Friday, September 23, 2022

DKT MPANGO AHUTUBIA BARAZA. KUU LA UMOJA WA MATAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jijini New York nchini Marekani.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto) Waziri wa Nchi Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa Zanzibar Mhe. Masoud Ali Mohammed , Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu na Mama Dionisia Mpango Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais Dkt. Mpango katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijijini New York nchini Marekani 

 


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania inaamini diplomasia na meza za mazungumzo ni chombo bora cha kutatua migogoro duniani na kwamba nchi zina wajibu wa kuzingatia utatuzi wa migogoro kwa njia za amani ili kulinda ustawi wa watu watu na kuepuka athari zinazoweza tokana na migogoro duniani.

Mhe. Dkt. Mpango amesema hayo jijini New York alipohutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

“Tanzania inaamini kuwa diplomasia na meza za mazungumzo ndiyo chombo muhimu na ni vitu vikuu vya kuzingatia wakati wa  kutatua migogoro duniani, Mataifa yanapaswa kuzingatia kuwa yanahaki na wajibu wa kulinda maisha ya binadamu hasa watoto na wanawake lakini pia lazima wahakikishe ustawi wa watu wote , ni muhimu  kutafuta suluhu au kutatua migogoro kwa njia za amani, hii inasaidia kuepuka athari zitokanazo na migogoro hiyo kama vile ongezeko la bei za chakula na mafuta na kushuka kwa uzalishaji wa kilimo na viwanda duniani kote,“ alisema Dkt. Mpango.

Makamu wa Rais pia amepongeza juhudi za Umoja wa Mataifa katika kukuza lugha mbalimbali duniani ikiwemo tamko la kihistoria la Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi (UNESCO) lililoitaja "7 Julai" kuwa Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani na kuwezesha lugha hiyo kuadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani na hivyo kuitambua arsmi kimataifa.

Amesema Tanzania inajivunia kushiriki katika shughuli za kulinda amani ambapo imechangia Askari katika misheni 5 kati ya 16 zilizopo za kulinda amani duniani na kuahidi kuwa  itaendelea kuchangia zaidi iwapo itaombwa kufanya hivyo na kuiomba Umoja wa Mataifa kuongeza uungaji mkono wake kwa juhudi za kikanda katika za kujenga na kulinda amani.

 

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Dkt. Mpango amesema nchi za Afrika zinahitaji mabadiliko ya haki na utaratibu katika kufikia matumizi ya nishati mbadala kwa kuzingatia hali za Maisha ya watu wa bara hilo wenye changamoto mbalimbali za upatikanaji wa nishati hizo na kutoa wito wa kuondolewa kwa upinzani dhidi ya ufadhili wa kimataifa katika utekelezaji wa miradi ya mageuzi katika nchi za Afrika ambayo inalenga kutumia rasilimali ikiwemo gesi kwa ajili ya nishati na matumizi mengine katika kufikia maendeleo.

 

Amesema biashara ya hewa ukaa barani Afrika inapaswa kufanyika kwa uwazi na kuwanufaisha wananchi waliotunza mazingira na misitu inayozalisha hewa hiyo kwa matumizi ya dunia na kuongeza kuwa Tanzania ni moja ya iliyowekeza zaidi katika uhifadhi wa misitu ambapo asilimia 30 ya eneo la ardhi ya taifa hilo imehifadhiwa.

 Kuhusu mapambano ya ugonjwa wa COVID 19, Dkt. Mpango amesema amezishukuru nchi na jumuiya za kimataifa zilizoshirikiana na Tanzania kupambana na janga hilo kuanzia utoaji wa vifaa vya uchunguzi, dawa, programu za msaada wa chanjo, ambazo zimekuwa muhimu katika kushinda vita dhidi ya janga hilo na kuwezesha nchi kufikia asilimia 60 ya kuchanja watu wake hadi sasa na kuongeza kuwa kuchelewa kwa Afrika kupata chanjo za ugonjwa huo kunasisitza hitaji la Nchi za Kiafrika kufanya kazi pamoja katika ukuzaji wa masuluhisho asilia kupitia utafiti wa pamoja wa kisayansi.

Ametoa wito kwa mataifa kuweka vipaumbele vya vitendo hasa kwenye malengo ya maendeleo endelevu ambapo amayasihi mataifa kujitolea kufanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa na Nchi Wanachama wake, kwa nia ya ushirikiano na mshikamano wa kimataifa kuelekea mustakabali endelevu.

