Wednesday, March 8, 2023

BALOZI MBAROUK AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALIMBALI DOHA QATAR

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) kwa nyakati tofauti amekutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Vallamvelly Muraleedharan pamoja na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Uhusiano wa Jumuiya za Kimataifa Mhe. Michelle Sison, Doha nchini Qatar.   

Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi zinazoendelea (LDCs) unaendelea Doha nchini Qatar.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Vallamvelly Muraleedharan. Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi zinazoendelea (LDCs) unaendelea Doha nchini Qatar.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Vallamvelly Muraleedharan, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zinazoendelea (LDCs) unaendelea Doha nchini Qatar.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Uhusiano wa Jumuiya za Kimataifa Mhe. Michelle Sison. Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi zinazoendelea (LDCs) unaendelea Doha nchini Qatar.

Mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Uhusiano wa Jumuiya za Kimataifa Mhe. Michelle Sison yakiendelea Doha nchini Qatar. Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi zinazoendelea (LDCs) unaendelea Doha nchini Qatar.





Tuesday, March 7, 2023

DKT. TAX AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya  Tanzania na Uingereza na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kudumisha na kuendeleza uhusiano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax) walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam






Thursday, March 2, 2023

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALIMBALI NCHINI AZERBAIJAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan, Mhe. Shahin Mustafayev. Viongozi hao walifanya mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya Isiyofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Baku, Azerbaijan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan, Mhe. Shahin Mustafayev. Mazungumzo hayo yalifanyika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya Isiyofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Baku, Azerbaijan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan, Mhe. Shahin Mustafayev.Vingozi hao walifanya mazungumzo  pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya Isiyofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Baku, Azerbaijan


Dkt. Mpango na Makamu wa Rais wa Cuba

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valders Mesa. Viongozi hao walikutana kwa mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya Isiyofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Baku, Azerbaijan 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valders Mesa. Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya Isiyofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Baku, Azerbaijan 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) akimpa zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valders Mesa. Viongozi hao wamekutana kwa mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya Isiyofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Baku, Azerbaijan 




VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE AFRICAN UNION COMMISSION


 

Tuesday, February 28, 2023

BALOZI SHELUKINDO ASISITIZA UMUHIMU WA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akipokea maua mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023. Balozi Shelukindo aliapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuushika wadhifa huo tarehe 27 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Fatma Rajab wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Alex Mfungo wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Naimi Aziz wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.


Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Caesar Waitara wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Bw. Japhary Kachenje wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ofisi za Wizara  jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Haji Janabi wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ofisi za Wizara  jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Talha Waziri wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ofisi za Wizara  jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Samwel Shelukindo ajitambulishe kwa menejimenti ya Wizara wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo (kushoto) akiongoza kikao cha Menejimenti kilichofanyika kwa lengo la kujitambulisha katika ofisi za Wizara jijini Dododma tarehe 28 Februari 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Fatma Rajab. 

Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Alex Mfungo na Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango, Bw. Haji Janabi wakifatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Mkurugenzi Idara ya Afrika, Balozi Naimi Aziz akijitambulisha kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo katika hafla ya mapokezi yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.


Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caesar Waitara (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Noel Kaganda wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Kutoka kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Swalehe Chondoma na Bw. Haji Janabi wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.


Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Leonce Bilauri na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji wakifuatilia kikao cha utambulisho cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrka Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo.

Sehemu nyingine ya wajumbe wa managementi wakifuatilia kikao.

Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Amani Mwatonoka na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Salma Baraka wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dododma tarehe 28 Februari 2023.

Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dkt. Isaac Kalumu  na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Talha Waziri wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dododma tarehe 28 Februari 2023.

Mwakilishi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Ally Kondo (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Biashara za Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi, Bw., Francis Berege wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akiwasili katika ofisi za Wizara  jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo (kulia) akisalimiana na sehemu ya madereva walioshiriki hafla ya mapokezi katika ofisi za Wizara jiji Dodoma tarehe 28 Februari 2023

Picha ya Pamoja






TANZANIA KUANZA SAFARI ZA NDEGE MOJA KWA MOJA HADI SAUDI ARABIA

Tanzania inategemea kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hadi Saudi Arabia ambapo safari ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Jeddah inatarajiwa kuanza tarehe 26 Machi 2023.

Hayo yamebainishwa katika mazungumzo ya Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab na kujadili maandalizi ya uzinduzi wa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na Saudi Arabia. 

Katika mazungumzo yao viongozi hao pia walijadili mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za Tanzania hususan nyama na matunda. 

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab wakikabidhiana zawadi baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Ali Mwadini akijadiliana jambo na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia



Monday, February 27, 2023

EU YARIDHISHWA NA UBORESHWAJI WA HAKI ZA BINADAMU, UTAWALA BORA NCHINI

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akichangia jambo wakati wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya. Majadiliano hayo yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Umaoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti akitoa mchango wake wakati wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya. Majadiliano hayo yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Balozi wa Umaoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti wakionesha makubaliano waliyosaini baada ya majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yakiendelea Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme akichangia mjadala wa kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kasiga akiongoza majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya Jijini Dar es Salaam

Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika Nchi za Jumuiya ya Ulaya wakitambulishwa 

Picha ya pamoja 



VACANCY ANNOUNCEMENT


 

Sunday, February 26, 2023

DKT. TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA ZAMBIA, BRAZIL NA VATICAN

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amepokea nakala za Hati za Utambulisho za mabalozi wateule wa nchi za Zambia, Brazil na Vatican.

Mhe. Waziri Tax amepokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Zambia nchini, Mhe. Mathew Jere, Balozi mteule wa Brazil nchini, Mhe. Gustavo Martins Nogueira na Balozi Mteule wa Vatican Nchini, Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti Waziri Tax amewahakikishia ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao ya kibalozi hapa nchini. Pia Waziri Tax ametoa rai kwa mabalozi hao kuendeleza na kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na nchi zao.

“Tanzania na Zambia tumekuwa marafiki na ndugu wa muda mrefu, Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Zambia katika sekta za biashara na uwekezaji kwa maslahi mapana ya pande zote mbili,” alisema Dkt. Tax  

Balozi mteule wa Zambia nchini, Mhe. Mathew Jere ameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Zambia na Tanzania katika sekta za biashara na uwekezaji, usafirishaji, pamoja na nishati.  

Kwa upande wake Balozi Mteule wa Brazil, Mhe. Gustavo Martins Nogueira ameahidi kuwa Brazil itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mapya ya kimkakati kwa manufaa ya mataifa yote mawili hususan kilimo, biashara na uwekezaji.

Naye Balozi wa Vatican nchini, mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino ameahidi kuendeleza kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya Vatican na Tanzania. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea  nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Zambia nchini, Mhe. Mathew Jere katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea  nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa  Brazil nchini,  Mhe. Gustavo Martins Nogueira katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea  nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa  Vatican nchini, Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam