Monday, May 17, 2021

TANZANIA YAENDELEA KUFANYA VYEMA UTAWALA BORA, HAKI ZA BINADAMU

Na Mwandishi wetu, Dar 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesema Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika viwango vya Utawala Bora na Haki za Binadamu hususani katika maeneo ya haki za kijamii pamoja na haki za kisiasa.

Mwenyekiti wa Tume hiyo (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) na kuongeza kuwa licha ya uwepo wa baadhi ya maeneo ya maboresho kwa sasa Tanzania iko katika daraja “A” miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika masuala ya Utawala Bora na Haki za Binadamu.

“Licha ya uwepo wa baadhi ya maeneo ya maboresho kwa sasa Tanzania iko katika daraja “A” miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika masuala ya Utawala Bora na Haki za Binadamu,” amesema Jaji Mwaimu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameipongeza Tume hiyo kwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuishauri Serikali katika kuzingatia na kutekeleza masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama ilivyoridhia katika majukwaa ya kimataifa. 

“Naipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kutekeleza majukumu yake vizuri ikiwemo kuishauri Serikali katika kuzingatia na kutekeleza masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama ilivyoridhia katika majukwaa ya kimataifa,” amesema Balozi Mulamula. 

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya Tanzania ni mwanachama katika tume nyingine za kikanda na kimataifa ambazo hupima viwango vya utekelezaji wa Haki za binadamu na Utawala Bora ambapo kwa sasa Tanzania ina kiwango “A”.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula wakati walipokutana kwa maongezi katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu wakati walipokutana kwa maongezi katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu yakiendelea katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu, Kamishna kutoka Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Nyanda Shuli na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.