Tuesday, June 13, 2023

KONSELI KUU YA LUBUMBASHI YAKUTANA NA MADEREVA

Kaimu Konseli Mkuu katika Konseli Kuu ya Tanzania, Lubumbashi, Bi. Asha Mlekwa akiwa na ujumbe wa wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jimbo la Haut-Katanga, Mhe. Erick Muta Ndala walifanya ziara ya kutembelea madereva wa malori ya Tanzania  yanayofanya safari kati ya Tanzania na DRC upande wa Jimbo la Haut-Katanga na Jimbo la Lualaba. Ujumbe huo uliofika maeneo hayo tarehe 12 Juni 2023 ulisikiliza changamoto za kiusalama zinazowakabili madereva wa malori wanaosafirisha mizigo kati ya DRC na Tanzania inayopita katika Bandari ya Dar es Salaam. Mhe. Ndala aliahidi kuendelea kuboresha hali ya usalama wa madereva na mizigo akitoa mfano wa mafanikio yaliyofikiwa katika kupunguza vitendo vya utekaji wa malori yanayobeba madini ya shaba.

Madereva wa Malori wakielezea changamoto wanazokutana nazo na kupewa majibu kutoka kwa Wahusika.
Kaimu Konseli Mkuu katika Konseli Kuu ya Tanzania, Lubumbashi, Bi. Asha Mlekwa  na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jimbo la Haut-Katanga, Mhe. Erick Muta Ndala na ujumbe wa wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwasili eneo la kuegesha malori kwa ajili ya kujadili  utatuzi wa changamoto wanazokabiliana nazo madereva wa Tanzania wanaofanya safari kati ya Tanzania na DRC.




Monday, June 12, 2023

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Alexander Schallenberg ofisini kwake jijini Vienna, Austria


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Alexander Schallenberg ofisini kwake jijini Vienna, Austria

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Waziri wa Austria anayeshughulikia masuala ya Ulaya na uhusiano wa Kimataifa Mhe. Alexxander Schallenberg ofisini  kwake jijini Vienna, Austria.

 





 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Alexander Schallenberg ofisini kwake jijini Vienna, Austria

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na ujumbe wake katika picha ya pamoja na na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Alexander Schallenberg ofisini kwake jijini Vienna, Austria

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Alexander Schallenberg ofisini kwake jijini Vienna, Austria 

Viongozi hao wamena kujadili masuala mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Austria.

Dkt. Tax alielezea kufurahishwa kwake na jinsi uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria ulivyo imara na hatua za kuhakikisha unaendelea kuimarika zinachukuliwa na pande zote mbili.

Waziri Dkt. Tax ameishukuru Serikali ya Austria hasa Wizara inayoshughulikia masuala ya Ulaya na uhusiano wa Kimataifa kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania Vienna tangu ulipoanzishwa mwaka 2021 na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Austria kama mdau wake mkubwa wa maendeleo.

 

Naye Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Alexander Schallenberg alisema Austria inaupongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake nchini humo na hivyo kuwa na uwakilishi kamili.

Alisema Austria itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano kama vile elimu, afya, miundombinu na kubadilishana watalaamu ili kuwezesha nchi zote mbili kunufaika na uhusiano huo.

 

WAZIRI DKT. TAX AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA IAEA JIJINI VIENNA


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Nishati na Atomiki (IAEA) Bw.  Rafael Grossi walipokutana jijini Vienna, Austria.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Nishati na Atomiki (IAEA) Bw.  Rafael Grossi walipokutana jijini Vienna, Austria.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena  na ujumbe wake wakizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Nishati na Atomiki (IAEA) Bw.  Rafael Grossi jijini Vienna, Austria.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (DMC) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda walipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Nishati na Atomiki (IAEA) Bw.  Rafael Grossi  jijini Vienna, Austria.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Nishati na Atomiki (IAEA) Bw.  Rafael Grossi na ujumbe wake walipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na ujumbe wake kjijini Vienna, Austria.

 kikao kikiendelea.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Nishati na Atomiki (IAEA) Bw.  Rafael Grossi jijini Vienna, Austria .

 

Katika mazungumzo yao Mhe. Dkt. Tax amemuhakikishia mkurugenzi huyo wa IAEA kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na shirika hilo kulishukuru kwa misaada inayoitoa kwa Tanzania kupitia sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kuipatia vifaa tiba na kuongeza idadi ya wataalamu nchini.

