Friday, February 6, 2015

Rais wa Ujerumani amaliza ziara yake nchini

Rais Joachim Gauck, akipata heshima ya nyimbo ya taifa lake ikiwa ni sehemu ya kumwaga mara baada ya kumaliza ziara ya siku tano hapa nchini. Katika ziara yake Rais Gauck ametembelea Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha na kutembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti. Kupitia Ziara ya Rais wa Ujerumani kume dhihirisha Uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Ujerumani, ukizingatia Ujerumani inaisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta maji 
Gwaride likitoa Heshima kwa Rais Gauk 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Daudi Felix Ntibenda akiongozana na Rais Gauck wakati wa kuagana naye 
Rais Gauck na Mkewe wakitazama ngoma ya kitamaduni la kabila la Kimaasai
Waziri wa Maji Mh. Prof. Maghemba akiagana na Rais Gauck mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akiagana na Rais Gauck.
Mkurugenzi Msaidiza Idara ya Amerika na Ulaya, Bibi. Victoria Mwakasege akiagana na Rais Gauck
Raid Joachim Gauck akiagana na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Itifaki Bwa. James Bwana mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano 
Rais Joachim Gauck na Mama Schadt wakiwaaga viongozi mbalimbali kwa kuwapungia tayari wa kuanza safari ya kurujea nchini Ujerumani
Viongozi Mbalimbali wa Serikali kwa pamoja wakimwaga Rais Gauck kwa kumpungia mkono katika kiwanja cha Ndege cha KIA.


Picha na Reginald Philip.


Katibu Mkuu John Haule, Balozi Mpya Nairobi, Kenya

Bw. John Michael Haule












TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bw. John Michael Haule, kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya.
Kabla ya uteuzi huu, Bw. Haule alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 2011 hadi uteuzi huu.
Aidha, Rais Kikwete amemhamisha kituo Balozi Batilda Burian kutoka Nairobi, Kenya kwenda Tokyo, Japan kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Salome Sijaona ambaye anarejea nyumbani baada ya kustaafu.

Imetolewa na:

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
05 Februari, 2015

Thursday, February 5, 2015

Iranian Foreign Minister visits Tanzania


Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Cooperation together with his Iranian counterpart Hon. Mohammad Javad Zarif signing an agreement on Promotion and Protection of Investment between the two countries. The signing ceremony took place at Serena Hotel in Dar es Salaam during a two-day visit to Tanzania by Hon. Zarif.
The signing continues while Officers from Iran and Tanzania facilitates the Ministers. Standing right is Mr. Gerald Mbwafu, Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation
Hon. Membe and Hon.Zarif exchanging the agreement

.....Press Conference

Hon. Membe gives his remarks during a joint press conference held at Serena Hotel.
A cross section of Press Personnel listening to Hon. Membe's (not in the photo) remarks
Hon. Zarif  speaking to Journalists (not in the photo)
Ambassador Simba Yahya (C), Director of the Middle East Department in the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation and Assistant Director in the same Department, Mr. Elibariki Maleko (R) during a joint press conference between Hon. Membe and Hon. Zarif.
Another section of  delegates from both countries during a joint press conference.


.....Official talks

Hon. Membe in official talks with Hon. Zarif, mainly on strengthening bilateral relations between Tanzania and Iran
Hon. Zarif (4th from right) leading the Iranian delegation during official talks
Tanzania delegation during the official talks with the Iranian delegation.
=============================

PRESS RELEASE

Tanzania and Iran today signed a Memorandum of Understanding for cooperation at the end of a two-day visit by Iranian Foreign Minister, Hon. Mohammad Javad Zarif.

The agreement signed by Hon. Zarif and his host, the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Bernard Membe in Dar es Salaam, covers promotion and protection of Investments in areas ranging from education, health, agriculture, energy to manufacturing.

Hon. Zarif paid a courtesy call on President Jakaya Kikwete yesterday and expressed Iran's eagerness to expand economic cooperation with Tanzania and other countries in the Great Lakes Region. He was accompanied by Chief Executuve Officers of a number of big Iranian companies, including Mapna Group, which has exported power turbines to Russia.

The entrepreneurs yesterday held a business forum with their Tanzanian counterparts under the Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA).

During official talks today, Hon. Membe and Hon. Zarif also agreed to cooperate in fighting terrorism and establish mechanism for the exchange of prisoners.

Hon. Membe expressed hope that economic sanctions imposed on Iran over its uranium enrichment scheme would be eased following the move to review the sanctions against Cuba. He said Tanzania supported the Persian country's use of nuclear power for peaceful domestic purposes.