Thursday, September 22, 2022

BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA 12 WA MAWAZIRI MARAFIKI WA UN WA USULUHISHI

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula  akishiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula  akijadiliana jambo na washiriki wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi uliofanyika  jijini New York.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula  akiwa katika Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi ujijini New York.

Wenyeviti wenza wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi Uturuki na Finland wakiwasikiliza washiriki wa kikao hicho

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula  ameshiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York. 


Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mulamula amesema usuluhishi ni njia muhimu  katika kutatua changamoto za migogoro duniani na kuusihi Umoja wa Mataifa kuliingiza suala la usuluhishi katika mifumo ya utatuzi wa migogoro ya Umoja wa Mataifa.

Amesema usluhishi ukiingizwa katika mifumo ya utatuzi ya migogoro ya Umoja huo utasaidia shughuli za upatanishi na utatuzio wa migogoro na hivyo kuufanya Umoja huo kufikia lengo la utatuzi wa migogoro na kuifanya dunia kuwa sehemu salama .

BALOZI MULAMULA ASHIRIKI HAFLA NEW YORK

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Arika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameshiriki katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum kwa Mawaziri wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameshiriki katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum kwa Mawaziri wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameshiriki katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum kwa Mawaziri wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameshiriki katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum kwa Mawaziri wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Arika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameshiriki katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum  na Ubalozi wa Leinchestein kwa ajili ya Mawaziri Wanawake wanaoshiriki mkutano wa UNGA 77 unaoendelea jijini New York

DKT. MPANGO AKUTANA NA MKURUGENZI WA USAID

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power Jijiji New York Nchini Marekani

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango katika picha na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijiji New York Nchini Marekani


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na ujumbe wake katika picha ya pamoja na ujumbe wa Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijiji New York Nchini Marekani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power wakionesha zawadi ya picha ambayo Bi. Samantha alipatiwa na Dkt. Mpango baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijiji New York Nchini Marekani

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power, Mazungumzo yamefanyika Jijiji New York Nchini Marekani .
 
Katika kikao hicho Makamu wa Rais ametaja hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya afya hususani afya ya mama na mtoto ambapo ameelezea kuanzisha programu mbalimbali za kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa kushirikiana na wadau ikiwemo programu ya M- Mama. 

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa afya katika kuboresha huduma za afya na kuongeza juhudi katika ujenzi wa miundombinu ya afya ikiwemo vituo vya afya pamoja na hospitali.
 
Makamu wa Rais ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Uviko 19 ambapo nchi hiyo imetoa msaada wa dozi milioni  5 za chanjo ya ugonjwa huo.
 
Amesema serikali imeweka mkazo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuweka sera rafiki na kuunganisha taasisi zinazohusika na uwekezaji ili kuondoa urasimu kwa wenye nia ya kuwekeza Tanzania. Pia Makamu wa Rais ametaja juhudi zinazofanywa katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji pamoja na nishati ili kuwa na mazingira rafiki kwa wawekezaji.
 
Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Makamu wa Rais ameikaribisha USAID kushirikiana na Tanzania katika kupata teknolojia rafiki ya mazingira itakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi na kijamii bila kuathiri mazingira.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Maendeleo  ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za mageuzi hususani katika sekta ya afya na kilimo.
 
Bi Samantha ameongeza kwamba shirika hilo linaiunga mkono Tanzania katika kuifanya kuwa tegemeo la upatikanaji wa chakula kwa kuwezesha kupatikana kwa mbolea ya gharama nafuu itakayosaidia kuinua sekta ya kilimo.

Mhe. Dkt. Mpango yuko nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Dkt. Mpango atahutubia Mkutano huo  Alhamis tarehe 22 Septemba 2022.

 


Wednesday, September 21, 2022

DKT. MPANGO ASHIRIKI KIKAO CHA DEMOKRASIA UN

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki  kikao cha majadiliano ya  Demokrasia kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa jijini New York.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika kikao cha majadiliano ya Demokrasia kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa jijini New York.

 

kikao cha majadiliano ya Demokrasia kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa kikiendelea jijini New York

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki  kikao cha majadiliano cha  Ajenda ya Demokrasia jijini New York.

Kikao hicho kiliwakutanisha Wakuu wa Nchi, Serikali na Mashirika ya Kimataifa kimefanyika  kando ya  Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea Jijini New York nchini Marekani kiliandaliwa na Shirika la la Maendeleo  ya Kimataifa la Marekani (USAID).
 
