Thursday, May 20, 2021

MAKABIDHIANO YA OFISI KATI YA BALOZI BRIG. JENERALI IBUGE NA BALOZI JOSEPH SOKOINE

Na Mwandishi wetu, Dar

Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambae kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amekabidhi Ofisi kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Joseph Edward Sokoine 

Makabidhiano ya ofisi yameshuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb).

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine akipokea ua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati walipokuwa wanamkaribisha katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Bw. Alex Mfungo. 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine akitambulishwa kwa baadhi ya wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa wizara na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Bw. Alex Mfungo wakati alipowasili katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine akiswasalimia baadhi ya wafanyakazi wa wizara katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimkabidhi ua Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam kwa makabidhiano ya Ofisi. Kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine. katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu mpya Balozi Joseph Sokoine. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam. 


Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu mpya Balozi Joseph Sokoine. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam. 


Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na  Katibu Mkuu mpya Balozi Joseph Sokoine wakiwa wameshikana mikono mara baada ya kukabidhiana ofisi  


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge mara baada ya makabidhiano ya ofisi

 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.