 


WAZIRI TAX AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA UNODC JIJINI VIENNA

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na udhibiti wa  biashara haramu ya dawa za kulevya na Uhalifu uliopangwa (UNODC) Mhe. Ghada Fathi Waly jijini Vienna.

 

 

 

kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na. ujumbe wake na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na udhibiti wa  biashara haramu ya dawa za kulevya na Uhalifu uliopangwa (UNODC) Mhe. Ghada Fathi Waly na ujumbe wake kikiendelea jijini Vienna

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na udhibiti wa  biashara haramu ya dawa za kulevya na Uhalifu uliopangwa (UNODC) Mhe. Ghada Fathi Waly jijini Vienna.

Mhe. Dkt. Tax ameelezea kuridhishwa kwake na kupongeza kazi zinazofanywa na Shirika hilo  kufuatia jitihada zao za kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya , ufisadi na uhalifu wa kupangwa.  

Amesema Umoja wa Mataifa na UNODC wanatekeleza jukumu muhimu katika kukabiliana na biashara haramu ya dawa, ambayo inatishia amani, usalama na afya ya watu duniani

Amesema kupitia mikakati yao kamili, mipango, na ushirikiano, wamekuwa muhimu katika kuongeza uelewa, kutoa msaada wa kiufundi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na masuala yanayohusiana na dawa kwa ufanisi.


TANZANIA YAZINDUA UBALOZI WAKE VIENNA, AUSTRIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa mataifa Vienna, Austria. Pamoja naye ni Naibu Waziri wa Austria aneyeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal ambaye alihudhuria hafla hiyo ya ufunguzi iliyofanyika tarehe 12 Juni, 2023.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Naibu Waziri wa Austria anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa  Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal wakipongezana  baada ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna, Austria.

 


Kaimu Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Vienna nchini Austria Bi. Elizabeth Rwitunga akizungumza katika hafla ya kuzindua Ubalozi wa Tanzania Vienna terehe 12 Juni, 2013

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna Austria.
Mhe. Dkt. Tax akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna Austria.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Naibu Waziri wa Austria anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa  Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal wakinyanyua mikono baada ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna, Austria.


 

Naibu Waziri wa Austria anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa  Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal akizungumza wakati wa hafla ufunguzi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna, nchini Austria.

 

Baadhi ya wanadiplomasia waliopo jijini Vienna walioshiriki hafla ya  ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna wakifuatilia ufunguzi huo.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Naibu Waziri wa Austria anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa  Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal katika picha ya pamoja na Diaspora wa Tanzania nchini Austria walioshiriki hafla ya  ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna

 






 



 


 

 

 


 

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua rasmi Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini Vienna nchini Austria.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo ni mafanikio yanayoimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Vienna na kinaonesha jinsi Tanzania inavyoipa kipaumbele Austria.

 

“Kufunguliwa kwa Ubalozi huu ni mafanikio makubwa ambayo yanaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo hapa jijini Vienna na kinaonesha kwa vitendo kuwa Tanzania inaipa kipaumbele Uhusiano wake na Austria,” alisema Dkt. Tax.

 

Ameishukuru Serikali ya Austria na Wizara inayoshughulikia masuala ya Ulaya na uhusiano wa Kimataifa kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania Vienna tangu ulipoanzishwa hadi kufikia siku ya uzinduzi.

 

Akiongelea uhusiano uliopo Dkt. Tax amesema Tanzania na Austria zimeendelea kufaidika na uhusiano mzuri kati yao kupitia maeneo mbalimbali kama elimu, afya, miundombinu na hivyo kuchangia maendeleo ya kiuchumi kwa faida ya wananchi wake.

 

Amesema Serikali ya Tanzania inathamini uhusiano na ushirikiano na wadau wote ambao wanapambania agenda moja za kulinda na kukuza amani na usalama pamoja na kupambana na uhalifu wa kupangwa, rushwa, ugaidi na amewaomba kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo endelevu kwa manufaa ya watu wote.