Katika majadiliano hayo , Makamu wa Rais amesema serikali ya Tanzania imeweka mkazo katika mageuzi ya kuimarisha uchumi na utawala wa kidemokrasia kwa kuhakikisha sekta binafsi inashiriki vema katika ujenzi wa taifa pamoja na kushirikiana na wadau wa kimataifa katika kufikia maendeleo.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango yuko nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan



BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI KUHUSU MAZINGIRA NA MAENDELEO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika  Mkutano wa Mawaziri kuhusu Mazingira na Maendeleo ulioandaliwa na Uingereza na Rwanda na kufanyika  jijini New York tarehe 20 Septemba, 2022 ikiwa ni mkutano wa pembezoni wakati huu wa Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika  Mkutano wa Mawaziri kuhusu Mazingira na Maendeleo ulioandaliwa na Uingereza na Rwanda na kufanyika  jijini New York tarehe 20 Septemba, 2022

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika Mkutano wa Mawaziri kuhusu Mazingira na Maendeleo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika  Mkutano wa Mawaziri kuhusu Mazingira na Maendeleo ulioandaliwa na Uingereza na Rwanda na kufanyika  jijini New York tarehe 20 Septemba, 2022

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameshiriki  Mkutano wa Mawaziri kuhusu Mazingira na Maendeleo ulioandaliwa na Uingereza na Rwanda na kufanyika  jijini New York tarehe 20 Septemba, 2022 ikiwa ni mkutano wa pembezoni wakati huu wa Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani.

Akizungumza katika mkutano huo, Balozi Mulamula amesema Tanzania imeandaa mpango maalum  utakaoongoza namna ya kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira kulingana na ukubwa wa athari hizo katika kila eneo nchini.

Amesema mpango huo umepangwa kulingana na ukubwa wa nchi na hali tofauti za hewa katika kila eneo, misimu ya mvua,  upepo, kiwango cha joto na shughuli za kijamii na kiuchumi katika eneo husika.

Ameongeza kuwa kupitia mpango huo changamoto 12 kuu zitokanazo na uharibifu wa mazingira ambazo ni uharibifu wa ardhi, ukataji miti, upotevu wa viumbe hai, mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa vyanzo vya maji, uharibifu wa fukwe na viumbe vya majini, usimamizi wa taka, uchafuzi wa hewa na uvamizi wa viumbe zimebainishwa na hivyo itaisaidia nchi kuchukua njia stahiki kukabiliana nayo na kuyatafutia afua zake kikamilifu

Tuesday, September 20, 2022

DKT. MPANGO : TUJITOE UPYA NA KUONGEZA UWEKEZAJI KATIKA ELIMU

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mageuzi katika sekta ya elimu ulioshirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wakuu wa Taasisi na Mashirika na wadau wa elimu jijini New York , Marekani tarehe 19 Septemba, 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa waliposhiriki Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mageuzi katika sekta ya elimu ulioshirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wakuu wa Taasisi na Mashirika na wadau wa elimu jijini New York , Marekani tarehe 19 Septemba, 2022

 


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema  Mataifa yanapaswa kujitoa upya na kuongeza uwekezaji  zaidi katika sekta ya elimu ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na ya uhakika katika kuelekea mwaka 2030.

 

Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema hayo alipohutubia Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliobeba ajenda ya Mageuzi katika sekta ya elimu ulioshirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wakuu wa Taasisi na Mashirika na wadau wa elimu jijini New York , Marekani tarehe 19 Septemba, 2022

Makamu wa Rais amesema elimu ni sehemu muhimu ya ajenda ya maendeleo 2030 hivyo hakuna budi kuchukua hatua katika kuleta mabadiliko kwenye sekta hiyo na kuongeza kuwa kupatikana kwa elimu bora kutapunguza matabaka katika ajira pamoja na kipato baina ya wananchi.

 

Amesema Tanzania imechukua hatua mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kuanza mchakato wa kuboresha mitaala kwa kuwashirikisha wadau wa elimu, kuwekeza katika vyuo vya ufundi stadi na mafunzo , kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari na kuongeza bajeti ya wizara husika kufikia asilimia 18 ya bajeti yote ya serikali.

