Friday, May 21, 2021

MAONESHO YA PILI YA KAZI ZA SANAA ZA TANZANIA YAFUNGULIWA JIJINI HONG KONG, CHINA.

Maonesho ya Pili ya Kazi za Sanaa za Tanzania yamefunguliwa tarahe 21 Mei, 2021 jijini Hong Kong nchini China. Hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo ilihudhuriwa na Jumuiya ya Wanadiplomasia na wafanyabiashara wa jijini Hong Kong


Katika hotuba yake ya Ufunguzi aliyoitoa kwa njia ya mtandao kutoka Beijing, Balozi wa Tanzania Nchini China ameeleza kwamba Tazania na China zimekubaliana kukuza mahusiano ya kitamaduni na sanaa na ili kuendelea kutoa fursa za kiuchumi kwa wasanii. 

Vilevile Balozi Kairuki ametumia fursa hiyo kuwaalika watalii kutoka China kutembelea Tanzania kujionea vivutio vya kiutamaduni na kazi za sanaa.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania jijini Hong Kong Ndugu Eddie Leung ameeleza kwamba Ofisi yake itaendelea kukuza mahusiano baina ya Tanzania na Hong Kong kupitia sanaa, utalii na biashara.

Aidha, Ndugu LEUNG ameahidi kuendelea kufadhili programu za mafunzo ya Uongozi kwa vijana wa kitanzania jijini Hong Kong. Mwaka 2019, Ndugu Leung alifadhili ziara ya mafunzo ya uongozi jijini Hong Kong kwa vijana 20 kutoka Tanzania.
Baadhi Wanadiplomasia na wafanyabiashara wa jijini Hong Kong wakikata utepe kwenye ufuguzi wa maonesho ya pili ya kazi ya sanaa za Tanzania zinazofanyika katika Jiji hilo.

Baadhi Wanadiplomasia na wafanyabiashara wa jijini Hong Kong wakiangalia kazi mbalimbali sanaa kwenye maonyesho yanayoendelea  jijini Hong Kong

Baadhi Wanadiplomasia na wafanyabiashara wa jijini Hong Kong wakisikiliza Hotuba ya Ufunguzi  ya Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.