 

“Serikali ya Tanzania inathamini uhusiano na ushirikiano na wadau wote ambao tunapigania agenda moja, ajenda hizi ni kama  kulinda na kukuza amani na usalama, kupambana na uhalifu wa kupangwa, rushwa, ugaidi na mengine mengi , nawaomba tuendelee kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo endelevu kwa manufaa ya watu wote,” alisisitiza Dkt. Tax.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo jijini Vienna Naibu Waziri anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal amesema Austria inapongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake Austria na kuungana na nchi nyingine 16 za Afrika zenye Ubalozi nchini humo na kuahidi kuusaidia Ubalozi huo kwa kila hali ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.

 

 “Austria inapongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake Austria na hivyo kuungana na nchi nyingine 16 za Afrika ambazo zina Balozi zao hapa nchini, niwa ahidi na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Austria iko tayari kuusaidia Ubalozi huo kwa kila hali ili ufikie  malengo ya kuanzishwa kwake”, alisisitiza Waziri huyo.

 

Amesema Austria inaangalia uhusiano wake na Tanzania ambao una miaka mingi ukiwa imara na dhabiti na kuongeza kuwa ni imani yao kuwa kufunguliwa kwa Ubalozi huo ni hatua muhimu ya kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo.

 

Alisema Tanzania ina picha nzuri nchini Austria na nchi yao ni mshirika mkubwa anayeamini katika demokrasia imara na kuongeza kuwa Tanzania kujihusisha na harakati za kutafuta amani katika ukanda wa Afrika Mashariki na katika maeneo mengine kunavutia zaidi.


“Tanzania ina picha nzuri hapa Vienna, niseme wazi kuwa Nchi yetu ni mshirika mkubwa anayeamini katika demokrasia imara na kujihusisha kwa Tanzania katika harakati za kutafuta amani katika ukanda wa Afrika Mashariki na kwingineko kunaongeza uzuri wa picha yake,” alisema.


Hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo ulioanzishwa mwaka 2021 ilihudhuriwa na  wanadiplomasia mbalimbali walioko jijini Vienna.

 

 








Sunday, June 11, 2023

DKT TAX AZUNGUMZA NA RAIS WA JUMUIYA YA SAN EGIDIO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Rais wa Jumuiya ya San Egidio, Marco Impagliazzo, walipokutana jijini Roma, Italia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jumuiya ya San Egidio, Marco Impagliazzo, walipokutana jijini Roma, Italia.

 

Mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Rais wa Jumuiya ya San Egidio, Marco Impagliazzo, yakiendelea .


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na ujumbe wake katika picha ya pamoja  na Rais wa Jumuiya ya San Egidio, Marco Impagliazzo na ujumbe wake , walipokutana jijini Roma, Italia.


 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana na Rais wa Jumuiya ya San Egidio, Marco Impagliazzo, jijini Roma, Italia. 

Dkt. ameipongeza jumuiya hiyo kwa kazi nzuri ya kutoa misaada ya kibinadamu na kuwakaribisha kushirikiana na serikali katika kutafuta amani na kuboresha maisha ya watu wenye uhitaji.

WAZIRI TAX AINADI TANZANIA KWA JUMUIYA YA WAFANYABISHARA WA ITALIA



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax Akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.    


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax Akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.  
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead Teri akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Dunia akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Baadhi ya Washiriki wa mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023 wakifuatilia mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Italia (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa TTB Bw. Damas Mfugale (wa kwanza kulia) Mkurugenzi Mkuu wa TIC Bw. Gilead Teri (wa pili kushoto) na mwakilishi wa ZIPA Bw. Khamis Dunia baada ya kukamilisha mazungumzo yao na  Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Stergomena Tax kwa kushirikiana na  Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kituo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wameinadi Tanzania kama Kituo bora cha uwekezaji kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Italia.
 
Waziri Tax amewaeleza Wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kurekebisha sera na sheria mbalimbali ili kuwafanya wawekezaji wawe na mazingira bora ya kuendesha shughuli zao na hivyo kuvutia wawekezaji wengi zaidi.
 
Wafanyabiashara hao wameelezwa kuwa Tanzania ni salama kwa wao kuwekeza mitaji yao, ambapo pia watakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kulifikia na kunufaika na soko kubwa la EAC, SADC na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).
 
Miongoni mwa sekta zilizowavutia Wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Kilimo, Utalii, Viwanda, Uchumi wa Buluu, na Ujenzi.
 
