
wa jengo la Wizara katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma unavyoendelea.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi Mhe. Dkt. Tax
amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo kuongeza kasi ili ujenzi ukamilike
kwa wakati.
“Nimetembelea hapa, nimejionea kazi ilipofika,
kazi bado ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili Mungu akijaalia mwezi
Oktoba mwaka huu badala ya Desemba ujenzi uwe umekamilika na tuone tunajipanga
namna gani,” amesema Dkt. Tax.
Amesema Wizara ina uhitaji mkubwa wa jengo hilo
kwa kuwa watumishi wametawanyika katika maeneo matatu tofauti na inakuwa ngumu kukutana kwa haraka pale inapobidi.
Amesema kukamilika kwa jengo Hilo kutatoa ahueni
kwa watumishi wa wizara na kuwawezesha kuwa sehemu moja na hivyo kurahisisha
utendaji kazi wa Wizara.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Dkt. Tax
aliambatana na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine na watendaji
wengine wa Wizara.
Ujenzi wa jengo la Wizara ulianza mwezi Januari
2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2023. Ujenzi huo utagharimu kiasi
cha Shilingi bilioni 22.9 ambazo
zimetolewa na Serikali ili kuziwezesha Wizara na Taasisi za Serikali kuwa na
majengo ya kudumu katika mji wa Serikali.
Ujenzi huo unafanywa na Umoja wa makampuni ya
Sole works na mshauri elekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha wageni alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 07 Januari 2023 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha wageni akiwa ameambatana na Mhe. Dkt. Tax kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 07 Januari 2023 |
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na wakandarasi wa jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambapo aliwahimiza kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo hilo. |
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na wakandarasi wa jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambapo aliwahimiza kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo hilo. |
Sehemu ya Wakurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamsikiliza Mhe. Dkt. Tax wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serijkali Mtumba |
Sehemu ya Wakurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamsikiliza Mhe. Dkt. Tax wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serijkali Mtumba Sehemu ya Wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa Jengo la Wizara wakimsikiliza Mhe. Dkt. Tax alipotembelea jengo la Wizara kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi |
Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa Jengo la Wizara akitoa maelezo kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo ambapo kwa sasa limekamilika kwa asilimia 55. |
Mkandarasi wa Jengo la Wizara akifafanua jambo kwa Mhe. Dkt. Tax kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo kwa kuonesha picha |
Mhandisi wa Wizara, Bw. John Kiswaga naye akitoa ufafanuzi kwa Mhe. Waziri Tax kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara |
Mhe. Balozi Mbarouk akiangalia sampuli ya fremu za milango na kusisitiza ujenzi huo uzingatie ubora wa hali ya juu wa vifaa vyote vitakavyotumika kama, mbao, vigae na marumaru. |
Mhe. Balozi Mbarouk akisisitiza jambo kwa wakandarasi kabla ya kuanza ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara |
Mhe. Dkt. Tax kwa pamoja na Mhe. Balozi Mbarouk wakiingia kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma |
Mhe. Dkt. Tax akipanda ngazi kuelekea ghorofa za juu za jengo hilo ili kukagua maendeleo ya ujenzi |
Mhe. Dkt. Tax akimsikiliza Mkandarasi wa Wizara, Bw. Kiswaga wakati akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya ujenzi wa jengo la Wizara |
Mhe. Dkt. Tax akitoa maelekezo kwa wakandarasi na kuwataka kuongeza kasi na kuzingatia ubora na viwango katika ujenzi wa jengo la Wizara |
Mwonekano wa jengo la Wizara linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma |
DKT. TAX AWATAKA WATUMISHI KUBORESHA UTENDAJI
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa mkutano wake wa kwanza na Watumishi wa Wizara hiyo tangu kuteuliwa kwake kwenye wadhifa huo mwezi Oktioba 2022. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza kumkaribisha Waziri Dkt Tax wakati wa mkutano na Watumishi wa Wizara hiyo. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza wakati wa mkutano na Watumishi wa Wizara hiyo na Waziri Dkt Tax |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Rajab wakati wa mkutano kati ya Mhe. Dkt. Tax na Watumishi wa Wizara hiyo. |
Mtaalam wa masuala ya Saikolojia kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma, Dkt. Mohammed akitoa mada kuhusu UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza wakati wa mkutano wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Mtoa Huduma za Kibenki kutoka Benki ya Stanbic akitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa kikao kati ya Watumishi hao na Waziri Mhe. Dkt Tax |
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Pili Sukwa akitoa neno la shukrani wakati wa mkutano kati ya Watumishi wa Wizara na Mhe. Dkt. Tax |
Mshereheshaji Bi. Semeni Nandonde akitoa maelezo ya ratiba kuhusu mkutano kati ya Mhe. Dkt. Tax na Watumishi |
Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
|
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Dkt. Tax |
Picha ya pamoja |