 

Amesema Serikali ya Tanzania inahakikisha upatikanaji wa elimu jumuishi kwa wote bila kujali jinsia , ulemavu na hali ya uchumi na kwa kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia Serikali  pia imedhamiria kuboresha usimamizi wa nguvu kazi ya walimu ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji bora kwa kuwajengea uwezo walimu na maofisa elimu kuhusu uunganishaji wa teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji  na uandaaji  wa masomo ya kidijitali.

 

Makamu wa Rais Dkt. Mpango, yupo nchini Marekani kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

 



BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO WA FINLAND

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa  na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe. Ville Skinnari jijini New York walipokutana jijini humo tarehe 19 Septemba 2022.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe. Ville Skinnari jijini New York walipokutana jijini humo tarehe 19 Septemba 2022.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe. Ville Skinnari jijini New York walipokutana kwa mazungumzo jijini humo tarehe 19 Septemba 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na timu yake kulia wakizungumza na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe. Ville Skinnari na timu yake kushoto jijini New York walipokutana jijini humo tarehe 19 Septemba 2022.


 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe.  Ville Skinnari jijini New York na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Findland.

 

Akizungumza katika kikao hicho Balozi Mulamula ameelezea nia ya Tanzania kushirikiana na Finland katika maeneo ya uendelezaji wa miundombinu, ICT, Kilimo na utunzaji wa mazao ya kilimo, nishati, gesi na biashara ya hewa ukaa.

 

Amesema Tanzania inaliona suala la miundombinu kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam kama jambo litakaloziunganisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini na hivyo kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa katika kanda hizo.

 

Amesema suala la uwepo na upatikanaji wa uhakika wa nishati za umeme na gesi ni miongoni mwa mambo ambayo Serikali inayatilia mkazo kwani inaamini kuwa yakikamilika yatavutia wawekezaji wengi nchini na hivyo kukukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla na ndio maana serikali inawekeza nguvu kubwa katika maeneo hayo

 

“Uwepo na upatikanaji wa uhakika wa nishati za umeme na gesi ni moja ya maeneo ambayo, Serikali inayatilia mkazo na yakikamilika yatavutia wawekezaji wengi zaidi nchini na  kukukuza uchumi wetu kwa ujumla na ndio maana serikali inaweka mkazo kukuza na kuimarisha maeneo hayo,” amesema Balozi Mulamula

 

Akiongelea suala la kuimarisha sekta ya kilimo nchini Balozi Mulamula amesema Serikali inalichukulia kwa umakini mkubwa suala hilo na ndio maana imekuwa ikiongeza bajeti yake kila mwaka ili kuifanya sekta hiyo ikue kwa kasi na hivyo nchi kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza nje na hivyo  kukuza kipato chake na cha wananchi kwa ujumla

 

Kuhusu eneo la ICT Balozi Mulamula amesema Serikali inatoa kipaumbele katika eneo hilo kwa kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya mafunzo ili kuwa na wahitimu wengi watakaokidhi mahitaji ya viwanda nchini na hivyo kuzalisha kisasa zaidi

 

Naye Waziri wa Finland Mhe. Skinnari amesema Finland iko tayari kushirikiana na Tanzania katika maeneo ya uendelezaji wa miundombinu hasa katika mpango wa upanuzi wa bandari ya Dar es salaam na kuifanya kuwa lango kubwa katika ukanda wa kusini  na Afrika Mashariki na kuangalia namna ya kuwa na maeneo ya kilimo bora zaidi kwa ajili ya uzalishaji wa chakula nchini.

 

Ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo ya biashara, uwekezaji na uendelezaji wa miundombinu ya ICT kwa kushirikiana na wadau wao mbalimbali. 

 

Mawaziri hao wako jijini New York kuhudhuria Mkutno wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani


UJUMBE WA TANZANIA UMESHIRIKI KONGAMANO LA WANAWAKE WA AFRIKA KATIKA UONGOZI

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (wa pili kulia) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Kongamano la Wanawake wa Afrika katika Uongozi lililofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 17 September jijini Durban, Afrika Kusini. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bi. Happiness Godfrey.

Pamoja na mambo mengine kongamano hilo pia limejadili juu ya kujenga uwezo wa wanawake kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Mtaalamu wa masuala ya Tafiti na Sera katika Taasisi ya Uongozi - Tanzania, Bi. Fortunata Makene akipokea zawadi ya Taasisi ya Wanawake wa Afrika kwenye Uongozi kutoka kwa Balozi wa Nigeria nchini Afrika Kusini, Mhe. H.M Manta kutambua mchango wa utaalamu wake katika masuala ya uongozi barani Afrika wakati wa kongamano hilo.

Majadiliano yakiendelea.

Ujumbe wa Tanzania ukiteta jambo baada ya mkutano.

Majadiliano yakiendelea.

 

Monday, September 19, 2022

DKT. MPANGO: DIASPORA ENDELEENI KUCHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa alipowasili kwa ajili ya kukutana na wanaDiaspora wa Tanzania wanaaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akiawa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto) na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston (kulia)  wakati wa kikao na wanaDiaspora wa Tanzania wanaaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston  akizungumza wakati wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula  akizungumza wakati wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani katiuka hafla iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York



 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na viongozi wa Jumuiya ya WanaDiaspora wa Tanzania waishio katika miji ya  New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani, baada ya Mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Jijini New York.

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Haji Suleiman (kushoto) akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Dkt. Elsie Kanza na Mkurugenzi wa Idara ya Multilateral Balozi Kahendaguza na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Balozi Swahiba Mndeme na mtumishi mwingine wa Ubalozi wa New York wakifuatilia mazungumzo ya Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mpango na Diaspora wa Tanzania walioko katika jiji la New York

Baadhi ya washiriki wa wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana na Diaspora wa Tanzania waliopo katika miji ya New York, Connect Cut na New Jesry nchini Marekani na kuwasihi kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Dkt. Mpango ametoa rai hiyo Jijini New York alipokutana kwa mazungumzo na viongozi pamoja na wanajumuiya ya wanadiaspora hao Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

Mhe. Dkt. Mpango amesema kitendo cha wanaDiaspora hao na wengine walioko duniani kote kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kinaendeleza jitihada za serikali za kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake.
 
''Muendelee kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kwani kufanya hivyo mnachangia maendeleo ya nchi yenu, mnaiunga mkono Serikali katika jitihada za kuleta maendeleo kwa watu  wake," alisema Mhe. Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango pia amewasihi wanadiaspora hao kufuatilia na kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini kwa manufaa yao binafsi, ndugu na jamaa na Taifa lao kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mpango amewataka wanadiaspora hao kuendelea kutafuta na kushawishi wawekezaji wengi kuja nchini na kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazopatikana nchini na kuendelea kuisemea vizuri nchi yao ya Tanzania.

Amewapongeza Diaspora wa Tanzania kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa wa uwekezaji hasa kupitia mfuko wa UTT Amis ambapo aliasema kuwa hadi kufikia mwaka 2021 wanadiaspora wa Tanzania walikuwa wamewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 3.9 za kitanzania katika mfuko huo.



DKT. MPANGO AKUTANA NA DKT KABERUKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akiwa katika mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akizungumza na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika picha na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka baada ya kukamilika kwa mazungumzo katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika picha ya pamoja na timu iliyoshiriki mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana kwa mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta maendeleo ya kiuchumi katika bara la Afrika na Tanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na jinsi taasisi hiyo inavyoweza kushirikiana na Benki ya Afroexim kuanzisha mfumo wa malipo wa pamoja Barani Afrika hasa ikizingatiwa utekelezaji wa Soko la Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Dkt. Mpango amesema kuanzishwa kwa mfumo huo kunaweza kufungua fursa nyingi na kurahisisha ufanyaji biashara katika Jumuiya mbalimbali kuanzia Afrika, SADC na EAC na kuongeza kuwa ni vyema  Taasisi hiyo na washirika wake kuangalia na kujipanga jinsi ya kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza kutokana na uanzishwaji wa mfumo huo

“Ni imani yangu kuwa kukamilika kwa mfumo huo kunaweza kuondoa vikwazo vingi visivyo vya kiforodha ambavyo nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliana nazo,” amesema Dkt. Mpango.
    
Naye Mwanzilishi wa Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Kaberuka amemhakikishia Dkt. Mpango utayari wa taasisi hiyo kushirikiana na Benki ya Afroexim kwa lengo la kuondoa vikwazo mbalimbali vya kibiashara ambavyo nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliana nazo na hivyo kuzuia ukuaji wa uchumi unaostahili.

Amesema wao kama wanaafrika wanaangalia njia na mbinu mbalimbali za kuwezesha ufanyaji biashara ndani ya bara la Afrika ili kujijengea uwezo wa kufanya biashara na hivyo kunufaika na rasilimali ilizonazo.

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango yuko jijini New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.