Mkutano huo uliofanyika jijini Roma, Italia ulijumuisha Wafanyabiashara waliowekeza nchi Tanzania katika Sekta mbalimbali na wenye nia ya kuwekeza nchini







Saturday, June 10, 2023

DKT. TAX AKUTANA NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WA ITALIA JIJINI ROMA AWAITA WAJE KUWEKEZA NCHINI

  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023

Baadhi ya washiriki wa mkutano kati ya  jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara walioshiriki  mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023

 

Baadhi ya washiriki wa mkutano kati ya  jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023



 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Italia jijini Roma na kuwaita waje kuwekeza nchini kwa kuwa Serikali ya Tanzania ina dhamira ya dhati kushirikiana nao kukuza uchumi kupitia biashara na uwekezaji .

Amesema ushirikiano huo imara utawezesha pande zote mbili kupata nafasi ya kufahamu fursa mbalimbali zinazopatikana katika nchi hizo, kunufaika nazo na kufanya kazi pamoja.

“Mmesikia mengi yakisemwa hapa, nichukue nafasi hii kuwahakikishia dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kutaka kushirikiana na jumuiya yenu katika biashara na uwekezaji, naona kwamba tukishirikiana kwa pamoja tutafahmu fursa zinazopatikana katika nchi zetu na kujua jinsi ya kunufaika nazo, na hivyo kufanya kazi kwa pamoja” alisema.

Alisema mikutano miwili ya jukwaa la biashara iliiyofanyika awali ilikuwa nyenzo za kupatiana taarifa kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italiana kuongeza kuwa jukwaa la tatu litakalofanyika mwezi Julai 2023 litakuwa na manufaa zaidi kwa pande zote mbili.

Amesema Italia imekuwa ni mdau mkubwa wa Tanzania na moja ya nchi zenye biashara na uwekezaji mkubwa nchini na kuipatia misaada ya kimaendeleo japo biashara kati ya nchi hizo imekuwa ikielemea upande mmoja akitolea mfano katika kipindi cha miaka mitano ya 2018 2022 na kuongeza ni matumaini yake kuwa mkutano huo utakuwa chachu ya kuweka sawa uwiano huo  wa biashara .

Akizungumza katika mkutano huo,  hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini Bw. Damas Mfugale alisema Tanzania ina vivutio vingi na vizuri na kuwakaribisha wafanyabiashara ho kuja nchini kuwekeza katika tasnia ya Utalii.

Naye Mkurugenzi wa Mkuu wa Kituo cha uwekezaji nchini Dkt. Gelead Teri alisema Tanzania imeboresha mazingira ya kufanya biashara nchini na kuzingatia garantii inayowekwa ya kupata faida na kurejesha gharama za mtaji pamoja na soko kubwa linaloizunguka nchi la Afrika Mashariki, SADC na sasa AfCFTA.

Alisema hali ya amani na usalama , eneo nchi ilipo, utajiri wa maliasilia ni miongoni mwa sababu kubwa za kuvutia wawekezaji nchini. Amewaita wafanyabiashara hao waje nchini na kwamba hawatajuta kufanya hivyo.

Naye Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Khamis Dunia amewakaribisha wafanyabiashara hao kuja Zanzibar kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu ya ICT na ujenzi wa bandari kubwa ya Mangapwani. Amewaambia wafanyabiashara hao waje Zanzibar ili wanufaike na kusaidiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika ujenzi wa bandari hiyo

Mkutano huo na jumuiya ya wafanyabiashara Italia uliofanyika jijini Roma uliandaliwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.

 

WAZIRI TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA FAO JIJINI ROMA, ITALIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu walipokutana kwa mazungumzo jijini Roma, Italia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani  (FAO) Dkt. Qu Dongyu. Katika mazungumzo yao Dkt. Tax amepongeza FAO kwa jitihada zake za kutafuta na kukusanya rasilimali kwa ajili ya jamii mbalimbali ili ziweze kunufaika na  maendeleo ya kilimo ambazo amesema Watanzania wengi pia wanazitegemea.

Dkt. Tax yuko nchini Italia kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuzungumza na jumuiya ya wafanyabiashara wa nchini Italia.

Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya FAO jijini Roma, Italy
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu katika picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa FAO, Ubalozi wa Tanzania nchini Italia na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki