Wednesday, May 5, 2021

TANZANIA KUHAKIKISHA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA KENYA INAINUA UCHUMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kongamano la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania lililofanyika jijini Nairobi nchini Kenya alipokuwa kwenye ziara rasmi ya siku mbli nchini Kenya kwa mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akihutubia Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya lilifonyika jijini Nairobi tarehe 05/05/2021

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo huku wakisikilizwa na Waziri wa uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe , Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda, na Waziri wa Utlii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Mhe. Leyla Mohamed Musa Mawaziri hao walikuwa nchini Kenya kuhudhuriaa Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya

Baadhi ya viongozi kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi

Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la wafanyabiashara wa  Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na Marais  wa nchi za Kenya na Tanzania

Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la wafanyabiashara wa  Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na Marais  wa nchi za Kenya na Tanzania

Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la wafanyabiashara wa  Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na Marais  wa nchi za Kenya na Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameihakikisha jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya kuwa Serikali anayoiongoza itaendelea kuchukua hatua kuondoa vikwazo vya kibiashara vilivyopo ili kuimarisha sekta binafsi na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.

Mhe. Samia alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi nchini Kenya na kuhudhuriwa kwa pamoja na Rais Samia na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Me. Uhuru Kenyatta.

Amesema Serikali za nchi hizo zitahakikisha kunakuwa na sheria nzuri, uwazi, mifumo ya kodi inayoeleweka na mifumo thabiti ya Mahakama itakayoshughulikia kesi za biashara kwa haraka na uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji katika nchi hizo

Amesema kufanyika kwa Kongamano hilo kumewezesha kuwepo kwa majadiliano ya pamoja kati ya Sekta Binafsi na Serikali, wafanyabiashara wao kwa wao na kuelezea kuwa ni kitu kizuri kwani kinachangia juhudi za kuinua na kuimarisha ukuaji wa biashara na sekta binafsi kwa maendeleo ya nchi zote mbili

Mhe. Rais Samia amesema Tanzania itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanya biashara ili kuwawezesha wafanyabiashara kuendesha shughuli zao kwa amani na utulivu kwani Sekta binafsi ni muhimu katika ukuzaji wa uchumi kwa kutoa ajira, kuleta masoko, hufungua fursa mbalimbali na kuchagiza moyo wa ujasiriamali miongoni mwa wananchi.

Amesema Tanzania imedhamiria kwa dhati kuona Sekta binafsi imara inayoweza kukabiliana na changamoto za uchumi za dunia kupitia uanzishwaji wa viwanda na hivyo kuongeza ubora wa bidhaa zinazozalishwa nahivyo kutoa ajira na utajiri wananchi kitu ambacho wafanyabiashara wanatakiwa kukifikia.

Awali akizungumza katika Kongamano hilo Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta ameitaka jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya  kuchangamkia fursa za kibiashara ambazo hazijafikiwa katika nchi hizo ili kukuza biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuleta maendeleo kwa watu wake.

Amewataka Mawaziri wanaohusika na biashara kukutana na kutatua changamoto zinazokwamisha ukuaji wa biashara katika nchi hizo ili kukuza uchumi na kuinua maisha ya wananchi wa nchi hizo na kuongeza kuwa ana imani kuwa hayo yote yakifanyika kwa pamoja bila ya kushindana ni wazi kuwa watakaoibuka washindi ni wananchi wa nchi hizo.

Amesema wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza kwenda kuwekeza nchini Kenya bila ya kudaiwa viza za biashara ili mradi wafate sheria kanuni na taratibu zilizopo. Amewagiza Mawaziri wanaohusika na mgogoro uliopo eneo la mpaka la Taveta hadi Namanga wakutane ili kuona nanma ya kuondoa changamoto na kutoa wiki mbili mahindi yaliyokwama huko yawe yameondolewa.

Mhe. Kenyatta pia amewataka Mawaziri wa Afya katika nchi hizo kukutana na kuangalia namna ya kuondoa changamoto iliyopo sasa upimaji wa virusi vya Corona na kutaka vyeti vilivyotolewa katik nchi moja vitambuliwe katika nchi nyingine.

 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.