Hon. Zarif said another session was scheduled for this coming weekend in Munich under their negotiations with Western countries on the nuclear programme, adding that he hoped good news would come out of the meeting as long as Iran's right to decide its own affairs was respected.

Responding to questions at a press conference later, Hon. Zarif defended the hanging of hundreds of people in Iran, saying they were convicts of drug trafficking. "This has helped to deter drug trafficking from Afghanistan to Europe. Don't forget that drug money is also used to finance terrorism," he said.

He was reacting to criticism that the hanging of 852 people by Teheran in the past year was an affront to human rights. Hon. Zarif explained that there was an internal debate in Iran on whether the death penalty should be reviewed.

Hon. Zarif and his delegation flew to Zanzibar for talks with the President of the Zanzibar Revolutionary Government, Dr. Ali Mohammed Shein, afterwhich he left for home.


Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation.
05th February,2015

 



Wednesday, February 4, 2015

Matukio mbalimbali ya ziara ya Rais wa Ujerumani nchini


...Mkutano na Waandishi wa Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck wakati wa Mkutano wa Pamoja na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) uliofanyika Ikulu Dar es Salaam kuelezea malengo na mafanikio ya ziara ya Rais Gauck  hapa nchini.
Sehemu ya Wajumbe kutoka Ujerumani na Tanzania pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Mhe. Rais Kikwete  akiongozana na Rais Gauck mara baada ya mkutano wao na waandishi wa habari

....Dhifa ya Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck pamoja na Mama Salma Kikwete na Mama Schadt, Mke wa Rais wa Ujerumani wakati wa Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa Ikulu, Dar es Salaam kwa heshima ya Rais Gauck. Rais Gauck yupo nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tano.
Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Gauck wakitakiana afya njema na ushirikiano imara baina ya nchi zao wakati wa dhifa hiyo huku Mama Salma akishuhudia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal pamoja na Mke wake Mama Asha Bilal (mwenye kilemba) wakijadili jambo na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Diana Melrose wakati wa dhifa ya kitaifa Ikulu. Kulia ni Mkurugenzi wa EPZA Kanali Mstaafu, Joseph Simbakalia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiteta jambo na mmoja wa wajumbe waliofuatana na Rais wa Ujerumani waliposhiriki dhifa ya kitaifa Ikulu
Dhifa ikiendelea
Brass Band ikitumbuiza wakati wa dhifa hiyo
Rais Gauck na Mke wake Mama Schadt wakifurahia burudani ya ngoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (katikati) akimsikiliza mmoja wa wajumbe waliofuatana na Rais Gauck walipokuwa wakati wa dhifa ya kitaifa iliyofanyika Ikulu
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sophia Mjema akifafanua jambo kwa Balozi Melrose huku Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisikiliza
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimweleza jambo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizarani hapo, Bi. Mindi Kasiga huku Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizarani hapo akisiskiliza.

Picha na Reginald Philip














Tuesday, February 3, 2015

Mhe. Rais Kikwete ampokea rasmi Rais Gauck-Ikulu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea  rasmi Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akiwa ameongozana na mgeni wake Rais Gauck mara baada ya kumpokea.
Rais Kikwete na Rais Gauck wakipata heshima ya nyimbo za mataifa yao ikiwa ni sehemu ya mapokezi ya Rais Gauck. 
Kikosi cha jeshi kikipiga mizinga 21 kwa heshima ya Rais Gauck
Rais Gauck akikagua Gwaride la Heshima
Sehemu ya waandishi wa Habari wakiwa kazini
Sehemu ya umati wa watu  waliofika Ikulu kwa ajili ya mapokezi ya Rais Gauck
Rais Gauck akisalimiana kwa furaha na wanafunzi waliofika Ikulu kumpokea
Picha ya pamoja
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mama Schadt, Mke wa Rais wa Ujerumani
Mhe. Rais Kikwete akimpatia Rais wa Ujerumani, Mhe. Gauck zawadi ya picha ya michoro maarufu nchini ya "Tingatinga"
Rais Kikwete akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Rais Gauck
Rais Kikwete na Ujumbe wake wakiwa kwenye mazungumzo rasmi na Mhe. Gauck na Ujumbe wake (hawapo pichani) Kulia kwa Rais ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Memnbe (Mb.). Wengine ni Prof. Jumanne Maghembe (wa tano kushoto) , Waziri wa Maji.  
Rais Gauck (wa tano kulia) na Ujumbe wake wakati wa mazungumzo rasmi
Mazungumzo yakiendelea
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kushoto) akiwa na Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo rasmi kati ya Rais Kikwete na Rais Gauck (hawapo pichani)

 Picha na Reginald Philip